Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akani-mention hapo chini!! Lakini kama nilivyosema, sikuwa interested na hii mada; ndo maana nikajibu:Jamani wale team diamond vingunge wenyewe mko wapi?
Mbona mmekaa kimya sana katika hili sakata ilhali mpo humu?
Tunahitaji kusikia kutoka kwenu kuhusiana na hili,sio sawa kabisa kukimbia jukwaa kwa issue kubwa namna hii inayomhusu mnayemtetea huku kila uchwao.
Siku 2/3 hizi mmetuachia jukwaa,tunawamisssssss
cc Chinga One [COLOR=#ff0000][B]chige[/B][/COLOR] The bold
Nifah akaendelea kunitaafuta cha rohoni... huyu hapa tenaSasa kukimbia nini hapa nifah? Kwanza ni post ya saa 9:18 PM nami ndo kwanza naiona 2:54 AM; karibu saa 6 baadae na kama usingeni-mention; wala nisingeiona simply because niliona notification yako na ya atoto; nikaona hawa "wangu", ngoja ni-login nijue kulikoni... kwahiyo haina kukimbia bhana!!
Baada ya hiyo intro; nimesoma post husika... mbona naona kama ni wa kujibu ni mashabiki wa Ommy Dimpoz kuliko wa Diamond? Manake hapo Diamond kasema yake... wanaopaswa kujibu au kutetea ni mashabiki wa Dimpoz...
Nikaona alaa, basi sawa... nikafungua thread mzima badala ya kuchangia zilizopo na nikam-tag Nifah! Nifah kuja kusoma; salalee... anakuta nimepiga kombora Ikulu; ndipo akaanza kulia lia:Aaaaah chige acha siasa zako wewe. Sijaongelea hii post (majibu ya diamond kuhusu alichokisema Ommy ktk interview)
Bali namaanisha sakata hili kwa ujumla. Tokea hili sakata limeanza (na lilikolezwa juzi baada ya chibu kuitwa xxl kueongelea hili) umekuwa kimya sana.
Anasema nimeshindwa kudhibiti hasira wakati anajua kabisa huu mjadala niliupotezea na wala sikuwa na time nao hadi alivyoniita mwenyewe! Anasema nimetumia muda mwingi kumkashifu Ommy Dimpoz huku akisahau baada ya mara ya kwanza kumwambia naona hii mada inawafaaa Team Kiba lakini ni yeye yeye akajibu kwamba anazungumziaChige,wewe ni mtu makini lakini katika hili umekurupuka.
Umeshindwa kuzidhibiti hasira zako juu ya hili saga badala yake umemshambulia Ommy katika skendo inayomtafuna. Mada yako 50% imelenga kumchafua Ommy na sio kuzungumzia masuala ya kikazi ambayo ndizo lawama alizozitoa Ommy. Kama mtu makini sikutegemea kabisa uingie katika huo mkumbo.
Sasa sijui amesahau kwamba tangia Chibu aende XXL mada yenyewe imetawaliwa na kuchafuana! Sijui jana hajamsikia Dimpoz alivyotoa maelezo yenye kutafsirika Diamond achunge mdomo manake anaweza kukuta Ommy Dimpoz analala na mama yake! Na asilimia kubwa ya maelezo ya Dimpoz ni jinsi Diamond alivyokuwa anambania... nikajaribu kuonesha hivi unapokalalamika kwamba Diamond alimtoroka badala ya kumfanyia connection Marekani... wakati kuna kila dalili kwamba Diamond hakuwa na uwezo huo! Ndipo nikahoji; hivi huyu Dimpoz ni kweli alikuwa anataka collabo huko Marekani au alikuwa na yake hasa ukizingatia ana kashifa za kupumuliwa?!Hivi mtu ndo kwanza ana nomination moja ya BET ndo awe na connection Marekani?!Tokea hili sakata limeanza (na lilikolezwa juzi baada ya chibu kuitwa xxl kueongelea hili) umekuwa kimya sana.
