Chige,wewe ni mtu makini lakini katika hili umekurupuka.
Umeshindwa kuzidhibiti hasira zako juu ya hili saga badala yake umemshambulia Ommy katika skendo inayomtafuna.
Mada yako 50% imelenga kumchafua Ommy na sio kuzungumzia masuala ya kikazi ambayo ndizo lawama alizozitoa Ommy.
Kama mtu makini sikutegemea kabisa uingie katika huo mkumbo.
Turudi katika hoja zako za connection na collabo.
Hivi unawezaje kusema kwamba Diamond asingeweza kumfanyia connection Ommy?
Diamond alikuwa anaenda katika tuzo za BET (kama sikosei)
Hivyo jina lake lilikuwa ktk vichwa/vinywa vya waliokuwa wengi...ile si connection kubwa tayari?
Diamond hakwenda kama ambavyo angeenda Ommy...yeye alienda kama star.
Hivyo endapo angeenda na Ommy hata ile kushake hands na akina Kanye West ingekuwa connection tayari.
Pia kuhojiwa kule na Karueche kungekuwa connection na hizo ndizo fursa zenyewe.
Katika hili Diamond anabeba lawama ya roho mbaya na wivu.
Hapendi wengine wapate japo kiduchu ya kile apatacho.
Hukuona Ali Kiba akienda na Baraka South Afrika?
Unadhani alienda nae kuuza sura?
Ile ni connection, hata kukutanishwa na Sauti Sol ni connection tayari.
Collabo hapa namuelewa Ommy,hata kama ningekuwa mimi nimemueleza rafiki mpango wangu kesho nikakuta keshaupandia dau ule mpango ingeniumiza na kunivunja moyo wa kuendelea na ule mpango.
Ni Ommy anayejua aliumia kiasi gani,hivyo kuipotezea kwake collabo na Davido huenda ana sababu zake nyingi na kulalamika huko ni sahihi.
Ni vyema tutaweka mihemuko na mahaba yetu juu ya tunaowashabikia wanapoteleza na kusema ukweli.
Kama ukweli ni vigumu kuusema basi ni busara zaidi kukaa kimya.
Period