Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe nae kweli hujui unachokiongea sallam ndio aliemleta davido na j martins bongo, AY na Sallam ni washkajiHUYU SALLAM NI MUONGO SANA CONNECTION YA DIAMOND NA DAVIDO NI AY NDIYE ALIYEFANYA,MKUMBUKE PIA COLLABO YA OMMY DIMPOZ NA J.MARTIN PIA AY ALIHUSIKA,HUYU MENEJA ATAKUWA KILAZO KWELI HANA UWEZO WA KUMTENGENEZA MTU COLLABO AACHE UPUUZI
Mkuu Eddy Love,HUYU SALLAM NI MUONGO SANA CONNECTION YA DIAMOND NA DAVIDO NI AY NDIYE ALIYEFANYA,MKUMBUKE PIA COLLABO YA OMMY DIMPOZ NA J.MARTIN PIA AY ALIHUSIKA,HUYU MENEJA ATAKUWA KILAZO KWELI HANA UWEZO WA KUMTENGENEZA MTU COLLABO AACHE UPUUZI
Naona taabu kukutafutia hao wengine, lakini msikie AY mwenyewe akihojiwa na Bongo5 kuhusu collabo yake na Sean Kingstone:HIZI NDO COLLABO BORA ZA KIMATAIFA ALIZOFANYA AY TENA BURE
1. ay ft romeo buree
2. ay ft p.square buree
3. ay ft ms trinity buree
4. ay ft sean kingstone bure
5. ay ft saut soul buree
6. ay ft goldie buree
Hapo ukisoma tu, hupati taabu kufahamu kwamba hawa watu tayari walishakuwa connected before lakini sio kwamba hata kuongea nae hujawahi kuongea nae hata siku moja; mnakutana tu from nowhere halafu akupe FREE COLLABO wakati anajua muziki ni biashara? Na huyo ni Sean anayefanya kazi US... anajua kwa msanii kutoka nchi ndogo kama hii labda angemtoza $3000-5000 ndo ingekuwa fair; sasa Sean mwenyewe akiangalia $5000 anaona ndogo sana kuuza utu wake... kwahiyo, pamoja na connection waliyokuwa nayo, lakini $5000 kitu gani bhana! Kinyume chake, hao akina Davido na J Martins hizo 5 Grands hadi kesho wana shida nazo kwahiyo haiwezekani mmekutana ghafla tu halafu akufanyie FREE!Sean Kingston hutoza $30,000 kufanya collabo, AY aeleza alivyofanikiwa kurekodi nae bila kumlipa.
Hajawai kunilipisha, talent yako ndio inakubeba sometimes” amesema AY. “Unajua ukiweka hela mbele kwaajili ya kufanya collabo na watu, inakua talent yako ndo inabebwa na hela, usipokuwa na hela hamna kitu tena. So mi nachofanya naitumia talent yangu. Kwanza inaanza ushkaji inafata talent, ikija talent sasa kunakua kuna kitu wanaita unajenga nae trust..”
Na wewe unataka ukatafutiwe collabo Marekani kama mwenzako Ommy Dimpoz?!sidhani kama umekilelewa hata ulicho kiandika wewe ni mjnga mwingine kwenye kundi la diamond
haaahaaaa yes unawezaNa wewe unataka ukatafutiwe collabo Marekani kama mwenzako Ommy Dimpoz?!
tuzo za AfrimaChige,wewe ni mtu makini lakini katika hili umekurupuka.
Umeshindwa kuzidhibiti hasira zako juu ya hili saga badala yake umemshambulia Ommy katika skendo inayomtafuna.
Mada yako 50% imelenga kumchafua Ommy na sio kuzungumzia masuala ya kikazi ambayo ndizo lawama alizozitoa Ommy.
Kama mtu makini sikutegemea kabisa uingie katika huo mkumbo.
Turudi katika hoja zako za connection na collabo.
Hivi unawezaje kusema kwamba Diamond asingeweza kumfanyia connection Ommy?
Diamond alikuwa anaenda katika tuzo za BET (kama sikosei)
Hivyo jina lake lilikuwa ktk vichwa/vinywa vya waliokuwa wengi...ile si connection kubwa tayari?
Diamond hakwenda kama ambavyo angeenda Ommy...yeye alienda kama star.
Hivyo endapo angeenda na Ommy hata ile kushake hands na akina Kanye West ingekuwa connection tayari.
Pia kuhojiwa kule na Karueche kungekuwa connection na hizo ndizo fursa zenyewe.
Katika hili Diamond anabeba lawama ya roho mbaya na wivu.
Hapendi wengine wapate japo kiduchu ya kile apatacho.
Hukuona Ali Kiba akienda na Baraka South Afrika?
Unadhani alienda nae kuuza sura?
Ile ni connection, hata kukutanishwa na Sauti Sol ni connection tayari.
Collabo hapa namuelewa Ommy,hata kama ningekuwa mimi nimemueleza rafiki mpango wangu kesho nikakuta keshaupandia dau ule mpango ingeniumiza na kunivunja moyo wa kuendelea na ule mpango.
