Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

"Eudorite, post: 19093534, member: 266448"]Soma tena. Nimeandika kama kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.
Tumekuuliza sana hutaki kujibu.

Tusaidie kuelewa umuhimu wa kujenga Chato ni upi kwa mujibu wa hoja yako?
Tunapinga ujenzi wa uwanja wa chato pasipo kutoa sababu za maana ndiyo sababu kuna ubishani hapa.
Hakuna anayepinga, tunahoji sababu za kiuchumi, kijaamii, kilinzi n.k.

Hakuna anayetueleza ni zipi ukiwemo wewe.
Tutaendelea kuhoji unless utueleze
Sababu za idadi ya watu na za kiuchumi zina walakini kwani watakaotumia uwanja huo su wakazi w chato pekee.
Ndiyo, tueleze kwa jiografia, shughuli za uchumi n.k. ni wakazi wa eneo gani jingine?
Mchumi makini lazima aangalie na shughuli za kiuchumi zilizopo jirani na uwanja huo. Kwa sasa na baadae. Hapo ndipo tunapaswa kujadili
Tueleze basi shughuli gani za kiuchumi ziwe Chato au kuzunguka hapo zinazoelekeza Ujenzi wa Chato airport
 
Maumivu ya kichwa huanza poolepoole,tumeanza na uwanja wa ndege Chato,tutakuja na Ikulu ya Tanzania Chato,tutafuata na kutoa maamuzi na uongozi wote wa nchi tukiwa Chato,mwisho tutahamishia serekali na makao ya nchi Chato.
 
Mbona hamuulizi uwanja wa shinyanga uko ibadakuli km 50 kutoka shinyanga mjini.
Umeleta hoja nzuri sana.
Kama tungetakiwa kujenga kiwanja basi ingekuwa Ibadakuli Inter airport

Williamson diamond -Mwadui imekuwepo kabla ya Uhuru.
Kilichopo ni uwanja mdogo wa kukidihi mahitaji ya eneo na wakazi

Wakazi wa Shinyanga hawahitaji uwanja wa ndege.
Walichohitaji ni MAJI, sote tukubaliane tu jitihada za Lowassa haziwezi kuwekwa pembeni

Kipaumbele hicho kimeinua maisha ya wananchi wa Shinyanga, kwa shughuli, afya na elimu. Mradi unaendelea hadi Dodoma

Huo ndio uwekezaji wa akili.

Leo Shinyanga ingekuwa na uwanja mkubwa, watumiaji pengine wangekuwa 500, kinyume na mamilioni ya watu wanaotumia maji sasa

Kipaumbele cha pili Shinyanga ni miundo mbinu ya usafiri

Tuliunga mkono uwekezaji wa reli ya kati katika kiwango cha SG ni muhimu.

Hakuna aliyelalamika in fact tulishangaa kwanini mradi haujaanza

Mradi wa Reli utasaidia shughuli za kiuchumi nchi nzima.

Utakuwa ni network kuanzia Mtwara hadi Musoma, Tanga hadi Kigoma.

Huu ni uwekezaji wa akili unaoweza kuelezwa kiuchumi, kijiografia, kiusalama na kijamii

Tunahoji, Chato imelenga nini?
 
Kwani

Wabunge wa Upinzani na Community yote ya Wapinzani mbona wamekaa kimya? Yetu macho na masikio. Hivi hapo Chato kila mkazi ana Maji safi ndani, hospital, shule,Na nyumba bora?
Wakiongea wanampa akili ya kufanya acha wakae kimya
 
Miezi saba ishindwe kukamilika runway,kuweka windsock na eneo la Apron?
Mbona JNIA ile rehabilitation iliyofanywa na Interbeton ilikuwa inafanyika huku operations zinaendelea?
Kufikia April yaani kiezi saba tangu ujenzi kuanza,vitu kama runway,apron na uwekaji wa windsock vitakuwa tayari...

Heri ya Mwaka Mpya mkuu Ngapulila
 
Geita unaijua? wapi utajenga uwanja wakati imezungukwa na milima, halafu watu walivyosongamana utamhamisha nani na umpeleke wapi? Mbona hamuulizi uwanja wa shinyanga uko ibadakuli km 50 kutoka shinyanga mjini.
Hapana. uwanja wa shy ni km 8-10_) kutokana shy mjini
 
Tukundane

Tayari mmeambiwa shughuli za kiuchumi zilizopo karibu na chato na si kwamba wewe na mwenzako hamzifahanu.

Mmeambiwa kuna mbuga za wanyama hapo jirani na mashapo ya madini.

Hapo kuna potential kubwa ya shughuli za utalii uvuvi kilimo na uchimbaji wa madini.

Chato pia imezungukwa na miji inayokua kwa haraka na imetajwa hapa.

Makao makuu ya mkoa wa geita hapafai kujenga uwanja maana ardhi ni adimu na imejaa dhahabu. Huwezi jenga uwanja juu ya dhahabu. Hivyo chato airport itakuwa ni uwanja wa mkoa husika.

Mwisho niwaombe wewe na wenzio kuthibitisha kwamba chato panajengwa uwanja wa KIMATAIFA. Ni juavyo panajengwa uwanja wa kawaida kawa wa Tabora Dodoma au Mpanda. Hili la kusema Chato INTERNATIONA Airport ni upotoshaji na ni makosa.
 
Geita unaijua? wapi utajenga uwanja wakati imezungukwa na milima, halafu watu walivyosongamana utamhamisha nani na umpeleke wapi? Mbona hamuulizi uwanja wa shinyanga uko ibadakuli km 50 kutoka shinyanga mjini.


Kwa hiyo kumbe Geita maana yake ni Geita mjini? Sikumaanisha hivyo. Ninaifahamu Geita kwa upana wake, undani na uhalisia wake nadhani inawezekana kuliko hata wewe. Twende pamoja.
 
Kwa hiyo kumbe Geita maana yake ni Geita mjini? Sikumaanisha hivyo. Ninaifahamu Geita kwa upana wake, undani na uhalisia wake nadhani inawezekana kuliko hata wewe. Twende pamoja.
Kwa unavyoielewa Geita unafikiri huu uwanja ungefaa kujengwa wapi?
 
Kwa unavyoielewa Geita unafikiri huu uwanja ungefaa kujengwa wapi?

Ninatamani sana kujua nia ya kuujengea chato ilikuwa ni nini hasa. Pengine mtazamo wangu unaweza uwe mbali na malengo ya mwenye nao.
 
Ninatamani sana kujua nia ya kuujengea chato ilikuwa ni nini hasa. Pengine mtazamo wangu unaweza uwe mbali na malengo ya mwenye nao.
jamani huu sio Airport kama mnavyotafasiri ni Landing Airstrip tu kama zile za wamissionary wa MAF kule kibondo nassa ilongero au kama viuwanja vya mgodini, lakini misukule ya ufipa ndio imeshupaza shindo
 
Mkuu inauma sana. Halileti mantiki hili kabisa. Sijui atakuja na sounds zipi kuhusu hili
 
Hivi, Chato IPO nchi gani?
 
Upo makini kujibu.Tusubiri mwezi wa NNE mwakani kuhitibisha huu mjadala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…