Hahahaaa... mi hata akininunia mwisho wa siku tutaelewana tu manake hapo zamani ilibaki kidogo tu niulizie kwao nikatoe posa kabisa sema ndo hivyo tena akanikataa!!! Anyway, Nifah, hivi ulishajibu swali husika kwa faida ya muulizaji na samsun?! Halafu kuna mtu humu... ama The bold au brave one nilimuomba ani-tag mara Nifah atakapojibu maswali 3 aliyokuwa ameulizwa! Hey guys, The bold/brave one, mbona bado hujani-tag?! Au bado hajajibu?!!Wadau tupo pamoja na nyinyi,mimi sitamuuliza nifah NASUBIRIA HILI JIBU maana mimi anaichukia avatar yangu kama ananijua kwa kuniona. MAANA UKIJENGA HOJA KUHUSU SHUTUMA ANAZOPEWA MOND BASI WEWE HUNA AKILI KWAKE,ILA ONGEA KWA KUMPONDA MONDI HATA PICHA YA KIKOMBE ATAKUWEKEA,JARIBUNI KUANGALIA HOJA ANAZOZIUNGA MKONO ZINAMUONGELEAJE MOND NDIO MUTAMJUA MTU HUYU.Na nawahakikishia ukiwa na tabia ya KILA MARA kumkosoa anapomponda MOND basi nanyi muda si mrefu atawanunia. ANAPANIKI KWA HARAKA SANA.
Huna lolote, sema kitofa kimekungia barabara, basi!! Dimpoz hajazungumzia kazi wala nini bali kazungumzia kitu kinachoweza kutafsirika kwamba ni roho mbaya ya Chibu! Kalia lia sana kuhusu collabo za akina Davido na collabo ya US... na yote hayo nimeyazungumzia!! Na kwavile ulisema nianzie siku ya Diamond kuwa XXL nami nikachukua ya Diamond nikaja kuchanganya na ya Dimpoz, chemical reaction iliyotokea hapo ni HEAT+COMBUSTION![emoji23] [emoji23] [emoji23] chige acha mambo zako bwana.
Ni kweli nilikuita uje kuongelea hili saga.
Badala yake wewe umeanza kumkandia Ommy na hizo maneno za Chibu wenu.
Ah...sie waarabu wa Pemba bwana,ungesema tofauti na haya uliyonena ingekuwa ajabu sana.
Pamoja na umakini wako lakini linapokuja suala la Chibu uko tayari hata kupoteza ile heshima yako uliyojijengea kumtetea hata kama kateleza.
Msijinadi sana na hiyo team yenu,watu wetu wengi wamepotea jukwaani kwa muda sasa.
Unakumbuka enzi za 'ligi' zetu tulivyokuwa tunawatoa KO daily?
Umesahau nondo za Mdakuzi?
Basi tu zama hazirudi.
WORDChige,wewe ni mtu makini lakini katika hili umekurupuka.
Umeshindwa kuzidhibiti hasira zako juu ya hili saga badala yake umemshambulia Ommy katika skendo inayomtafuna.
Mada yako 50% imelenga kumchafua Ommy na sio kuzungumzia masuala ya kikazi ambayo ndizo lawama alizozitoa Ommy.
Kama mtu makini sikutegemea kabisa uingie katika huo mkumbo.
Turudi katika hoja zako za connection na collabo.
Hivi unawezaje kusema kwamba Diamond asingeweza kumfanyia connection Ommy?
Diamond alikuwa anaenda katika tuzo za BET (kama sikosei)
Hivyo jina lake lilikuwa ktk vichwa/vinywa vya waliokuwa wengi...ile si connection kubwa tayari?
Diamond hakwenda kama ambavyo angeenda Ommy...yeye alienda kama star.
Hivyo endapo angeenda na Ommy hata ile kushake hands na akina Kanye West ingekuwa connection tayari.
Pia kuhojiwa kule na Karueche kungekuwa connection na hizo ndizo fursa zenyewe.
Katika hili Diamond anabeba lawama ya roho mbaya na wivu.
Hapendi wengine wapate japo kiduchu ya kile apatacho.
Hukuona Ali Kiba akienda na Baraka South Afrika?
Unadhani alienda nae kuuza sura?
Ile ni connection, hata kukutanishwa na Sauti Sol ni connection tayari.
Collabo hapa namuelewa Ommy,hata kama ningekuwa mimi nimemueleza rafiki mpango wangu kesho nikakuta keshaupandia dau ule mpango ingeniumiza na kunivunja moyo wa kuendelea na ule mpango.
Ni Ommy anayejua aliumia kiasi gani,hivyo kuipotezea kwake collabo na Davido huenda ana sababu zake nyingi na kulalamika huko ni sahihi.
Ni vyema tukaweka mihemuko na mahaba yetu kando juu ya tunaowashabikia wanapoteleza na kusema ukweli.
Kama ukweli ni vigumu kuusema basi ni busara zaidi kukaa kimya.
Period
Huku watoa hoja wapo wengi sana labda kama upo addicted na magazeti ndo umeniona mimi na The bold peke yake... manake wote tuna udhaifu wa kuandika magazeti kama ilivyo kwa Mdakuzi ukifuatia na wewe mwenyewe!! kedrick nae ni full nondo sema robo magazeti! samsun nae ni full nondo sema yeye sio mwandishi... brave one full nondo na magazeti hayamshindi! Halafu kuna Chinga One, Paula kilaki!! List ni ndefu! Lakini huko kwenu ukitoa wewe na Mdakuzi, kinachobaki ni ukame mtupu!Ndioooo umesahau ulikuwa peke yako mwenye kuweza kujenga hoja?
