Hatimae Nimepata Bajaj ya mkataba! Upi ushauri wako?

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
1,634
Reaction score
3,833
Habari JF
Baada ya kupambana kwa muda mrefu Sasa nimepata Bajaj ya mkataba!

Nikimaliza itakuwa Yangu!

Ubunifu ntakao ufanya Ni Kama ifuatavyo.
Nitaandaa Business card sizizo pungua 100

Nitakuwa Ninampa abiria ili tuwe na ukaribu wa kazi.

Kama Kuna mtu analakuongezea karibu Sana.

Mkataba msingi wake Ni afya
Kwaiyo nitaanza ratiba ya kwenda Gym Kila siku usiku ili magonjwa yasiwe changamoto kwangu!

Naombeni Kama Kuna ushauri au lolote mnisaidie
 
We muhaya?bajaj na business card?kuna bolt siku hizi hakuna kujisumbua kusave namba za bajaj au bodaboda.
 
Gym na business cards ni unnecessary moves ambazo zitakuongezea gharama za uendeshaji. Ushauri wangu kula vizuri, fanya kazi sehemu yenye movement nzuri na uaminifu kwa wateja wako utatoboa.
 
Nenda kajikinge na ukikinge kifaa chako..dunia sio mbaya ila walimwengu wabaya.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mzee unaijua Bajaj vizuri, ili upate hela inabidi 12 - 14 hours upo road unakanyaga , otherwise jiandae kurudisha chombo cha watu
 
Gym na business cards ni unnecessary moves ambazo zitakuongezea gharama za uendeshaji. Ushauri wangu kula vizuri, fanya kazi sehemu yenye movement nzuri na uaminifu kwa wateja wako utatoboa.
Nashukuru Sana
 
Oya !Upo mkoa Gani ?Naunapiga root Gani ?
 
Gym na business cards ni unnecessary moves ambazo zitakuongezea gharama za uendeshaji. Ushauri wangu kula vizuri, fanya kazi sehemu yenye movement nzuri na uaminifu kwa wateja wako utatoboa.
Sawa mkuu Ila naona mazoezi Ni muhimu maana kuumwa ndio sababu ya kushindwa kurejesha au unasemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…