Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

uLevi wa madaraka
alafu unaomba uombewe ili iweje kwa ufisadi huu.
na hapohapo umekula hela za rambirambi za bukoba
siombeagi mafashisti mimi
 
Sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,
mkuu kwa hiyo maeneo mengine yasiyo na kiongozi yatafaidika vipi, kwa mfano maeneo ya kusini lini watajengewa huo uwanja wa ndege?

Hakuna dhambi mbaya kama ubaguzi kamwe.
 
Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Hata Mimi kwa jicho la UKADA ni majungu lakini kitaalam Barafu ameongea sana point aisee hasa kiuchumi na fikra baada ya awamu yetu hii ikiisha.
 
barafu,

Well said mkuu, duu hii kwel ni critical thinker umefafanua vizuri sn mkuu mawazo kama haya yangekuwa yanafanyiwa kaz na watawala tusingekuwa hapa tulipo.

Kwel JamiiForums ni mwisho wa yote ktk kuwasilisha fikra pevu. Big up sana mkuu ujumbe umewapata wahusika maana najua huwa wanatembelea sana hum, japo wanakomaa kuiondoa hii midia ili tusione pambanuzi kama hizi.
 
Kipigi,

Toa faida za Chato airport!! Wacha kupiga makelele, mtoa mada katoa uchambuzi wa kitaalamu wewe unaanza kuingiza chuki zako kwa wakaskazini!!

Mtoa mada katoa pendekezo kuwa uwanja wa Mwanza ungeboreshwa kwa faida za kiuchumi kuliko huo wa Chato ambao ni kama tu mali ya watu wawili au watatu(maana ndiyo wanaomudu kupanda ndege huko chato) Mh marehemu Deo filikunjombe aliwahi kumuuliza Mh waziri mkuu mstaafu Pinda kuhusiana na faida za ujenzi wa kiwanja cha ndege huko sumbawanga! Tena Deo alikuwa akipinga vikali hizo white elephant projects kuwa hazina faida!! Deo hakuwa wa kaskazini wala hakuwa CHADEMA.

Wewe endelea kuwabinukia wakubwa! Wa kuhoji wapo! Na watahoji tu
 
Uwanja umeshajengwa, mvimbe mpasuke mtajijua wenyewe.

Watetea mafisadi na wabaguzi wakubwa nyinyi( malofa)
 
Kipigi

Angejenga barabara nzuri basi ambayo ingetumika na wengi kama ilivyo barabara za Kaskazini.

Lakini kajenga uwanja ambao atakuwa anautumia yeye tu sana sana na wachina wezi wanaoiba rasilimali zetu.

Hata sijui ulikua unafikiria nini wakati una comment.
 
barafu,

Kwa hizi nondo/facts lazima na jinsi jamaa hawezi tolerate criticism. Unawaamsha mapepo.

NB: msiende likizo asee bado tunahitaji more facts
 
Umemwaga Povu lakini umeshindwa kujibu Hoja za barafu...
Uwanja wa Chato una Manufaa gani Kiuchumi z
 
aisee!!
 
Mfano nikuulize. Hivi walipoamua kujenga uwanja wa KIA hapo ulipo miji ya Moshi Arusha na Boma Ng'ombe ilikuwa na watu wangapi wakati huo. Kwa nini wasingepanua kiwanja cha moshi au cha arusha vilivyo kuwepo.
Hoja hii inatokana na mapungufu ya kutafuta habari kwa kina

Tulijadili sana hapa JF kwaini KIA ilijengwa.
Mpango wa pili wa maendeleo 1964-1969.
Tazama sababu za ujenzi wa kiwanja hicho na historia yake
Ujenzi wa uwanja wa chato ni muhimu na haujakwamisha wala kuzuia ujenzi wa viwanja vingine muhimu vya Mwanza Tabora Mpanda Mbeya Shinyanga Simiyu Mara Bukoba Kigoma Singida nk.
Ni fair point, usiishie hapo tueleze kwa ukubwa unaotarajiwa nini faida za ujenzi wa uwanja huo? Hicho ndicho muhimu kujadili hapa
Ni jukumu letu kuonyesha umuhimu wa ujenzi au upanuzi wa hivyo viwanja vingine tunapojadili ujenzi wa kiwanja cha chato, na kupiga kelele hivyo viwanja navyo vijengwe. Kuliko kukashifu uwanja kujengwa chato.
Tunarudi pale pale, kuwekeza lazima kuwe na sababu.
Hatuwezi kuwekeza kiwanja kikubwa Segera bila sababu.

