Hatimae leo nimeanza mazoezi

Poa poa mkuu
 
Unajua maana ya diet lakini?.
Mkuu sizungumzi diet kilugha na maana yake.

Nazungumzia diet na yale wanayofanya watu.

Mfano kuna mtu alikuwa anasema anafanya diet kwa kushindia juisi ya kabichi na madudu flani hivi.akapungua kilo vizuri sana kwa hiyo diet yake.lakini sasa akawa hawezi kuishi vile siku zoteeee ili abakie katika umbile lile.sasa ajabu si akarudi kwenye menyubyake ya zamani ambayo ndiyo anaiweza na ndiyo utaratibu wa maisha yake.
Akarudi kula chai chapati asubuhi.

Mchana ugali

Jioni wali.

Saivi kaongezeka tenaa ati asema anataka afanye diet,sasa hyo diet anayoisema na kuimaanisha huyu si anajisumbua tu au?
 
Aisee yani kwenye chukuchuku unatia karanga na njugu na korosho au vepe mkuu?
 
mi nazungumzia kujiwekea mfumo mzuri wa kula,unatakiwa ujue kila u achoingiza mwilini na faida na hasara zake.

Kujinyima kula kwangu ni big no nishajaribu nikafeli Ila nilichoweza ni kubadilisha aiana ya vyakula navyokula na vile vyakula vya starehe/ladha kuvizibiti.Mfano badala ya kunywa soda deile ukajitengea siku moja kwa wiki ndio unakunywa,badala ya kula nyama kila siku ukawa unakula mara moja au mbili kwa wiki,badala ya kukarangiza sana masotojo ukawa unakula zaidi michemsho.kujipangia nini unakula siku nzima badala ya kula kila kinachopita mbele yako.Badala ya kuishi ili ule unatakiwa ule ili uishi.Usichanganye chakula lishe na chakula starehe kinachofurahisha tu ulimi na pua yako lakini kikiingia mwilini kinakutesa.u dig?
 
Mimi nina kakitambi kana ni nyemelea yani kameniganda mazorzi napiga na kuacha. sasa fomula gani nitumie kukatoa bila kuathiri kilo nilizo nazo.

Kuna kipindi nilifanya extensive diet nikapungua tena ikawa shida.

Ifuatayo ni milo yangu kwa siku naomba ushauri wapi nipunguze:

Asubuhi
1 Viazi mviringo vya kucheemsha
2. mayai ya kukaanga 2 au matatu (spanich egg)
3. soseji 3 ( za kuku ama kitimoto)
4. Kahawa na maziwa vikombe kimoja na nusu
5. fresh juisi glasi moja (sometime inakuwa ya tikiti au nanasi au papai. siku nyngine inakuwa mix
6. vipande viliwi au kimoja cha omellette
7. matunda (ndizi moja, nanasi vipande 4, embe
8. cookie moja.

Mchana
1. Hapa mara nyingi nakula wali na nyama ya ngombe na kuku katika mapishi mabali mabli
2 matunda na juisi fresh.

Usiku
1. nakula wai ama mashed potatoes, nay red meat katika mapishi mablimbali
2. Bia 2 - 4

NB: mboga za majani napata kwa nadra sana maana hazipatikani kila siku.
 
Hii ndo pooa sasa.kuliko diet wanazozisema watu za kushindia juisi wakati hawawezi kudumu hivyo maisha yao yote.ndo mana nikasema diet nikikusudia hizi za majuisi juisi ni ubabaishaji tu.
 
😲😲🀐🀐🀐 mkuu hapo kwenye breakfast ni wewe peke yako au unakuwa una wageni waalikwa kwa fasinade ya tumbo???
 
punguza red meat na ngano,pia hakikisha mlo wa usiku unakula mapema atleast masaa manne kabla ya kulala.Kunywa maji walau glasi moja robo saa kabla ya kula na robo saa baada ya kula,hakikisha unakunywa walau lita mbili za maji kwa siku.Pia chakula unachokula kisipikwe na mafuta mengi na ikiwezekana kula chukuchuku.
 
kwenye matunda hapo pia uwe unabadilisha badilisha.
 
Kwenye chukuchuku hapo ni tatizo.
Na hilo la kula masaa manee kabla ya kulala ni gumu kuliko kutokula kabisa.
 
Ha ha ha ha "tuna ambiana mambo ya kitapeli tu " hii sentensi imenifurahisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…