Nisaidia ufafanuzi katika haya;
1. Kwa nilivyoelewa ni kwamba Dimpoz aliona akae mbali na Simba kwasababu jamaa ana roho mbaya hataki mafanikio yake; sasa kwanini it has been two years since wako mbali mbali, kwanini dimpoz hajatumia hilo "jicho la fursa" alilonalo kutafuta hizo collabo mpaka leo???
2. Kama Simba ndio alikuwa anafanya figisu Dimpoz asifanikiwe, kwanini kipindi dimpoz yule karibu na Simba alikuwa anashine na baada ya kukaa mbali naye amekuwa doro.?? Maana nilidhani ilitakiwa iwe vice versa.. Kama alikuwa anabaniwa kipindi kile na bado alikuwa juu kimuziki, sasa hivi kama habaniwi tena na Simba si ndio alitakiwa awe hakamatiki kimuziki???
3. Mkitaka kujua unafiki wa huyu dimpoz anavyodai leo kuwa amesaidiwa zaidi na kiba kipindi yuko underground! Hebu nendeni YouTube tafuteni video ya siku ya kwanza alipopanda kwenye jukwaa la KTMA kupokea tuzo ambapo alipanda jukwaani na simba na wote wawili wakaongea! Hebu nendeni mkaandilie ile video alafu mje mniambie kuwa Dimpoz sio mnafiki na snitch..
Nijibu haya kwa sasa!
Point kubwa mnayoimiss (nadhani mnaijua ila kwa ushabiki mnajitia upofu)
Ommy Dimpoz na Diamond kwa wakati ule saga linaanza nani aliyekuwa star na connection nyingi?
Bila shaka hadi leo hii ni Diamond.
Hivyo kivyovyote Ommy alitegemea ile friends with benefits kutoka kwa Diamond.
Ndio maana hata safari ya Marekani alililia ashikwe japo mkono nae aende ili atumie safari ile kama fursa ya kupata connection.
Kilichotokea kinafahamika tayari.
Hivyo baada ya Ommy kupotezewa na ikumbukwe tayari alishapigwa bao katika collabo na Wanaija najaribu kuvivaa viatu vyake ni lazima alivunjika moyo sana.
Rafiki aliyemtegemea amshike mkono kamtosa!
Alijitahidi kujitutumua na Wanjera na nyinginezo lakini hakufua dafu.
Ikumbukwe hapo Kiba alisharejea katika kiti chake...hivyo media na attention yote ilikuwa kwa Kiba kafanya nini?
Diamond kafanya nini?
Ommy alikosa nguvu na ikumbukwe alishanyea kambi kwa Kiba pia.
(Kiufupi ni kwamba Ommy ni ile aina ya watu wasioweza kujisogeza hadi washikwe mkono)
Ndio maana ameshindwa kutoboa kama solo,kaamua ajirudi kwa Kiba kupata support.
Nadhani kwa maelezo hayo nimeua ndege wawili kwa wakati mmoja,yanajitosheleza.
Ommy ni mnafiki kiasi ndio maana hata mimi alinikera aliposhindwa kumpa support Ali Kiba aliyemtoa alipoamua kurejea katika muziki.
Nilimchukia sana.
Ila katika hili suala Diamond hawezi kukikwepa kikombe cha unafiki na roho mbaya pia.
Hapa ndio panapoleta malumbano maana mnashindwa kukiri hili ilhali liko wazi.