Hatimaye CCJ chasajiliwa

Hatimaye CCJ chasajiliwa

Mwananchi

WAKATI kesho Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa akitarajiwa kutoa usajili wa muda kwa Chama cha Jamii (CCJ), taarifa zinaonyesha makao makuu ya chama yanarajiwa kuwa Mwananyamala.

Hatua ya CCJ kupewa usajili wa muda inakuja kipindi ambacho joto la siasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, likiwa juu.

Msajili wa Vyama Siasa John Tendwa akiweka bayana kwamba, atakuwa tayari kuhakiki wanachama wa CCJ hata ndani ya miezi mitatu wakimaliza kazi, taarifa zinasema tayari chama hicho kimeanza maandalizi makubwa.

Katibu Mkuu wa CCJ Renatus Muabhi, alithibitishia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kwamba, makao yao makuu yanatarajiwa kuwa Mwananyamala kama hakutakuwa na mabadiliko.

"Makao makuu yatakuwa Dar es Salaam eneo la Mwananyamala, tumejipanga vema kila kitu kiko vizuri tu hadi sasa tunaamini tutakwenda vizuri," alifafanua Muabhi.

Kwa mujibu wa Muabhi, CCJ itatangaza ofisi hiyo itakuwa mtaa gani kesho wakati wa mkutano na waandishi baada ya kupewa usajili huo wa muda na Msajili wa Vyama.

Muabhi alifafanua kwamba, chama kimejipanga vema katika kupanga safu ya uongozi imara ambao utawezesha kusukuma mbele ajenda za chama mara baada ya kuanza kukusanya wanachama.

"Baada ya kukusanya wanachama, tutapanga vema safu yetu ya uongozi kuanzia ngazi ya chini hadi makao makuu, tunachokifanya sasa ni kujiandaa kutimiza hilo la kukusanya wanachama," alisisitiza.

Kuhusu bendera, alisema bendera ya chama hicho siyo kama ya TANU kama ilivyoelezwa awali bali bendera ya chama hicho imefunikwa na rangi ya dhahabu.

CCJ ujio wake unaangaliwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa kama tishio kwa CCM, kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea Urais hapo Oktoba.

Tayari Spika wa Bunge Samuel Sitta, aliwahi kusema kwamba, haoni tatizo la kusajiliwa CCJ huku pia akisema hawezi kuzuia watu kumhisisha na chama hicho kama mgombea hapo Oktoba.

CCJ imekuwa ikitikisa nchi tangu taarifa zake kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, kwani kuna majina makubwa yanatajwa kuwemo akiwemo Spika Sitta, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, John Malecela, lakini wote wamekanusha.

Hata hivyo, mwasisi wa CCM Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kuonya kwamba bila CCM madhbuti nchi itayumba na upinzani wa kweli ungetoka ndani ya CCM onyo ambalo wadadisi wa mambo ya siasa anaona kama linakaribia.
 
Tendwa kishawapa usajili huo wa muda rasmi nusu saa iliyopita, picha zitafuata dakika si nyingi ambazo zitawekwa kwenye 1st post.
 
Tendwa kishawapa usajili huo wa muda rasmi nusu saa iliyopita, picha zitafuata dakika si nyingi ambazo zitawekwa kwenye 1st post.

Safi sana, but Tendwa said CCJ is a hoax...teh teh teh.siasa za bongo dizziness
 
Ndugu wana jamvi, demokrasia ya kweli na makini si mlolongo wa vyama.

Mlolongo wa mavyama mengi, ni dalili ya uroho wa madaraka, ubinafsi uliokithiri ukiambatana na u parpet. Kwa kuweka maslahi ya taifa nyuma na kutanguliza mbele maslahi binafsi.

