Ben T
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 245
- 263
Habari Wanajamvi natumaini kuwa hamjambo!
Nami nimeona nitoe angalau mchango wangu kwenye hili suala la mafuta ya Kula kuadimika ghafla baada ya TRA kuzuia Meli mbili ambazo kwa mujibu wa TRA zimebeba mafuta ambayo ni tayari kwa matumizi (Refined Palm Oil) na kwa mujibu wa TBS Meli hizo zimebeba mafuta ghafi (Crude Palm Oil) ambayo ni lazima yaende Kiwandani kusafishwa.
Kwenye hili suala kuna mambo ambayo yamejitokeza ambayo ni ya Msingi.
1. Kuna Taasisi mbili za Serikali ambazo ni TRA na TBS kwa muji
bu wa maelezo ni kuwa taarifa zilizowasilishwa TRA ziko tofau
ti na kilichopatikana TBS baada ya kuchukua sampuli za mafu
ta hayo. TBS wamefanya uchunguzi wao na wamebaini kuwa hayo mafuta ni mafuta ghafi hivyo yanastahili kulipa ushuru wa asilimia 10 , lakini TRA wanadai kuwa hayo mafuta si ghafi bali ni mafuta yaliyotayari kutumika na yana stahili kulipiwa asilimia 25 kama ushuru. Mfanyabiashara ambaye ameleta mafuta hayo anadai kuwa mafuta ni ghafi hivyo nae anastahili kulipa 10% kama ushuru. Alipoombwa atoe uthibitisho zaidi kuiridhisha TRA kama hayo mafuta ni ghafi Mfanyabiashara ameshindwa kutoa na tatizo ndiyo linaanzia hapo.
Sasa kwa mujibu wa tukio hili Nchi imeanza kutumia akiba yake ya Mafuta kutoka kwenye Hifadhi yake kuu na ikumbukwe kuwa si watumiaji tu wa kawaida ambao huwa wanatumia mafuta pekee bali Viwanda vikubwa vya Chakula pia hutumia mafuta kama malighafi ya uzalishaji.
Tatizo hili limekuzwa ghafla kupitia vyombo vya habari lakini sisi Wanainchi tukiwa tunapata taarifa za upande mmoja tu , huku tukikosa kusikia upande wa pili wa Mfanyabiashara juu ya uthibitisho alioombwa kuutoa kama ameutoa tayari.
Mimi ningewaomba Watanzania wenzangu kuwa tusiwe wepesi kulaumu tu, tupate kwanza taarifa sahihi ndiyo tutoe lawama. Hapa kuna kitu kinafichwa, iweje TBS waseme mafuta ni ghafi na TRA waseme mafuta si ghafi na Mfanyabiashara nae ashindwe kutoa uthibitisho wa ziada kuwa mafuta ni ghafi?
Tuombe muda kidogo ila naamini kila kitu kitafahamika!