Bahati yako,shukuru sana ujio wa The bold.
Na kama kuna kitu kimeniuma basi ni huyo bwana kuwa upande wenu,natamani angekuwa kwetu,mngetukomaaa
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Au natamani Mdakuzi arudi halafu huku niko nae halafu huko wewe na The bold.
Mbona jukwaa lingewaka?
Kumepooza sana huku siku hizi.
Kama sio hili bifu jipya tulishasahauliana kabisa.
Aaaah chige bhana huo mfano sio,ndio maana nimekausha.
Hauendani na kilichopo mezani.
[emoji126] [emoji126] [emoji126]
Mkuu kwakuwa we mshabiki was dai una haki kuona hivyo ila mi wote siwakubali kwa kushabikia ccm tukubaliane yaliomo yamo.Hilo la saxophone nimeona halina maana na linafanana na issue ya kina Davido! Kwa sababu, ikiwa Dimpoz alikubaliana na mtu ampigie saxaphone lakini wiki moja baadae akamkuta Diamond na huyo mtu... sasa tatizo lipo wapi hapo? Kwani baada ya kumalizana na Diamond, Dimpoz nae asingeweza kuendelea na hizo program ya saxophone? Sasa nini kilimfanya aachane na hilo suala? Yaani kwavile tu Diamond "alimuwahi?!" au?! Tangu lini mpiga saxophone ikawa akishampigia mtu mmoja hawezi tena kumpigia mwingine?Mbona inaonesha kana kwamba, endapo idea ya jambo katoa yeye, basi mwenzake akifanya kabla yake tu; Dimpoz anasusa!!!!
Wanjera ilikuwa released March 2015 na hapa tayari mawasiliano yalikuwa yameshavurugika kabisa baada ya Ommy Dimpoz kwenda na Wema South Afrika ku-shoot video ya Wanjera! Sasa sijui ni utoto au ujinga, zikavuja picha za Wema na Ommy Dimpoz wakiwa kwenye pozi za kimahaba! Dimpoz mwenyewe anasema hapo Diamond alipatia sababu tu!!!
View attachment 439389
Ommy Dimpoz akakanusha na kusema hakuna mahaba yoyote kati yao! Ingawaje wakati huo Wema na Diamond walikuwa wameachana lakini kila mmoja anafahamu bado moyo wa Diamond ulikuwa kwa Wema! Sasa sijui walifanya hivyo ili kumrussha roho Diamond; wenyewe ndo wanajua! Sijui ni Wema ndie alipiga na kuvujisha ili kumuumiza Chibu; wenyewe ndo wanajua! Na baada ya hapo; kila kitu kikavurugika jumla!!! Na wakati hayo yanatokea; Diamond alikuwa hajapata tuzo yoyote zaidi ya Channel O!!! Ilikuwa ndo anaanza ku-struggle kutoka na kujitanua Afrika na wala sio kidunia! Remember, hapo hata ngoma ya Nana ft Mr. Flavor ilikuwa bado haijatoka!
Kuhusu mbona la kwamba "alivyokuwa anamtoroka hata kama kaulizwa kama anasepa mbele kesho...!" Sasa hilo si ndo la US... Diamond alianza kusema hana uhakika kama ataenda lakini ghafla, akashitukia keshaondoka! Na Dimpoz kazungumzia tuzo ilikuwa kufuata tuzo za AFRIMMA ambazo! Tuzo pekee za AFRIMMA wakati Diamond wapo pamoja na Dimpoz zilikuwa ni za 2014 ambapo Diamond hakukuwa na influence yoyote! Hata BET aliyotaja Ommy Dimpoz; by the time Diamond ilikuwa ndo kwanza:
View attachment 439400
Sasa hivi kweli inaingia akilini, mtu amekuwa nominated kwa mara ya kwanza; na hata kushinda hakushinda lakini pamoja na yote hayo eti alishakuwa na connection Marekani lakini akamtoroka mwenzake!!!!
Burudani ni burudani na siasa ni siasa jombaa!! Hata pale Billiz, ingawaje ni ya Mwenyekiti wa CHADEMA lakini wapenda burudani wa CCM hawawezi kuacha kwenda eti kisa panamilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA!!! But all in all, muziki ni biashara... biashara haichagui mteja!Mkuu kwakuwa we mshabiki was dai una haki kuona hivyo ila mi wote siwakubali kwa kushabikia ccm tukubaliane yaliomo yamo.
