Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Nianze kwa kutoa pongezi kwa JamiiForums.com kutupazia sauti kuhusu gharama kubwa iliyokuwa ikitozwa kupata huduma ya choo Mbezi stendi ya daladala, hatimaye bei imeshuka na kuwa sh. 200.
Bei ya choo ilikuwa kero kubwa sana hasa kwa watu wenye shughuli zao maeneo ya stendi, bei hiyo ilisababisha baadhi ya watu kujisaidia vichakani au kwenye mitaro na kusababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira na harufu kali ya haja ndogo maeneo ya stendi.
Leo nilikwenda pale ili kupata huduma hiyo nikatoa kiasi cha sh. 500 kama bei niliyokuwa nimezoea, nikastaajabu narudishiwa chenji ya sh. 300 nikamwambia muhudumu kuwa umenirudishia 300 ya kazi gani nimekupa 500 muhudumu akanijibu bei imeshuka sasa ni 200.
Hii imekuwa nafuu sana kwa watumiaji wa stendi ile, itasaidia kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira safi na nadhifu.
Pia soma: