Hatimae Naona Kama 1+1 = 2 Inaleta Maana

Bhana kiukweli Supporters wa Domo huwa wananiboa sana... mbona majority mna nondo kali namna hii??!!! Sasa ukimsoma brave one, The bold, kedrick, samsun hadi moyo unasimama... honestly speaking; sio unafiki wala nini... I do appreciate you guys-- sio leo but since then!

Sasa na wewe Sambusa kavu mbona leo ndo nakuona kwa mara ya kwanza hapa jamvini lakini una nondo mzito namna hiyo?! Kumbe ndo maana Team Kiba huwa hawakawagi kumwaga mipovu; manake wakigeukia huku, nondo... wakigeukia kule nondo...

Tena mkuu Sambusa kavu wacha nikung'ate sikio! Hii mada mimi wala sikuwa na time nayo... in short, nilishaipotezea! Lakini huyo huyo Nifah anayesema "Kama mtu makini sikutegemea kabisa uingie katika huo mkumbo. " Lakini ni yeye yeye ndie aliniingiza kwenye hii mada... Nifah huyu hapa: Akani-mention hapo chini!! Lakini kama nilivyosema, sikuwa interested na hii mada; ndo maana nikajibu:
Nifah akaendelea kunitaafuta cha rohoni... huyu hapa tena Nikaona alaa, basi sawa... nikafungua thread mzima badala ya kuchangia zilizopo na nikam-tag Nifah! Nifah kuja kusoma; salalee... anakuta nimepiga kombora Ikulu; ndipo akaanza kulia lia: Anasema nimeshindwa kudhibiti hasira wakati anajua kabisa huu mjadala niliupotezea na wala sikuwa na time nao hadi alivyoniita mwenyewe! Anasema nimetumia muda mwingi kumkashifu Ommy Dimpoz huku akisahau baada ya mara ya kwanza kumwambia naona hii mada inawafaaa Team Kiba lakini ni yeye yeye akajibu kwamba anazungumzia
Tokea hili sakata limeanza (na lilikolezwa juzi baada ya chibu kuitwa xxl kueongelea hili) umekuwa kimya sana.
Sasa sijui amesahau kwamba tangia Chibu aende XXL mada yenyewe imetawaliwa na kuchafuana! Sijui jana hajamsikia Dimpoz alivyotoa maelezo yenye kutafsirika Diamond achunge mdomo manake anaweza kukuta Ommy Dimpoz analala na mama yake! Na asilimia kubwa ya maelezo ya Dimpoz ni jinsi Diamond alivyokuwa anambania... nikajaribu kuonesha hivi unapokalalamika kwamba Diamond alimtoroka badala ya kumfanyia connection Marekani... wakati kuna kila dalili kwamba Diamond hakuwa na uwezo huo! Ndipo nikahoji; hivi huyu Dimpoz ni kweli alikuwa anataka collabo huko Marekani au alikuwa na yake hasa ukizingatia ana kashifa za kupumuliwa?!Hivi mtu ndo kwanza ana nomination moja ya BET ndo awe na connection Marekani?!

Lakini anyway, I know Nifah for a long time now... na ni moja ya marafiki zangu wa mwanzoni kabisa hapa celebrities!! In short, hakutarajia kwamba ningegonga Ikulu kwa kutumia atomic bomb!!! Lakini hapa pia ama alisahau au hajui kwamba mimi huwa naanzisha mada mara chache sana... mimi ni mchangiaji zaidi kuliko kuwa mwanzishaji! Sasa mtu asiyeandika andika siku akiandika; kombora linaweza kuangukia popote pale hasa unapoandika mada ambayo wala haikuwapo kichwani mwako!!!

Sasa Nifah rafiki yangu; hebu nisaidie jambo moja! Assume una braza wako halafu huyo braza wako mimi ni rafiki yangu! Nafika kwenu kuwaaga kwamba kesho naenda Mbeya; mara braza wako na yeye anataka tufuatane...! Anaulizwa unataka kwenda kufanya nini Mbeya; anajibu anataka akachukue korosho..... aaaaaaaaaaargh! Mbeya na korosho wapi na wapi?! Hivi hapo kaka ako atakuwa anataka korosho au ana yake!!!! Halafu nikimtoroka, ndo utanilaumu????!!!!!
 
Hahahaaa... mi hata akininunia mwisho wa siku tutaelewana tu manake hapo zamani ilibaki kidogo tu niulizie kwao nikatoe posa kabisa sema ndo hivyo tena akanikataa!!! Anyway, Nifah, hivi ulishajibu swali husika kwa faida ya muulizaji na samsun?! Halafu kuna mtu humu... ama The bold au brave one nilimuomba ani-tag mara Nifah atakapojibu maswali 3 aliyokuwa ameulizwa! Hey guys, The bold/brave one, mbona bado hujani-tag?! Au bado hajajibu?!!
 
Huna lolote, sema kitofa kimekungia barabara, basi!! Dimpoz hajazungumzia kazi wala nini bali kazungumzia kitu kinachoweza kutafsirika kwamba ni roho mbaya ya Chibu! Kalia lia sana kuhusu collabo za akina Davido na collabo ya US... na yote hayo nimeyazungumzia!! Na kwavile ulisema nianzie siku ya Diamond kuwa XXL nami nikachukua ya Diamond nikaja kuchanganya na ya Dimpoz, chemical reaction iliyotokea hapo ni HEAT+COMBUSTION!

