Acha ushabiki usiokuwa na tija. Chato haihitaji airport kubwa hivyo, ingewekewa airstrip tu kama ile ya buzwagi kahama ingefaa kabisa mkuu akitaka kwenda kwake anatua vizuri tu. Ulishafika chato? Kaangalie kioja cha traffic lights za chato, gari ni za kuhesabu, inabidi ziongoze mikokoteni inayovutwa na punda, sasa kwa usawa huo hao wasafiri wa kupanda ndege hapo watatoka wapi? hakuna biashara kubwa chato au kivutio chochote cha utalii!!! Mbaya zaidi hata sehemu zinazoizunguka chato ziko hoi kiuchumi!!! Itazame biharamulo, bwanga, buziku , ngara, muleba, hao abiria watatoka wapi? Nakuhakikishia hakuna shirika la ndege litapeleka ndege zake hapo kwasababu hakutokuwa na abiria, itakayotua hapo ni ndege ya Rais tu, na akistaaf ndo ujue utakuwa mwisho wa matumizi ya uwanja huo. Uzalendo uko wapi kwenye mradi huu??