Hatimae USA hatoweza kufika kwenye space kwasabu ya Ujinga wa Trump.

Hatimae USA hatoweza kufika kwenye space kwasabu ya Ujinga wa Trump.

snipa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
4,523
Reaction score
2,165
Baada ya vita kubwa kati ya Trump na Elon Musk, kuhusiana na bajeti iliyopitishwa, huku Trump akiona itasaidia uchumi na Elon musk akiona inaongeza deni, sasa ndoto za wamarekani zinaenda kuzimwa.

Trump alikuwa na lengo lakuitawala Space lakini alijisahau bila Elon musk hawezi toboa.

Kupitia ukurasa wake wa Truth social Trump amesema Kosa kubwa ambalo Biden alilifanya ni Kufund project za Musk ikiwemo Space X, na njia muhimu ni kufuta mikataba yote aliyopewa elon na Serikali ya US ili kupunguza matumizi.

elon nae hajaonyesha unyonge na katangaza kusimamisha shughuli zote za Dragon Spacecraft.

Ikumbukwe Marekani itamlazimu akawapigie magoti Russia au China ili aende kwenye space mana space shuttle alushazifungia mnamo 2011.
IMG_20250605_235548.jpg
 
Mafahali wawili hawawezi kukaa zizi moja.

Tycoons, Billionaires are fighting let the giants eat themselves, let's see how it goes...
 
Trump amemtumia Elon kushinda uchaguzi, kisha anamtupilia mbali.

Ushawishi wa Trump umeshuka kutokana na sababu mojawapo kwamba anamkumbatia Elon Musk.

Kwa sababu Trump anapenda sifa na kuona anafanikiwa kama rais, kumbagaza Elon ni suala lililokuwa limetarajiwa mapema sana.

Wakati Trump angependa kubaki katika sifa yake ileile ya kukuza uchumi na kubana matumizi, Elon naye anataka kurejesha biashara zake katika afya ya zamani.

Wateja wengi wamejiondoa kwake ikiwa ni pamoja na kuchukiwa na raia kwa sababu tu ya uhusiano wake na Trump.

Sasa huo mtikasi baina yao una faida kwa Donald Trump na pia una faida kwa Elon Musk.

Kwamba zitakoma shughuli za utafiti katika anga za juu na mradi wa kuhamia Sayari Mars kuanzia mwaka 2027, hilo haliwezekani kwa sababu ni sehemu ya mpango mkuu wa serikali ya Marekani na mfumo mzima wa ulimwengu.

Nujuacho ni kwamba Trump na Elon wataendelea kuwa mabesti wakubwa hadi mabilionea hao waamie zao huko kwenye sayari nyingine.
 
Tatizo hadi wamefikia hatua ya personal issues, Musk kaanza kumdiss trump issue ya kuhusika kwenye ngono za watoto, jambo ambalo waarabu wanahisi, ndio suala ambalo israel wanatumia kumblackmail trump, lakini not big issue.

Suala la kukwama kwa project za Space ni kweli itakuwa ngumu lakini wakimtema musk itawachukua muda sana kwasabu vyombo vingi walisha retire.
Otherwise Trump aingize masuala ya national interest ktk space na security ili kumbana musk.
akishindwa hapo itabidi wamrudie tu Boeing, ili kufika kwenye space ila shida tu ni kuwa Boeing Starliner sio economic kwasabu seat moja inacost hadi $91M ukilinganisha na $55M kwenye Dragon za Musk, tofauti ya $36M kwa seat moja ndio extra cost ambayo US tax payers wataingia ambayo kwa watu wanne ni zaidi ya $144M.

Trump hana namna kama kweli anataka costs cut ni lazma amrudie musk, NASA kutumia Boeing Starliner ni hasara kubwa sana,

Na amini Safari ya Mars mchina yuko mbele sana shida tu ni kuwa hawapendi media.
 
Marekani walishaenda space kitambo, hawamtegemei Musk.
Sahihi lakini NASA walishajikita kumfund Musk, ndiomana vifaa vya zaman walishaviretire, assume ISS tu nayo Musk alikula deal la kuilipua, so US bila musk kwenye space yuko old fashioned.
 
Raisi wa marekani hawezi kukurupuka
 
🇺🇸Elon Musk Lost $34 Billion in One Day Due to Trump Dispute, Tesla Lost $150 Billion, and Trump Lost Only $1 Billion — Bloomberg
 
Tofauti ya Trump na Magufuri ni kwamba mmoja alikua billionair, Lkn mwishini wote watafeli tu
 
Suala la kukwama kwa project za Space ni kweli itakuwa ngumu lakini wakimtema musk itawachukua muda sana kwasabu vyombo vingi walisha retire.
Hawaku retire kwa kupenda bali mazingira yaliwalazimisha.
Boeing mradi wake wa space shuttle ulikuwa unasuasua unachelewa kufikia deadline ndipo wakawekeza kwa SpaceX.
Boeing hatimae walikwama kuwarudisha wana anga duniani hadi SpaceX ilipofanikiwa kuwarudisha.
Wamarekani wametiliana saini na shirika la Rascosmos ya Urusi Mkataba kuwasafirisha wana anga wa Marekani kwenda international space station na kuwarudisha.
Nashangaa hapa JF watu wanawapondea Russia teknolojia yao ni duni!
 
Russia hayupo nyuma kwenye Tech shida marekani anapenda media.

Hakuna mkataba unaowataka Russia kupitia Roscosmos kupeleka astronauts USA kwenye Space.

Mkataba uliopo kati ya NASA na Roscosmos ni (No cost seat swap)
Mkataba unaowaruhusu Astronauts wa Russia kusafikiri kutumia vifaa vya nasa na Nasa kusafiri kutumia vifaa vya Russia bila directly payment.

Ikiwa marekani atakuwa hana chombo chochote cha kwenda kwenye space hiyo no cost seat swap haitowezekana kwasabu NASA atamtegemea russia pekee so ni lazma alipie
 
Hakuna mkataba unaowataka Russia kupitia Roscosmos kupeleka astronauts USA kwenye Space.
Hukunielewa labda nimeandika vibaya nitarudia kusoma wapi nimekosea. Sijui kwanini umenielewa kinyume chake.
Marekani ndiyo aliye hitaji huduma ya Russia kusafirishiwa wana anga wake.
Au kwa mfumo uliyo uelezea.
 
Miradi mikubwa ni vizuri kufadhiliwa na serikali, lakini itategemea sera ya serikali kwa kipindi hicho; fikiria upoteze muda wako na akili yako kutengeneza kitu ambacho soko lake bado halijapatikana, Je kipindi hicho utakuwa unakula nini na utawalipa nini wafanyakazi?

Ni sawa na kupoteza muda wa miezi kadhaa ukichimba uwanjani kwako ukihisi labda unaweza kupata madini. Je, kipindi hicho unachimba huku ukipoteza muda wa kwenda kulima au kufanya biashara zingine, utakuwa unakula nini?

Kwa mazingira hayo, Marekani kujiondoa kwenye ufadhili huo, inatafsiri ya kuwa huo mradi wake hawautaki kwa sasa.​
 
Back
Top Bottom