Hatimae Naona Kama 1+1 = 2 Inaleta Maana

Hatimae Naona Kama 1+1 = 2 Inaleta Maana

Nadhani tukipata jibu la kwanini Ommy hakufanya kolabo na Davido na Iyanya ndio tutajua nani MBAYA.
 
HUYU SALLAM NI MUONGO SANA CONNECTION YA DIAMOND NA DAVIDO NI AY NDIYE ALIYEFANYA,MKUMBUKE PIA COLLABO YA OMMY DIMPOZ NA J.MARTIN PIA AY ALIHUSIKA,HUYU MENEJA ATAKUWA KILAZO KWELI HANA UWEZO WA KUMTENGENEZA MTU COLLABO AACHE UPUUZI
Wewe nae kweli hujui unachokiongea sallam ndio aliemleta davido na j martins bongo, AY na Sallam ni washkaji
 
HUYU SALLAM NI MUONGO SANA CONNECTION YA DIAMOND NA DAVIDO NI AY NDIYE ALIYEFANYA,MKUMBUKE PIA COLLABO YA OMMY DIMPOZ NA J.MARTIN PIA AY ALIHUSIKA,HUYU MENEJA ATAKUWA KILAZO KWELI HANA UWEZO WA KUMTENGENEZA MTU COLLABO AACHE UPUUZI
Mkuu Eddy Love,

Huyo unayemuita kilaza ndiye aliyekuwa anatumiwa na Prime time promotions (clouds FM) kuwaleta wasanii wa kimataifa kwenye matamasha ya fiesta.! Tenda zote za kuleta international artists ni huyu jamaa alikuwa anapewa!

Yeye ndiye aliyemleta Davido kwenye fiesta, so alikuwa na access kubwa na management ya Davido kuliko mtu yeyote yule.. Simba aliwasiliana na AY kwasababu AY alikuwa ni mshkaji na Sallam kitambo but Sallam hakuwa na ushkaji na Simba! So ilikuwa rahisi kwa Simba kupitisha ombi lake through AY hatimae lifike kwa Sallam na Hatimae kwa Davido..

Pia huyu huyu unayemuita kilaza ndiye meneja wa AY ambaye unamuamini kuwa ni genius!
 
HIZI NDO COLLABO BORA ZA KIMATAIFA ALIZOFANYA AY TENA BURE

1. ay ft romeo buree
2. ay ft p.square buree
3. ay ft ms trinity buree
4. ay ft sean kingstone bure
5. ay ft saut soul buree
6. ay ft goldie buree
Naona taabu kukutafutia hao wengine, lakini msikie AY mwenyewe akihojiwa na Bongo5 kuhusu collabo yake na Sean Kingstone:
Sean Kingston hutoza $30,000 kufanya collabo, AY aeleza alivyofanikiwa kurekodi nae bila kumlipa.

Hajawai kunilipisha, talent yako ndio inakubeba sometimes” amesema AY. “Unajua ukiweka hela mbele kwaajili ya kufanya collabo na watu, inakua talent yako ndo inabebwa na hela, usipokuwa na hela hamna kitu tena. So mi nachofanya naitumia talent yangu. Kwanza inaanza ushkaji inafata talent, ikija talent sasa kunakua kuna kitu wanaita unajenga nae trust..
Hapo ukisoma tu, hupati taabu kufahamu kwamba hawa watu tayari walishakuwa connected before lakini sio kwamba hata kuongea nae hujawahi kuongea nae hata siku moja; mnakutana tu from nowhere halafu akupe FREE COLLABO wakati anajua muziki ni biashara? Na huyo ni Sean anayefanya kazi US... anajua kwa msanii kutoka nchi ndogo kama hii labda angemtoza $3000-5000 ndo ingekuwa fair; sasa Sean mwenyewe akiangalia $5000 anaona ndogo sana kuuza utu wake... kwahiyo, pamoja na connection waliyokuwa nayo, lakini $5000 kitu gani bhana! Kinyume chake, hao akina Davido na J Martins hizo 5 Grands hadi kesho wana shida nazo kwahiyo haiwezekani mmekutana ghafla tu halafu akufanyie FREE!

Halafu hoja yako kwamba ni AY ndie aliwaleta akina Davido, sio kweli! Huyu Sallam watu wameanza kumfahamu sana baada ya kuwa Meneja wa Diamond lakini yupo kwenye game kama promoter muda mrefu sana! Alishawahi pia kuwa Meneja wa Mr. Nice sema ndo vile tena hawakufika mbali!!!
 
sidhani kama umekilelewa hata ulicho kiandika wewe ni mjnga mwingine kwenye kundi la diamond
Na wewe unataka ukatafutiwe collabo Marekani kama mwenzako Ommy Dimpoz?!
 