Ni Ommy anayejua aliumia kiasi gani,hivyo kuipotezea kwake collabo na Davido huenda ana sababu zake nyingi na kulalamika huko ni sahihi.
Ni vyema tutaweka mihemuko na mahaba yetu juu ya tunaowashabikia wanapoteleza na kusema ukweli.
Kama ukweli ni vigumu kuusema basi ni busara zaidi kukaa kimya.
Period
Toa facts. Hatutaki assumptionsHujui chochote wewe... kunakuwa na quid pro quo arrangement kati ya wasanii, kwa mfano, ngoma ile ile upande mmoja inaweza kuitwa X ft Y lakini ukienda nchini kwa Y, itaitwa Y ft X... hapo, issue ni mtonyo! Au inaweza kuwa kwa ajili ya kila mmoja kumtangaza mwenzake!! Kinyume chake, collabo ya Ommy na J Martins ni ya kutengenezewa... ya kuomba na sio ya kukubaliana na ndio maana Sallam akasema wazi "... safari hii lazima ulipe!"
Conclusion yako haina tofauti na ya yule mwanaume aliyelilia kwenda Marekani na Mwanaume mwenzake ili akamtafutie collabo!!!!!
Kawa-smart hao wanaosukumwa na chuki...! Yaani ukimsikiliza, unashindwa kabisa kujua anacholalamika ni nini! Na inavyoonekana Ommy Dimpoz alikuwa karibu sana na Sallam kuliko Diamond alivyokuwa na Sallam!! Sasa kama kweli shida yake ilikuwa ni kufanya collabo na Davido pamoja na Iyanya; sasa sijui nini kilimfanya asifaye nao! Diamond alilipa pesa hadi Nigeria kumfuata Davido kufanya shooting ya Number I Remix... sasa kama TZ ilishindikana, sijui kwanini huyo Dimpoz hakumfuata huyo Davido na Iyanya huko huko Nigeria!!! Kama alivyosema, alitaka bure bure kama ilivyokuwa kwa J Martin!
Mkuu umesoma tayari ukaelewa kama ulivyosema?mbn wote mnachangia tayari mkiwa na upande?Nisaidia ufafanuzi katika haya;
1. Kwa nilivyoelewa ni kwamba Dimpoz aliona akae mbali na Simba kwasababu jamaa ana roho mbaya hataki mafanikio yake; sasa kwanini it has been two years since wako mbali mbali, kwanini dimpoz hajatumia hilo "jicho la fursa" alilonalo kutafuta hizo collabo mpaka leo???
2. Kama Simba ndio alikuwa anafanya figisu Dimpoz asifanikiwe, kwanini kipindi dimpoz yule karibu na Simba alikuwa anashine na baada ya kukaa mbali naye amekuwa doro.?? Maana nilidhani ilitakiwa iwe vice versa.. Kama alikuwa anabaniwa kipindi kile na bado alikuwa juu kimuziki, sasa hivi kama habaniwi tena na Simba si ndio alitakiwa awe hakamatiki kimuziki???
3. Mkitaka kujua unafiki wa huyu dimpoz anavyodai leo kuwa amesaidiwa zaidi na kiba kipindi yuko underground! Hebu nendeni YouTube tafuteni video ya siku ya kwanza alipopanda kwenye jukwaa la KTMA kupokea tuzo ambapo alipanda jukwaani na simba na wote wawili wakaongea! Hebu nendeni mkaandilie ile video alafu mje mniambie kuwa Dimpoz sio mnafiki na snitch..
Nijibu haya kwa sasa!
....trust me kuna relationship imevunjika kisa binti ni team kiba na kijana ni team diamond ... wamebishana km mnavyobishana humu wakaishia kutukanana mitusi na kutemana.... Haya mambo ni makubwa
Haaahaa... hapo kwenye ubepari wa akina Sallam ni TRUE kwa 100% na ndio maana wanafanikiwa! Tena heri ya Bab Talle; lakini Sallam na Fella... ni full Mabepari!!!! Huyo Sallam mwenyewe; fanya masihara sehemu nyingine lakini sio kwenye kazi.... na bahati mzuri vile vile wamekutana na mtu aliye serious na kazi! Manake hata huyo Diamond mwenyewe, kwenye maisha ya kawaida yupo cool sana; sasa ngoja ukutane nae kwenye kazi alivyo mbishi na "mkorofi"!Ommy mpenda mteremko. Anataka shortcuts ya Maisha.
Mwenzake katumia ubunifu na moja kati ya kitu bora ambacho Diamond alikifanya ni kusimamiwa kazi zake na Tale, Fella na Sallam.
Hawa jamaa ni pure wabepari. Hakuna urafiki kwenye kazi zao ndio maana ni wasimamizi pekee wenye Maendeleo.
Ommy anataka kuleta ukigoma Daslam, tupa kuleeeeee!