Hatimaye CCM, kwa kuipakata DP world, yathibitisha ni genge la ulaji lisilo na uadilifu wala uzalendo!

Hatimaye CCM, kwa kuipakata DP world, yathibitisha ni genge la ulaji lisilo na uadilifu wala uzalendo!

Kwa hiyo bila shaka hata wewe unashangaa kama ninavyoshangaa mimi.
Hayo yote uliyo yaorodhesha ili kuiwezesha CCM kutoka madarakani yataanzia wapi iwapo ni CCM hao hao ndio wanatakiwa wawafanyie hisani waTanzania ili mambo hayo yafanyike?

Jameni, hebu acheni kuifanya CCM, tena hii ya Samia (?), ionekane kama wao ndio wanaotufuga binaadam wote wa nchi hii.
Mkuu ugumu upo hapo kwamba, unayemtaka atoke kwenye uongozi ndiye mwenye mamlaka ya yeye kutoka kwenye huo uongozo/madaraka. Hapo ndipo penye ugumu na hasa ukizingatia wa-TZ wengi hawana elimu ya siasa.
 
inaongozwa na individual mwenye nguvu ya ushawishi anayeamua atupeleke wapi, kama huyu ameamua kutupeleka utumwani kwa wajomba zake, wengine wakamsapoti.
Ninakuelewa unachoeleza mkuu 'denooJ'; ila kama ni "nguvu ya ushawishi", sioni nguvu hiyo akiwa nayo Samia. Tokea hili swala la DPW lianze, nimesikia tu mara moja akilizungumzia akiwa Mwanza, kwa kusema kuwa "Yeye ni mTanzania".

Au una maana ya "nguvu ya ushawishi" inayotegemea matumizi ya nguvu?
 
Kataika mambo ya ovyo yaliyofanya na ccm ili ni kubwa sana na halitaweza kuiachq salaama kama hayo mengine kama wanafukilia hili litapita kama mengine ni kujidanganya
 
Mkuu ugumu upo hapo kwamba, unayemtaka atoke kwenye uongozi ndiye mwenye mamlaka ya yeye kutoka kwenye huo uongozo/madaraka. Hapo ndipo penye ugumu na hasa ukizingatia wa-TZ wengi hawana elimu ya siasa.
Mimi ninaona tofauti kabisa na wewe; hasa kuhusu hilo la "wa-TZ wengi hawana elimu ya siasa."

Haya yanayoendelea sasa chini ya CCM, hayajawahi kutokea hata mara moja katika uhai wa CCM; angalau hata huko nyuma CCM waliweza kufanya maigizo kidogo ili waonekane wapo kwa maslahi ya nchi na wananchi wao.

Sasa imekuwa wazi kabisa kwamba CCM haipo kwa maslahi mapana ya wanachi, na ni hao wananchi sasa watakaoamua kutokana na upeo wao wa siasa walio nao kuleta mabadiliko.

Ninakuomba ukisome vizuri kichwa cha mada hii aliyoiweka hapa mkuu 'Mag3'.
Nisingeweza kuchagua kichwa cha mada kilicho sahihi zaidi ya hiki alichokitumia mleta mada.
 
Kwa kweli na bila kumung'unya maneno hilo ni genge la wahuni...mods please do the needful!
Ni wahuni tu wanaweza wakaridhia mkataba wa hovyo kama huu wa DP World

cc:Active, BlackBold, Boqin, Cookie
Hapana.
'Heading' ilivyo sasa, ndiyo sahihi kabisa.
"uhuni" tu, wa aina hii kwa minajili ya nini?

This is serious stuff.
 
Hapana.
'Heading' ilivyo sasa, ndiyo sahihi kabisa.
"uhuni" tu, wa aina hii kwa minajili ya nini?
Inatia uchungu! Wakati mwingine mtu unaweza tu kubaki umeduwaa kwa yanayotendeka nchini kwani mengi yanashangaza, yanaudhi na kukasirisha.
This is serious stuff.
Agreed, serious stuff indeed! Nchi imepoteza dira na waliotufikisha huko tunashirikiana nao, tunakula nao na tunalala nao.

We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them. To even entertain such notion, that we can, is shear madness.
 
Back
Top Bottom