Hao kina Dipoz na Kiba lazima watengeneze uhasama na Abdul ili waweze kuishi.Hawawezi kusimama wenyewe ni wepesi mno.
 
Chige,wewe ni mtu makini lakini katika hili umekurupuka.
Umeshindwa kuzidhibiti hasira zako juu ya hili saga badala yake umemshambulia Ommy katika skendo inayomtafuna.

Mada yako 50% imelenga kumchafua Ommy na sio kuzungumzia masuala ya kikazi ambayo ndizo lawama alizozitoa Ommy.
Kama mtu makini sikutegemea kabisa uingie katika huo mkumbo.

Turudi katika hoja zako za connection na collabo.
Hivi unawezaje kusema kwamba Diamond asingeweza kumfanyia connection Ommy?
Diamond alikuwa anaenda katika tuzo za BET (kama sikosei)
Hivyo jina lake lilikuwa ktk vichwa/vinywa vya waliokuwa wengi...ile si connection kubwa tayari?
Diamond hakwenda kama ambavyo angeenda Ommy...yeye alienda kama star.
Hivyo endapo angeenda na Ommy hata ile kushake hands na akina Kanye West ingekuwa connection tayari.
Pia kuhojiwa kule na Karueche kungekuwa connection na hizo ndizo fursa zenyewe.
Katika hili Diamond anabeba lawama ya roho mbaya na wivu.
Hapendi wengine wapate japo kiduchu ya kile apatacho.

Hukuona Ali Kiba akienda na Baraka South Afrika?
Unadhani alienda nae kuuza sura?
Ile ni connection, hata kukutanishwa na Sauti Sol ni connection tayari.

Collabo hapa namuelewa Ommy,hata kama ningekuwa mimi nimemueleza rafiki mpango wangu kesho nikakuta keshaupandia dau ule mpango ingeniumiza na kunivunja moyo wa kuendelea na ule mpango.
Ni Ommy anayejua aliumia kiasi gani,hivyo kuipotezea kwake collabo na Davido huenda ana sababu zake nyingi na kulalamika huko ni sahihi.

Ni vyema tutaweka mihemuko na mahaba yetu juu ya tunaowashabikia wanapoteleza na kusema ukweli.
Kama ukweli ni vigumu kuusema basi ni busara zaidi kukaa kimya.
Period
tuzo za Afrima
 
Hujui chochote wewe... kunakuwa na quid pro quo arrangement kati ya wasanii, kwa mfano, ngoma ile ile upande mmoja inaweza kuitwa X ft Y lakini ukienda nchini kwa Y, itaitwa Y ft X... hapo, issue ni mtonyo! Au inaweza kuwa kwa ajili ya kila mmoja kumtangaza mwenzake!! Kinyume chake, collabo ya Ommy na J Martins ni ya kutengenezewa... ya kuomba na sio ya kukubaliana na ndio maana Sallam akasema wazi "... safari hii lazima ulipe!"

Conclusion yako haina tofauti na ya yule mwanaume aliyelilia kwenda Marekani na Mwanaume mwenzake ili akamtafutie collabo!!!!!
Toa facts. Hatutaki assumptions
 
Huo ni uchambuzi au ujambuzi maan naona unajiulza maswali na unajijibu mwenyew huu mchezo hauitaji hasira wa kubwa mnaona mmeonewa sanaaa this tym kumbe inaumaa hata chai ujanywa cjui umeoteshwa duuu
 
Me nilielewa hizo dola 3000 na 5000 ni posho ya Sallam kama dalali. Anyways hizo points nyingine nimekuelewa vizuri sana naunga mkono hoja
 
Inasikitisha kuona watu wataifa moja, mkoa mmoja kabila moja wanachukiana kiasi hiki... then nimegundua media houses za Tanzania wanalipalilia hili bifu la diamond Vs AK&OD.... Haswa wale mawingu..... hili bifu linawanufaisha wenye bifu na media houses tu.... wasanii wengine linawadidimiza tu coz kwa mfano darasa juzi katoa ngoma kali sana bt imetoka kipindi ambacho kuna mtifuano so concentration ipo kwenye bifu now... mashabiki ambao ni mm na ww ambao wengine hata wenye bifu hatujawahi kuwatia machoni tunaishia kula ubuyu social media huku tukichukiana pasipo sababu....trust me kuna relationship imevunjika kisa binti ni team wema na kijana ni team diamond ... wamebishana km mnavyobishana humu wakaishia kutukanana mitusi na kutemana.... Haya mambo ni makubwa
 