Nani kati yao alieanza kutoka nje ya mada hadi kupumuliana kisogoni?kwangu dai kumkimbia dimpo haina excuse Mara zote alizokimbia,kwa nilivyoelewa swala la mpiga sexaphone dai hakuwa nalo ila alilikuta kwa dimpoz akalifanyia Kaz fasta ubaya ni kuwa walikutwa,kwa nilivyoelewa ni kama dimpoz alimuamini dai mia mia ila dai ni mjanja hakumuamini the same,dai ni mjanja anajua kutambua wazo zuri kwa haraka nadhani ndo mana yuko hapo,unajua kimsingi binadamu tunatakiwa kuwa hivyo ili utoke na wasanii wengine waache kubweteka na mafanikio madogo wanayopata.Unaona sasa double standard hizo...! Wewe unaona ni sawa ukisema Mama yake Diamond analiwa na Makuli wa Sokoni Tandale lakini hapo hapo unahoji Diamond kusema "Mwanaume anapumuliwa kisogoni...!" Nadhani hata mfano wa Dimpoz kwamba anaweza kumwita mtu anapumuliwa kisogoni kumbe mtu mwenyewe ni baba ake! Na leo hapa ndo nimepata habari kwamba; kumbe ile mitusi mizito mizito waliyotukanwa familia mzima ya akina Diamond; Dimpoz nae aka-LIKE kuonesha amependezewa na hayo matusi! Lakini pamoja na yote hayo; mwenzake amejikita kwa Dimpoz... hajamtolea mfani mama ake wala dadake! Ndo maana nikatangulia kusema kwamba wanadhani kuna wengine wakidhalilishwa ni sawa tu lakini waki-fight back; tayari tatizo!!!!
Sasa kukujibu swali lako; kwani Diamond ni kichaa aibuke from nowhere akamtukana Dimpoz? Kwanini hakumwambia anapumuliwa wakati zilipovuja picha za Dimpoz na Wema?! Sasa kama amefanya au anaamini amefanya mambo ambayo mwanaume hastahili kufanya kwa mwenzake; obvious usishangae kuambiwa anapumuliwa! Kama watu wanalipa mamilioni kutengeneza video kuvutia watu halafu mwisho wa siku unakula "views" za kutosha halafu anatokea mwingine anasema unanunua views; hizo ni kauli za watu wanaopumuliwa manake huwa hawaheshimu hustles za watu na kinyume chake watazihusisha na mambo ya kijinga!
Mkuu maana yangu Niko neutral katika hili nilitaka kutoa mchango wangu kwa jinsi nilivyoelewa,na nilidhani kuna watu neutral tuchambue bila timu tuone kama kuna tija tushauri nini wafanye hawa watu.Burudani ni burudani na siasa ni siasa jombaa!! Hata pale Billiz, ingawaje ni ya Mwenyekiti wa CHADEMA lakini wapenda burudani wa CCM hawawezi kuacha kwenda eti kisa panamilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA!!! But all in all, muziki ni biashara... biashara haichagui mteja!
Sasa suala la kwamba Dimpoz alimuamini sana Dai linatoka wapi?! Kwani huyo Dai alifanya nini cha ajabu?! Au huyo mpiga saxophone alitoka nje ya nchi kwamba baada ya kufanya kazi na Diamond; hapo hapo angepanda ndege na kuondoka na ingekuwa ngumu kurudi tena!! Na uzuri zaidi, alivyofika studio huyo jamaa bado alikuwepo! Kwanini hakufanya nae? Au kwanini wasingeweka appointment cku nyingine? Tena studio ni mambo ya kawaida sana... unaweza ukaenda studio leo na kutengenezewa beat; unarudi siku nyingine ukaingize vocal unakuta beat keshapewa mtu mwingine!!Nani kati yao alieanza kutoka nje ya mada hadi kupumuliana kisogoni?kwangu dai kumkimbia dimpo haina excuse Mara zote alizokimbia,kwa nilivyoelewa swala la mpiga sexaphone dai hakuwa nalo ila alilikuta kwa dimpoz akalifanyia Kaz fasta ubaya ni kuwa walikutwa,kwa nilivyoelewa ni kama dimpoz alimuamini dai mia mia ila dai ni mjanja hakumuamini the same,dai ni mjanja anajua kutambua wazo zuri kwa haraka nadhani ndo mana yuko hapo,unajua kimsingi binadamu tunatakiwa kuwa hivyo ili utoke na wasanii wengine waache kubweteka na mafanikio madogo wanayopata.
Na wewe unataka?!Mnapumuliwa na domo mxieee