Iran na Oman zinaripotiwa kukaribia kufikia makubaliano mapya ya kuruhusu usafiri wa meli kurejea katika Mlango-Bahari wa Hormuz, huku nchi hizo mbili zikitarajiwa kugawana udhibiti wa njia za kupita pamoja na mapato yatakayokusanywa kupitia kile kinachoelezwa kuwa “ada za huduma.”
Kwa mujibu wa maafisa wa Iran na Marekani walioelezwa kufahamu mazungumzo hayo, meli zinazoingia Ghuba ya Uajemi zitatumia njia iliyo karibu na pwani ya Iran na kusimamiwa na Tehran. Meli zinazoondoka Ghuba zitatumia njia ya upande wa Oman, karibu na pwani ya nchi hiyo.
Soma zaidi:Rais wa Marekani Donald Trump aagiza boat za Iran zilizoko mlango bahari wa Hormuz zizamishwe
Maafisa wawili wa Iran wamesema meli hazitatozwa ada kwa jina la “ushuru wa kupita,” bali zitalipa ada za huduma zinazohusishwa na ulinzi wa mazingira, usalama wa meli na mizigo, alama za kuongozea meli, wafanyakazi na shughuli nyingine za usimamizi wa baharini.
Mapato yatakayopatikana kupitia ada hizo yanatarajiwa kugawanywa sawa kati ya Iran na Oman. Mfumo huo unalenga kuipa ada hiyo sura ya malipo ya huduma badala ya ushuru wa lazima wa kutumia njia ya kimataifa
Source:Simulizi na sauti