Hakuna kashfa ya Chato, ni hoja yasababu nzuri ziwe za kiuchumi, kijamii au kiusalama Tunaomba msaada wa hilo
Kuna tatizo gani kila walaya kuwa na kiwanja bora cha ndege kama kinalipa?
Hakuna tatizo kabisa.

Korogwe ilikuwa council wakati wa Mkoloni.
Ni Moja ya Wilaya kongwe katika taifa hili, haina Kiwanja.

Tunduru ni Wilaya Kongwe katika Taifa hili, kiwanja chake ni airstrip tu

Hatuhitaji kiwanja nyumbani Bondei- Muheza kwasababu ni saa 1 kutoka Pongwe Tanga

Hatuhitaji Kiwanja Kisarawe kwasababu ni saa 1 kutoka JNIA

Hatuhitaji likiwanja likubwa Mkuranga na Nyamato kwasababu ni saa 1 kufika JNIA

Tunahitaji kuwekeza kwa malengo.

Hatuhitaji uwanja mkubwa Kigoma, tunahitaji Reli ya STG na daraja la maragarasi kwasababu kiuchumi ina maana sana.

Hoja yako kila Wilaya iwe na kiwanja ni mfu.

Hatuhitaji kiwanja Kibaha na ni ujinga uliotukuka kuwekeza tu likiwanja kwasababu baada ya miaka 20 litakuwa na faida

Ni akili pevu kama fedha hizo zitajenga reli ya Mtwara-Liganga

Hatuhitaji likiwanja likuubwa Wilaya ya Butiama ili watumie watu 6.

Tunahitaji fedha hizo kujenga reli ya kuunganisha Musoma na Mwanza

Inatosha
Mie namwomba JPM na.... aendelee pale Mugumu kuweka kiwanja cha kisasa maana jamaa anaonekana ni mtaalamu wa ujenzi maana anaweza kujenga hivi viwanja kwa muda mfupi.
Ningemuomba JPM na serikali yake wafikirie kuunganisha reli ya kati ifike Musoma

Uwanja wa Musoma ulikuwa kama airstrip wakati huo EA Airways DC 10 ikitua.

Niliona kwa macho yangu wakati mkuu wa mkoa akiwa Kisoki kama si Wasira na Mkurgenzi akiwa Marehemu Khalidi aliyejenga Makondeko.

Ndege ziliposhindwa kutua mkandarasi aliyeweka 'moram' ni P.F.Nyakutonya

Hii Jet ya Rais ilifanyiwa majaribio baada ya uwanja kukamilika.

Mgeni wa kwanza kutua ni Chancellor wa Ujerumani Wilbrandt akimtembelea Nyerere Butiama

Nyerere hakukifiri njia nzuri ni kujenga kiwanja kikubwa.

Mahitaji ya watu wa Mara yalikuwa Daraja la Kirumi lililojengwa na Maulidad & Ross.

Matete yalibomoa kwanza,niliona nikitoka Kinesi, niliogopa boti za Hosea na maji
Tukapita pale Kirumi kwa kivuko ambacho kilikuwa ni hatari

Daraja la Kirumi lilitumika na KAMATA na Tanganyika Bus wakati yanapitia Kenya kwenda Mwanza. Barabara ya kati ilikuwa haipitiki kwa baadhi ya nyakati

Kirumi ni kiungo kizuri hadi sasa kati ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda

Huo ndio uwekezaji wenye tija.

Nyerere angeweza kujenga uwanja mkubwa tu Butiama

Alifikiria Taifa kwanza na si yeye kama mtu

Hapa niwaalike wakubwa tutete ya enzi Jasusi na JokaKuu
 
Nimelipenda tu bango lako limeeleza yote ila wenye stroke kwenye Ubongo watakuja wanalia kumsifia mwenyekiti
 
Ni bora mara kwa 100% waziri mkuu aliyepeleka duka la MSD jimboni kwake ikiwa hata mkoani hakuna kuliko haya ya Chato. Ni aibu hata kusimulia kwa mwingine!
 
Nimeona picha za Rais akiwa ameenda kuwafariji jirani zake, kwenye Gazeti la leo 30.12.2016 Mwananchi.

Ni aibu sana, jirani zake wanaishi kwenye nyumba duni sana, za tope

Sijui Rais anajisikiaje kujenge kiwanja cha ndege kwa Nyumba kama hizo za jirani zake.

Lakini pia yale matamko yake anajisikiaje akiwa na jirani zake wa hali hiyo?

Time will tell
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…