Hatimaye CCJ chasajiliwa

Hatimaye CCJ chasajiliwa

Yataibuka mengi kabla ya uchaguzi mkuu. Kama Tendwa atakifuta chama hiki au kukataa kukisajili mapema ili kisishiriki uchaguzi mkuu, nitaamini kuwa kuna vigogo wa CCM ndani kwani Tendwa anafanya kazi ya CCM.
Hao wanaotajwa kuwa wanatoka CCM si wajitokeze wazi wazi? wanaogopa nini? Kwani siasa mpaka uwe CCM?
 
Tendwa, si uwaache tu CCJ? wananchi wa sasa ni waelewa zaidi ya wale wa 1947. Hakuna ajuaye watanzania wa sasa wanawezaje kupata kile wanachokitaka wenyewe.
 
  • Baada ya usajili tu yazoa wanachama 2,400 Dar es Salaam
Maelfu ya watu mkoani Dar es Salaam wamejiunga na Chama kipya cha Cha Jamii (CCJ), ikiwa ni siku moja tangu kipate usajili wa muda.

Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, aliliambia Nipashe kuwa hadi kufikia jana, jumla ya watu 2,400 walikuwa wamegawiwa kadi, huku wengine wakiwakataa kutokana na kutilia shaka dhamira yao ya kujiunga na chama hicho.

Nipashe ambayo ilifika katika ofisi za CCJ jana, ilishuhudia watu hao, ambao wengi wao wakiwa ni vijana pamoja na wafanyabiashara ndogondogo ‘wamachinga’ wakiwa wamemiminika katika ofisi hizo zilizoko Mwananyamala, huku kila mmoja akiwania kununua kadi za chama hicho.

Pia, makundi ya vijana wenye hamasa na shauku kubwa ya kutaka mabadiliko ya kisiasa nchini, walishuhudiwa wakiwaomba viongozi wa CCJ kadi ili wakazigawe maeneo mbalimbali, huku wengine wakiwaomba viongozi hao idhini ya kwenda kuchapisha fulana za chama hicho kwa gharama zao wenyewe. Watu hao walianza kumiminika katika ofisi za CCJ juzi, muda mfupi baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kuwakabidhi viongozi wa chama hicho cheti cha usajili wa muda.

Muabhi alisema kati ya idadi ya watu waliogawiwa kadi, 800 walijiunga na CCJ juzi na 1,600 walijiunga jana. “Ni wengi sana wanaokuja kama unavyoona hapa. Wengine tumewakataa, tuna wasiwasi nao. Sababu kuna watu wanaweza kutumika kutuharibia. Ni lazima tuwafahamu. Kwa mfano, mtu anakuja hapa hana hata kadi ya mpiga kura, sasa hapo tutampokeaje katika chama?” alihoji Muabhi.

“Hatuna uchu wa aina hiyo, sababu tunakubalika. Tunataka watu makini, wenye moyo wa huruma, wazalendo, wenye uchungu na nchi na waje na maelezo ya kutosha kuonyesha uasili wao katika jamii,” aliongeza.

Alisema tangu juzi wamekuwa wakipokea simu na ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) kutoka kwa watu mbalimbali mikoani, ambao wanawasubiri wafike ili wajiunge na chama hicho.

Muabhi alisema baada ya kukamilisha uhakiki wa wanachama 200 mkoani Dar es Salaam wanatarajia kwenda kufanya ziara katika mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Morogoro, Pwani na Unguja na Pemba.

Naye Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo, alisema wanatarajia kukamilisha uhakiki wa wanachama wao katika mikoa 10 ndani ya muda mfupi kabla ya kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa maombi ya usajili wa kudumu.

Kabla ya chama hicho kukabidhiwa cheti cha usajili wa muda, ulizuka uvumi kuwa baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wangejiengua na kujiunga na CCJ. Taarifa hizo ziliwafanya baadhi ya vigogo wa CCM kujitokeza na kutoa kauli za kuibeza CCJ kwamba hakina ubavu wa kubomoa chama chao.


CHANZO: NIPASHE
 
Naombeni kuuliza.hivi wanapaswa kuwa na wanachama wangapi ili wapewe usajili wa kudumu?
 
Chadema mko wapi wenzenu wa ccj ambao ni wachanga wanagombewa na wananchi nyie mnagombana tuu,upuuzi!
 
Jamaa wanatafuta mshiko tu kipindi hiki cha uchaguzi, mbona wasianzishe mapema ili wajipange uzuri kama nia yao ya dhati ni kujipanga kumkomboa Mtanzania?

Ndio wale wale tu kama jina lao linavyojieleza CCJ (sisi je). Baada ya kuona wenzao chama cha mananihii wanakula kiulaini, wakajiuliza 'na sisi je?
 
nimesema tatizo la Tanzannia ni uongozi; CCJ watawala watu wa kawaida kile ambacho wamenyimwa na wengine..
 
Muabhi alisema kati ya idadi ya watu waliogawiwa kadi, 800 walijiunga na CCJ juzi na 1,600 walijiunga jana. "Ni wengi sana wanaokuja kama unavyoona hapa. Wengine tumewakataa, tuna wasiwasi nao. Sababu kuna watu wanaweza kutumika kutuharibia. Ni lazima tuwafahamu. Kwa mfano, mtu anakuja hapa hana hata kadi ya mpiga kura, sasa hapo tutampokeaje katika chama?" alihoji Muabhi.

Sidhani kama hiko ni kigezo cha kuwakataa wanachama kwani ninavyojua mimi muda wa kujiandikisha bado upo, so wangejiandikisha hata baada ya kuwa wanachama.

Labda kama kuna sababu nyingine ya msingi.
 
Lets wait and see as the events unfolds! Maana duu kama kweli kuna kundi litameguka CCM kwenda CCJ baadaye mwakani basi ushindani wa ukweli utakuwepo kwenye uchaguzi wa mwaka huu
 
kweli hawa jamaa ni watu makini hadi kuweza kujiunga nao, bado napata shida juu ya hilo labda hadi hapo hao vigogo wanaodaiwa wapo watakapo jitokeza isije kuwa ni chama cha vigogo wanaolalamikiwa kuwa mafisadi wameamua kuanzisha chama
 
Huwa nasikia msemo usemao " kama huwezi kupambana nao, ungana nao", "mnaowadhania" wameshindwa kupambana nao wakiwa pamoja, watawaweza wakiwa nje?
 
kweli hawa jamaa ni watu makini hadi kuweza kujiunga nao, bado napata shida juu ya hilo labda hadi hapo hao vigogo wanaodaiwa wapo watakapo jitokeza isije kuwa ni chama cha vigogo wanaolalamikiwa kuwa mafisadi wameamua kuanzisha chama

Hata mimi hofu yangu ni hiyo.
lakini je kama ni kweli cha hao vigogo na sera zao zinalipa kuna tatizo?
 
nimesema tatizo la Tanzannia ni uongozi; CCJ watawala watu wa kawaida kile ambacho wamenyimwa na wengine..

Though ni Out of Point lakini Mwanakijiji Asante Kwa Hii Avatar yako, ni ile uliyonza nayo Mapambano
 
I smell ukombozi tokana na chama hiki.
Kama kuna mtu alitazama TBC1 LEO katika kipindi cha JAMBO, yule mtangazaji Marina H.Marin anajaribu kukikandia sana chama hiki, wakati msajili Tendwa anajibu very fairly!...Sijui TBC wana hila gani na chama hiki...I HATE THEM!
 
Back
Top Bottom