Kamwe serikali ya CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuwa na mlolongo wa mavyama mengi. Bali CCM itahakikishiwa nafasi yake ya kudumu kulitawala taifa hili kwa kuwa na mlolongo wa mavyama.
Mawazo mazuri mkuu, ila umechokoza na haujaleta suluhu tufanyeje? Ni vyema pia ukakumbuka fitina ndani ya vyama vya upinzani hufanywa na CCM hiyo hiyo na mara nyingi zimekuwa zikitumika hata pesa kuwatoa nje ya track watu ambao wanaonekana ni threat kwao. Na kwa kuwa hata nchi tajiri zina watu maskini hali ni mbaya zaidi kwa nchi maskini na ndio maana siasa za kwetu zimejaa njaa nyingi na imekuwa ni rahisi mno kuwa trap viongozi wengi wa vyama vya upinzani kutokana na hali halisi ya njaa ndani ya vyama vyao.

Ni vyema sasa tukaja na suluhu ya kweli kama nchi tutoke vipi na tuvisaidiaje vyama vya upinzani?
 
It is a pity kuona watu wanakazania kutaka kujua majina ya vigogo wa CCJ badala ya kuangalia Katiba ya CCJ na Sera zake zina mwelekeo gani. Tanzania haitaendeshwa wala kukombolewa kwa majina ya vigogo bali nia thabiti ya kizalendo kuhakikisha nchi inarudisha heshima yake na kuleta maendeleo ya haraka kwa walio wengi. Tanzania imepoteza heshima yake ndani na nje ya nchi kutokana na kunuka ufisadi. Enzi hizo Wanigeria ndio waliokuwa wananuka kwa utapeli na sisi sasa tunasifika kunuka ufisadi! Sakata la rada peke yake limeweza kuchafua jina la Tanzania katika medani ya kimataifa ukiacha ufisadi wa ndani unaovuma kutokana na kesi zilizo mahakamani na ambazo bado zinapigwa danadana hazijafikishwa huko. Ufisadi umetanda kila kona ya nchi kwa kiwango cha kutisha. Fedha za Umma zinamung'unywa tu badala ya kuwasaidia wananchi kupata huduma za jamii na kuwaletea maendeleo wanayostahili.

Je CCJ ina mikakati gani itakayoirudishia nchi hii heshima yake na kuwaangalia asilimia 80 ya Watanzania wasiokuwa na uhakika wa maisha yao ya kila siku? Hayo ndiyo ya msingi na si kujua majina ya vigogo. Kukazania majina ya vigogo ni ku-underrate uwezo wa kuongoza wa Watanzania wengine ambao si vigogo. After all 'vigogo' ndio walioifikisha nchi hapa ilipo kwa kukaa kimya muda wote huu mpaka nchi inafika hapa.

BORAMAISHA

Sera pekee hazitoshi kwani ziko kwenye makaratasi tu,watekelezaji wa sera ni muhimu sana kuwajua. Kama kuna chama kinaongoza Tanzania kuwa na sera nzuri ni CCM ila watekelezaji ndiyo tatizo. Hawafuati sera zao wenyewe.

Tunataka kujua watu walio behind CCJ ili tuone kama wana integrity ya kutosha kuwafuata. Muhimu ni viongozi kwani sera zinatakiwa kupata watu wenye nia.

Mfano kuna kiapo kimoja iko CCM inasema.."Nitasema kweli daima,chuki kwangu mwiko" . Do you think wanafuata kiapo hiki? Au ni namna ya kudanganya wananchi.
 
Tendwa kishawapa usajili huo wa muda rasmi nusu saa iliyopita, picha zitafuata dakika si nyingi ambazo zitawekwa kwenye 1st post.

Asante Mkuu kwa taarifa hii. Nami lilipita pale ofisi ya msajili majira ya saa 6:40 nikakuta kelele nyingi sana pale na wamembeba kiongozi wao juu juu na mabango wao. Oh nilichoka sana na design ya wale wapambe wake!!! I doubt kama kitakuwa challenging political party (of course to exisiting parties, including CCM).
 
Tendwa kishawapa usajili huo wa muda rasmi nusu saa iliyopita, picha zitafuata dakika si nyingi ambazo zitawekwa kwenye 1st post.

Tunashukuru mkuu, hivi Tendwa wakati anasema CCJ is a Hoax alikuwa na maana gani au ndiyo yale yale ya wanasiasa wetu kuwa they dont mean what they say.
 