Halafu unasema linapokuja suala la Chibu... kwani hapa ni mada zipi zinazotawala kama sio hizo hizo za Chibu na Kiba!!! By the way, ni kipi alichoongea Dimpoz ambacho sijakizungumzia?!

Halafu kwenye ligi mtutoe knockout nyinyi? Team Kiba kwenyewe wanaojua kuandika ni wewe na Mdakuzi peke yake... hizo knockout zitokee wapi!!!

Halafu mbona hujanijibu kuhusu kaka ako atakayekuwa ananililia twende wote Mbeya eti anataka akachukue korosho?!
 
WORD
 
Ni wivu chuki na misifaa tuuu ya domo mfyuuuuu na wanaomsapoti wote wanapumuliwa na wao nyambafff zao.........sisikilizi tena nyimbo za domo
 
Huku watoa hoja wapo wengi sana labda kama upo addicted na magazeti ndo umeniona mimi na The bold peke yake... manake wote tuna udhaifu wa kuandika magazeti kama ilivyo kwa Mdakuzi ukifuatia na wewe mwenyewe!! kedrick nae ni full nondo sema robo magazeti! samsun nae ni full nondo sema yeye sio mwandishi... brave one full nondo na magazeti hayamshindi! Halafu kuna Chinga One, Paula kilaki!! List ni ndefu! Lakini huko kwenu ukitoa wewe na Mdakuzi, kinachobaki ni ukame mtupu!

Kuhusu mfano wangu unaswihi sana tu sema unajifanya hauswii!!! Wewe unang'ang'ania uende Marekani na mtu akakutafutie kollabo wakati unajua kabisa uwezo huo hana na hata angekuwa nao collabo haitafutwi kienyeji namna hiyo; sasa si sawa na kung'ang'ania kwenda Mbeya kuchukua korosho wakati unajua kabisa Mbeya hawalimi korosho!!!!!
 
Mkuu kwakuwa we mshabiki was dai una haki kuona hivyo ila mi wote siwakubali kwa kushabikia ccm tukubaliane yaliomo yamo.
 
Mkuu kwakuwa we mshabiki was dai una haki kuona hivyo ila mi wote siwakubali kwa kushabikia ccm tukubaliane yaliomo yamo.
Burudani ni burudani na siasa ni siasa jombaa!! Hata pale Billiz, ingawaje ni ya Mwenyekiti wa CHADEMA lakini wapenda burudani wa CCM hawawezi kuacha kwenda eti kisa panamilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA!!! But all in all, muziki ni biashara... biashara haichagui mteja!
 
Nani kati yao alieanza kutoka nje ya mada hadi kupumuliana kisogoni?kwangu dai kumkimbia dimpo haina excuse Mara zote alizokimbia,kwa nilivyoelewa swala la mpiga sexaphone dai hakuwa nalo ila alilikuta kwa dimpoz akalifanyia Kaz fasta ubaya ni kuwa walikutwa,kwa nilivyoelewa ni kama dimpoz alimuamini dai mia mia ila dai ni mjanja hakumuamini the same,dai ni mjanja anajua kutambua wazo zuri kwa haraka nadhani ndo mana yuko hapo,unajua kimsingi binadamu tunatakiwa kuwa hivyo ili utoke na wasanii wengine waache kubweteka na mafanikio madogo wanayopata.
 
Mkuu maana yangu Niko neutral katika hili nilitaka kutoa mchango wangu kwa jinsi nilivyoelewa,na nilidhani kuna watu neutral tuchambue bila timu tuone kama kuna tija tushauri nini wafanye hawa watu.
 
Sasa suala la kwamba Dimpoz alimuamini sana Dai linatoka wapi?! Kwani huyo Dai alifanya nini cha ajabu?! Au huyo mpiga saxophone alitoka nje ya nchi kwamba baada ya kufanya kazi na Diamond; hapo hapo angepanda ndege na kuondoka na ingekuwa ngumu kurudi tena!! Na uzuri zaidi, alivyofika studio huyo jamaa bado alikuwepo! Kwanini hakufanya nae? Au kwanini wasingeweka appointment cku nyingine? Tena studio ni mambo ya kawaida sana... unaweza ukaenda studio leo na kutengenezewa beat; unarudi siku nyingine ukaingize vocal unakuta beat keshapewa mtu mwingine!!

Ukitaka kuwa mkweli; huchelewi kuuona ubinafsi wa Dimpoz kwamba, kama kitu ame-propose yeye basi hataki mwingine afanye na akifanya anasusa! YOTE aliyoyalalamikia alikuwa na uwezo wa kuyafanya bila kuathirika chochote kile!

Kuhusu nani kaanza kutoka nje ya mada-- kutoka nje ya mada kivipi? Kama kuongea kwenye media Dimpoz ndo kaanza kwamba kuna watu wanajidanganya... wananunua views ili ionekane videos zao zinaangaliwa sana!! Ikapita kama wiki moja Diamond ndo akaandika "Mtu unamchukia mwanaume mwenzako kisa kakataa kukupumulia...!"

Anyway, hapa naomba unijibu swali moja: Kwa uonavyo wewe, Je, unaamini Diamond wa 2014 alikuwa na connection USA za kumwezesha kumtafutia mtu collabo?

Nimekuuliza hilo swali kv umerudisha hoja ya kumkimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…