Hatimaye Arsenal yashuka mpaka nafasi ya pili msimamo EPL

Kuna ujinga flani arsenal wamekuanao kwa miongo mingi sana. Huo umewagharimu leo

Huu mchezo wa kugonga gonga mpira hata sehemu ya kufunga, unakosesha magoli mengi sana. Shaka alikua na goli zuri la kusawazisha mapema

Mbaya zaidi kugongagonga golini kwetu, tumeangalia mpira roho juu juu mpaka mpira unaisha

Yani adui kapandisha timu, anakabia kwenye final third ya kwetu tena ni nje kidogo tu ya 18, lakini mpira unaanzishwa hapo hapo golini, wanaanza kupasiana pasiana, golini kabisa, unategemea nini.

Basi tu naipenda arsenal ntafanyaje
 
Kuna ujinga mwingi sana huwa unafanywa na Arsenal,sijui huwa mpango wa timu au ligi ya uingereza inafanya,angalia trend yake,mechi mbili za nyuma zote amepoteza na hii nilikuwa nina uhakika atafungwa,hii ni kawaida sana kwa Arsenal,ni kama kuna kitu kinapangwa ili kuzipa timu flani ushindi au kutengeneza mazingira yawe magumu kwenye kupata ushindi....
 
Umruhusu man city wakae juu pale kuwandoa tena huwa ni kazi sana.

wakishinda kiporo arsenal wanarudi juu. hofu yangu tu gape la point tatu ni dogo mno. yaani ukiteleza tu anakaa tena Yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…