Mwananchi

Hatua ya CCJ kupewa usajili wa muda inakuja kipindi ambacho joto la siasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba, likiwa juu.

Msajili wa Vyama Siasa John Tendwa akiweka bayana kwamba, atakuwa tayari kuhakiki wanachama wa CCJ hata ndani ya miezi mitatu wakimaliza kazi, taarifa zinasema tayari chama hicho kimeanza maandalizi makubwa.

Amesema mwenyewe hata ndani ya miezi mitatu tusubiri tena aseme vinginevyo
 
Hakuna jipya kwenye hiki chama ila ni mambo yale yale na mwimbo ule ule kama vyama vingine na pia ukiona vyama kama hivi ni kiini macho ila kama kweli wapenda demokrasia wajiunge kwenye vyama vilivyopo
 
Kila la kheri CCJ, Mnachotakiwa kukifanya ni kuzungumza hasa, kwa hoja za haja! Kwa masula nyeti! Kwa wakati mwafaka! Na nia yenu iwe ni kujenga nchi sio kuganga njaa! Tuko pamoja!!
 
Hao wana CCJ waanzilishi lol... wanachekesha.. They dont appear to knw anything about hicho chama.. Full posho jelo jelo...
 
"You can have as many political parties as you like, as long as I remain The President" -- attributed to Mobutu Sese Seko Kuku wa Zabanga.
 
Tanzania Daima

HATIMAYE Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imeridhia kukipa usajili wa muda Chama Cha Jamii (CCJ), baada ya kukikwepa kwa zaidi ya miezi miwili.

Habari za uhakika zilizoifikia Tanzania Daima zinasema ofisi ya msajili jana ilimwandikia mwenyekiti wa muda wa CCJ, Richard Kiyabo yenye kumbukumbu namba RPP/CCJ/136/09, ikijibu maombi ya usajili wa muda.

Barua hiyo iliyoandikwa na Ibrahim Mkwawa kwa niaba ya msajili, ilisema itakikabidhi chama hicho cheti cha usajili wa muda Machi 2 mwaka huu saa tano asubuhi katika ofisi za msajili.

Ilieleza kuwa msajili ameridhika na maombi ya usajili wa muda wa chama hicho baada ya kukidhi matakwa ya sheria namba tano ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

“Hivyo basi, Msajili wa Vyama vya Siasa atakabidhi cheti cha usajili wa muda kwenu siku ya tarehe 2/03/2010 saa tano asubuhi kwenye ofisi ya msajili,” ilieleza sehemu ya barua hiyo ambayo Tanzania Daima ilipata nakala yake.

Licha ya kupatikana kwa barua hiyo, ofisi ya msajili imetaka kuongezewa nakala tatu za katiba ya chama hicho kabla ya kukabidhiwa rasmi cheti cha usajili wa muda mapema juma lijalo.

Jana, gazeti hili liliandika kuhusu ucheleweshwaji wa usajili wa muda hali iliyodaiwa kukwamisha utekelezaji wa baadhi ya mambo kwa lengo la kujiimarisha kama chama ili kukabiliana vilivyo kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Hata hivyo, ofisi ya msajili iliahidi kukutana na CCJ leo ili kuwapa maelekezo ya lini hasa watapata usajili wa muda, lakini katika hali ya kushtukiza, viongozi wa chama hicho walipokea simu zilizowataka kufika ofisini kwa msajili jana mchana.

“Tumepokea simu kutoka kwa msajili mwenyewe akisema kwa nini tumeamua kumshitaki kwa jamii, sasa ametuita… sijui anakwenda kuzungumza nini, tukishakutana nae mchana wa leo (jana) tutajua cha kufanya,” kilieleza chanzo cha habari chenye kuaminika kutoka CCJ na kuongeza kwamba, ahadi ya kukutana na msajili ilikuwa leo.

Awali, viongozi wa juu wa chama hicho walisema tayari chama chao kimetengeneza katiba, kanuni za chama, bendera, kadi na kwamba inao zaidi ya wanachama 3,000 kwa Dar es Salaam pekee, hivyo walikuwa wakisubiri kupata usajili kabla ya kukizindua rasmi.