Yaaaan wewe ndio sijakuelea pamoja na maelezo marefu,ngoja nikueleweshe kwenye hili na kutaka kuongozana na D ulaya haikuwa apate collabo na wamarekan bali wasanii wakubwa toka africa waliokuwa wakishirik ktk hizo show ambazo D pia alipata mwaliko ndugu Duuh
 
Kawa-smart hao wanaosukumwa na chuki...! Yaani ukimsikiliza, unashindwa kabisa kujua anacholalamika ni nini! Na inavyoonekana Ommy Dimpoz alikuwa karibu sana na Sallam kuliko Diamond alivyokuwa na Sallam!! Sasa kama kweli shida yake ilikuwa ni kufanya collabo na Davido pamoja na Iyanya; sasa sijui nini kilimfanya asifaye nao! Diamond alilipa pesa hadi Nigeria kumfuata Davido kufanya shooting ya Number I Remix... sasa kama TZ ilishindikana, sijui kwanini huyo Dimpoz hakumfuata huyo Davido na Iyanya huko huko Nigeria!!! Kama alivyosema, alitaka bure bure kama ilivyokuwa kwa J Martin!

Ommy mpenda mteremko. Anataka shortcuts ya Maisha.

Mwenzake katumia ubunifu na moja kati ya kitu bora ambacho Diamond alikifanya ni kusimamiwa kazi zake na Tale, Fella na Sallam.

Hawa jamaa ni pure wabepari. Hakuna urafiki kwenye kazi zao ndio maana ni wasimamizi pekee wenye Maendeleo.

Ommy anataka kuleta ukigoma Daslam, tupa kuleeeeee!
 
Nisaidia ufafanuzi katika haya;

1. Kwa nilivyoelewa ni kwamba Dimpoz aliona akae mbali na Simba kwasababu jamaa ana roho mbaya hataki mafanikio yake; sasa kwanini it has been two years since wako mbali mbali, kwanini dimpoz hajatumia hilo "jicho la fursa" alilonalo kutafuta hizo collabo mpaka leo???

2. Kama Simba ndio alikuwa anafanya figisu Dimpoz asifanikiwe, kwanini kipindi dimpoz yule karibu na Simba alikuwa anashine na baada ya kukaa mbali naye amekuwa doro.?? Maana nilidhani ilitakiwa iwe vice versa.. Kama alikuwa anabaniwa kipindi kile na bado alikuwa juu kimuziki, sasa hivi kama habaniwi tena na Simba si ndio alitakiwa awe hakamatiki kimuziki???

3. Mkitaka kujua unafiki wa huyu dimpoz anavyodai leo kuwa amesaidiwa zaidi na kiba kipindi yuko underground! Hebu nendeni YouTube tafuteni video ya siku ya kwanza alipopanda kwenye jukwaa la KTMA kupokea tuzo ambapo alipanda jukwaani na simba na wote wawili wakaongea! Hebu nendeni mkaandilie ile video alafu mje mniambie kuwa Dimpoz sio mnafiki na snitch..

Nijibu haya kwa sasa!
Mkuu umesoma tayari ukaelewa kama ulivyosema?mbn wote mnachangia tayari mkiwa na upande?
 
....trust me kuna relationship imevunjika kisa binti ni team kiba na kijana ni team diamond ... wamebishana km mnavyobishana humu wakaishia kutukanana mitusi na kutemana.... Haya mambo ni makubwa

Hahahahahaha duuuuuuuhh.!!
Nimejisikia nimtag team kiba damu damu.. Cc: Nifah

[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ommy mpenda mteremko. Anataka shortcuts ya Maisha.

Mwenzake katumia ubunifu na moja kati ya kitu bora ambacho Diamond alikifanya ni kusimamiwa kazi zake na Tale, Fella na Sallam.

Hawa jamaa ni pure wabepari. Hakuna urafiki kwenye kazi zao ndio maana ni wasimamizi pekee wenye Maendeleo.

Ommy anataka kuleta ukigoma Daslam, tupa kuleeeeee!
Haaahaa... hapo kwenye ubepari wa akina Sallam ni TRUE kwa 100% na ndio maana wanafanikiwa! Tena heri ya Bab Talle; lakini Sallam na Fella... ni full Mabepari!!!! Huyo Sallam mwenyewe; fanya masihara sehemu nyingine lakini sio kwenye kazi.... na bahati mzuri vile vile wamekutana na mtu aliye serious na kazi! Manake hata huyo Diamond mwenyewe, kwenye maisha ya kawaida yupo cool sana; sasa ngoja ukutane nae kwenye kazi alivyo mbishi na "mkorofi"!
 
Back
Top Bottom