Hatimaye Bojan Krkic aliyetabiriwa kama Messi ajaye amestaafu kandanda

Hatimaye Bojan Krkic aliyetabiriwa kama Messi ajaye amestaafu kandanda

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Bojan Krkic Perez, mzaliwa wa Catalunya, Spain miaka 32 iliyopita hatmaye ametangaza kusatafu kabumbu.

Bojan ambaye akiwa katika shule ya soka (akademi) ya Barcelona (La Masia) alikuwa anatajwa kama mrithi wa Messi au Messi ajaye.

Alikuwa anacheza kama mshambuliaji au winga, kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha huko La Masia, akapandishwa timu ya wakubww kwa haraka mwaka 2007 na alidumu mpaka mwaka 2011 huku akicheza na role model wake Lionel Messi kikosini.

Miaka ikasogea, Bojan hakuwa yule tena aliyetabiriwa makubwa, akajikuta anaondoka Barcelona mara baada ya kupata muda mchache wa kucheza. Akazurura kwenye vilabu vingi Ulaya kikiwemo Stoke City FC.

Baadae akatimkia zake Canada kabla ya kwenda Japan na kisha kustaafu. Wachambuzi wengi wa soka wanashangaa mpaka leo ni namna gani Bojan alishindwa kufikia matarajio ya wengi. Ni kama ilivyotokea kwa akina Jack Wilshere, Dele Alli, Tom Cleverley na wengineo na ndio imetokea kwa Bojan.

Anastaafu soka huku akimuacha role model wake akiendelea kusakata kabumbu🤣🤣

Adios Amigo Bojan👋🏼
 
Unfinished talent
crop-21567837.jpg
 
Neymar usimuweke kwenye hii List..huyu kijana akafanya makubwa
Nimemuweka wa mwisho kwa maana kwamba angementantain kiwango chake japo kwa nusu msimu ,tungesahau wakina Messi na CR7,let say musimu huu alianza vizuri akawazidi mbape na Messi kwenye contribution ya magoli kwa Psg ,Ila kwenye world cup mechi ya pili tu akaumia ,,,saivi Tena kaumia atakosa mechi zote za msimu huu

Yule neymer wa confederation cup 2013 asingekuwa na majeruhi ingekuaje??
 
Back
Top Bottom