Sehemu ya Katiba ya CCJ inaeleza: “Kwa kuwa Tanzania inao utajiri wa kutosha wa rasilimali unaoweza kuleta maendeleo ya haraka ya nchi kiuchumi na kuleta mabadiliko makubwa ya maisha kwa kila mwananchi ikiwa ombwe la uongozi litashughulikiwa.”

Sehemu nyingine ya katiba hiyo inaeleza kwamba itahakikisha utajiri wa rasilimali zilizopo unatumika kwa maendeleo ya wananchi kwa kuondoa umaskini, ujinga, na maradhi huku aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, uonevu, rushwa au ufisadi vinatokomezwa nchini.

Ujio wa CCJ umeleta mtikisiko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea urais Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wanadai kuanzishwa kwa CCJ ni mkakati wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo ina lengo la kupotosha umma kuhusu hatima ya CCM na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Vile vile, wanadai CCJ imeanzishwa ili kuupotosha umma unaoikosoa CCM, na kuumaliza nguvu upinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kimekuwa mwiba mkali kwa CCM katika miaka ya hivi karibuni.

Baadhi ya vigogo wa CCM wanaohusishwa na CCJ ni Spika wa Bunge Samuel Sitta, makundi ya wanachama na viongozi waliojiweka mbele kupambana na ufisadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba na John Malecela. Lakini wote wamekanusha jambo hilo.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, hatua ya vigogo hao kuikana CCJ ni mwanzo mbaya na fursa iliyopotea ya kukikuza na kukijenga chama hicho. Wapo baadhi ya vigogo waliojitambulisha na chama hicho, lakini hawataki kutajwa majina magazetini kwa sasa.

UPDATE:

March 02, 2010

ccj3.jpg

ccj1.jpg

ccj2.jpg

CCJ yapata usajili rasmi

Hawa jamaa ni wa UWT; angalia hata uvaaji wao mara nyingi vijana wa SYSTEM huvaa t-shirts nyeupe ndani halafu juu ndio inafuata Kaunda suit kama alivyovaa huyu jamaa wa kulia!!!The whole thing seems to have been stage managed.
 
Kama ni UWT wa bongo watajulikana mapema sana huwa hawajui kujificha
 
I don't have any interest in ccj, but this is a haux for real, just like mreamas' cases were in those days.
Hivi ukiishinda serikali ndo nakuajebbaadae? Serikali inafungwa au? Au ndo bwah blah.
Sheria sijui mm, fundi wa matrekta.
 
*ATOA USAJILI WA MUDA, ATANGAZA KUKICHUNGUZA KUANZA SIASA KABLA YA USAJILI

SIKU moja kabla ya kutoa hati ya usajili wa muda hapo jana kwa Chama Cha Jamii (CCJ), Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, tayari aliiweka hatma ya kisiasa ya chama hicho njia panda baada ya juzi kutangaza kuanza uchunguzi kuona kama kilianza shughuli za kisiasa miaka miwili iliyopita kabla ya usajili.

Jana Tendwa alihitimisha safari ya miezi miwili ya CCJ kusaka usajili wa muda, lakini tayari akiwa amekiweka pabaya chama hicho, baada ya juzi kunukuliwa na kituo cha ITV akisema ofisi yake inafanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kama chama hicho kilianza siasa kabla ya kusajiliwa miaka miwili iliyopita na ikithibitika atakifuta.

Kauli hiyo ya kitisho ya Tendwa akiitoa siku moja kabla ya kukabidhi hati hiyo huku akisisitiza kwamba, chama hicho kitapaswa kufuata taratibu za kisheria katika utendajikazi wake.

CCJ chama ambacho kimesababisha mtikisiko ndani ya CCM kimekuwa kikifuatilia usajili wa muda katika Ofisi ya Msajili kwa karibu miezi miwili sasa tangu kuwasilisha maombi yao Januari 20, mwaka huu.

