Hatimae tunamiliki TATA yetu baada ya kumaliza marejesho

Hatimae tunamiliki TATA yetu baada ya kumaliza marejesho

mkuu kwa mujibu wa maelezo yako hapo ni kwamba milion 60 iwe imerudi ndani ya mwaka inamaana kila mwezi uwe unarudisha milion 60 sasa kwa biashara ya tata inauwezo wa kuleta walau milion 6 kwa mwezi maana tano yao, moja kwa ajili yako posho za madereva bado hatujazungumzia mafuta unaweza kunisaidia kwenye hilo
hujanielewa kidogo mkuu ni kuwa hiyo milioni 60 unailipa ndani ya miezi 12 Ina maana unaigawa hiyo 60 kwa 12 kwa hiyo kila mwezi unapeleka milioni 5. Naamini umenielewa mkuu.
 
Pokea pongezi zangu za dhati kwa hatua uliyopiga kiongozi.
Mkuu mie nna maswali kadhaa ningependa kusikia mawili matatu kutoka kwako
1. Hiyo gari ilikuwa Tata marcopolo, Tata Starbus au Tipper?
2.Je, mkopo wa hiyo gari ulikuwa na thamani gani? Ulikuwa wa muda gani?
3.Ulitumia utaratibu gani kufanya marejesho, kwa wiki au mwezi?
4.Ulikutana na changamoto zipi wakati hujamaliza marejesho ya mkopo?
Mwisho kabisa ungependa kuwashauri nini wale ambao wangependa kumiliki gari mpya aina ya TATA kwa njia ya mkopo?
Natumaini mtoa mada umeyaona haya Maswali, sio mbaya tukikapata majibu kuna kitu tutajifunza.
 
hujanielewa kidogo mkuu ni kuwa hiyo milioni 60 unailipa ndani ya miezi 12 Ina maana unaigawa hiyo 60 kwa 12 kwa hiyo kila mwezi unapeleka milioni 5. Naamini umenielewa mkuu.
Mkuu naomba soma hii hesabu nazani jamaa ndio swali lake lipo hapo:.
60,000,000/12(miezi) = 5,000,000
5,000,000/30(siku) = 166,666.66667

Hii ina maanisha kila siku ulitakiwa kusanya 167,000 ili mwisho wa mwezi upeleke millioni 5!.
Navojua kwa dsm, boss kwa siku anapewa laki 1 kwa costa (sijajua TATA bei gani)
 
Mkuu naomba soma hii hesabu nazani jamaa ndio swali lake lipo hapo:.
60,000,000/12(miezi) = 5,000,000
5,000,000/30(siku) = 166,666.66667

Hii ina maanisha kila siku ulitakiwa kusanya 167,000 ili mwisho wa mwezi upeleke millioni 5!.
Navojua kwa dsm, boss kwa siku anapewa laki 1 kwa costa (sijajua TATA bei gani)
Nilimjibu member anayeitwa Fromsirwithlove aliekuwa mchangiaji no 16 masaa sita yaliyopita.Asante Kwa kuelewa
 
Ni naona wewe ni marketing officer wa hiyo muhindi na hizo TATA zake kama vipi weka tu mawasiliano yake
Watu wamcheki
Ahsante
 
Nilishajibu soma ndugu[emoji26]
Kama ulishajibu asante sana. Ila nasikia Gachuma anauza hizo gari pia though sijui kama ni TATA starbus au marcopolo!!! Ndio maana nilitaka jibu ambalo umesema umejibu japo sijaona, yeye(Gachuma) anauza M70. Kama ungejibu ningepiga maswali pia lakini asante.
 
Nina wasi wasi hii TATA ililala yombo na huyu memba. Tokea April 2018 hajawahi tia mguu JF. Hizi kazi za barabarani tumwachie mola roho zetu

Hapana. Huenda aliona humu kuna watu waoga sana wa kujaribu akaona ajikite kwenye biashara.

Huenda basi ziliongezeka. Inabidi tujifunze kutoka kwake.
 
Hi great thinkers. Leo Nina furaha isiyo na kifani tumekamilisha marejesho Kwa Mhindi.Mwaka 2017 January Mimi kaka na Dada yetu tumekamilisha marejesho leo asubuhi Kwa muhindi.

Hatimae gari imekuwa yetu rasmi bado ipo katika hali nzuri leo inapata service Kwa mchaga kesho tuanze kusanya zetu.Hapa tupo Kiwangwa kuku anachomeka ndizi mkaango castle kopo za kutosha zinamiminika makooni.

Nawaasa msiogope mikopo jamani tupige maisha ukiwa na plan nzuri unatusua.
12e0387fa86ac64c04aa46c1d3cbd168.jpg
Mtafilisika heeee kula gani huko?
 
Back
Top Bottom