Hofu ya CCJ kuanza kazi za kisiasa miaka miwili nyuma, inaangaliwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa kama inayotokana na nguvu zake ikiwemo mtandao mpana nchi nzima huku viongozi wake wakitangaza jana kwamba, wanatarajia kukamilisha kazi ya kuzunguka nchi na kupata idadi ya wanachama 200 katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu baada ya kupata hati hiyo badala ya miezi sita.

Habari zaidi zinadai kwamba kwamba baadhi ya vigogo serikalini na katika CCM walikwishafuatwa wakiwemo wakuu wa mikoa ambao baadhi walikubali kuunga mkono na wengine kukataa.

Lakini wakati Tendwa akitoa hati hiyo na onyo la kukifuta chama hicho, Mwenyekiti wa CCJ Richard Kiyabo, alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa tuhuma mbalimbali dhidi ya chama hicho na kusema hakina uhusiano wowote na Idara ya Usalama wa Taifa kwani mpango huo una lengo la kukivuruga ili kionekane ni chama pandikizi.

Kiyabo alifafanua kwamba, CCJ ni chama tofauti na vingine vya upinzani kwani kimejipanga vema kuhakikisha kinakidhi mahitaji ya msingi ya kidemokrasi kwa Watanzania.

"CCJ siyo chama cha Idara ya Usalama wa Taifa, ni chama cha usalama wa maisha ya Mtanzania, ni chama makini tofauti na vingine vya upinzani kwa hiyo kuna tofauti kubwa," alisisitiza.

Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akibebwa juu pamoja na katibu wake Renatus Muabhi na baadhi ya wanachama waanzilishi, alisema lengo, nia na madhumuni ya CCJ ni kushiriki uchaguzi wa Oktoba.

Aliweka bayana mkakati huo kwamba, katika kufanikisha azma hiyo CCJ imejipanga kukusanya wanachama wanaotakiwa kisheria ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na nusu.

"Tumejipanga kushiriki uchaguzi, nia tunayo na hadi sasa maandalizi ni mazuri tu kwani tutaweza kukusanya wanachama wetu ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na nusu," aliongeza.

Kuhusu usajili wa wanachama, alisema tayari walizundua mchakato huo rasmi siku hiyo ya jana baada ya kupata usajili huo na kuongeza: "Hata ninyi waandishi wa habari mnakaribishwa."

Akizungumzia kuhusu kuwepo vigogo ndani ya CCM, Kiyabo alirudia kwamba wao wanalenga wanachama 20 milioni na hadi sasa hawana vigogo wowote ndani ya chama hicho tawala.

"Sisi hatuzungumzii sijui vigogo, hatuna vigogo ndani ya CCM tunachozungumzia ni namna ya kuwapata wanachama 20 milioni nchini kote, inawezekana sasa wanachama ukichanganya na CCM waliopo ni 10 milioni," aliongeza.

CCJ ujio wake unaangaliwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa kama tishio kwa CCM na Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Tayari Spika wa Bunge Samuel Sitta, aliwahi kusema kwamba, haoni tatizo la kusajiliwa CCJ huku pia akisema hawezi kuzuia watu kumhusisha na chama hicho kama mgombea hapo Oktoba.

CCJ imekuwa ikitikisa nchi tangu taarifa zake kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, kwani kuna majina makubwa yanatajwa kuwemo akiwemo Spika Sitta, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, John Malecela, lakini wote wamekanusha.
Hata hivyo, mwasisi wa CCM Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kuonya kwamba bila CCM madhbuti nchi itayumba na upinzani wa kweli ungetoka ndani ya CCM onyo ambalo wadadisi wa mambo ya siasa anaona kama linakaribia.

SOURCE: MWANANCHI.
 
%5Cccjmwenyekiti.jpg
Baadhi ya mashabiki wa chama kipya cha siasa CCJ, wakimbeba Mwenyekiti wa chama hicho Richard Kiyabo baada ya kutoka kwa Msajili wa vyama vya siasa alipokabidhiwa cheti cha usajili wa muda jijini jana.

*ATOA USAJILI WA MUDA, ATANGAZA KUKICHUNGUZA KUANZA SIASA KABLA YA USAJILI

Ramadhan Semtawa

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18295
 
Back
Top Bottom