Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Kwanza Nikiona post za dizaini hii huwa nakuwa disapoited sana. Hivi mnadhani kila mtu ameshikiliwa akili zake na watu wengine? Kwanini kila nayeeleza mapungufu ya kitu fulani kwenye serikali laziama apewe jina la upinzani? Hivi kwakuwa wewe ni mtu wa kusifia hata pale ambapo mapungufu ni shahiri dhahiri unadhani kila mtu yupo hivyo?

Pili, hizi hoja za ukaskazini,umagharibi nk unazitoa wapi? Huu mtizamo wa kibaguzi baguzi unakusaidia nini? Hafu unasema "kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,[/QUOTE]" kwanini unaangalia uwekezaji wa serikali katika mtizamo wa kimaslahi binafsi namna hiyo? Ok tuchukulie kuwa hiyo ni fursa kwao, wananchi wa kawaida itawaidiaje, je multiplier effect ya uwekezaji wa namna hiyo ipoje haswa kwa wananchi wa kawaida unaodhani hiyo ni fursa kwao?

Nikiri tu simfahamu mleta mada wala misimamo yake lakini kupitia nyuzi zake anaonekan ni mtu objective sana. Wakati serikali nanunua bombadia alionehsa kuunga mkona na kutoa hoja za kitaalamu ni kwanini uamuzi ule ulikuwa sahihi. Leo anapoeleza mapungufu ya maamuzi mengine sioni itakidi za kichama bali na ona hoja zenye mashiko.

Mwisho niwaase wadau hasa vijana tuachane na hoja mufilisi na itikadi zisizo na maana. Serikali inapofanya jambo zuri wanaonufaika ni watanzania wakiwemo ndugu na jamaa zako hovyo pongeza na acha ubinafsi. Hali kadhalika ikikosea kosoa kwa staha maana wanaoathirika pia ni ndugu na jamaa zako.
 
mkuu kwa hiyo maeneo mengine yasiyo na kiongozi yatafaidika vipi, kwa mfano maeneo ya kusini lini watajengewa huo uwanja wa ndege?

Hakuna dhambi mbaya kama ubaguzi kamwe.
Mbona uwanja wa Mtwara ni mzuri na umeboreshwa fresh, hapa kinachofanyika ni siasa hizi nyingine ni mbwembwe tu.
 
Uwanja wa chato unajengwa ili mkuu awe anashuka na ndege akienda mapumziko. Hamna sababu nyingine zaidi ya hiyo. Uwanja huu hautasaidia chochote kiuchumi na sidhani kama ndege za kibiashara zitatua uwanja huu.
 

Well said mkuu, siyo kwamba hilo hawalijui - wanacho tafuta ni how to get even na Mzalendo "YOHANA" ni hilo tu mkuu.
 
Wakati KIA inajengwa Boma la Ng'ombe kulikuwa na nini?
 
Rudi kwenye hoja...Matusi ni dalili ya kuupumzisha ubongo kufanya kazi yake.Utendee vema ubongo wako
Kwani mkoa wa geita una uwanja wa ndege? Kujengwa uwanja wa ndege mkoa wa geita imekuwa shida? Mbona hamjasema kuhusu uwanja wa songwe
 
Fortunately huu utakuwa na shughuli za kiuchumi. kuna national parks pale

kama hiyo mbuga ni Serengeti au yenye equal status basi itakuwa sahihi ..,.maana hizi mbuga hata bila serekali TANAPA huwa wakiona hata huwa wanajenga AIRSTRIPS ...
 
Huna lolote kinachokusumbua ni wivu tu unajifichia kwenye uchumi nani amekwambia wa Mwanza hautajengwa??? utakapojengwa wewe mwenyewe utasema wanajenga tu kanda ya ziwa!!! unataka Kiongozi wa nchi aende kwa baiskeli nyumbani kwake???? mbona hatujakusikia ukihoji barabara zilizojengwa tena siku nyingi na miundo mbinu ya umeme hadi huko polini ambako hata watu wanaenda kwa msimu!!!!
 
Chato International Airport ni project ya hovyo hovyo iliyo fanywa kwa kumuogopa Rais Magufuli

Unafiki nao ni approach ya ushindi kama si usalama.

Ningefurahi kama uwanja ungejengwa Geita ili kurahisisha mawasiliano ya kiuchumi katika kanda ile ukizingatia wingi wa heka heka za wafanyabiashara wa madini katiak eneo lile.

Ninaomba iwe kaam ilivyo siku zote isije kesho tukaanza kuulizana mchawi wa raslimali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Just imagine ingekuwa ndo Lowassa Rais (angalizo ni mfano tu sina mapenz naye kiasi hicho)alafu akajenga Monduli international Airport badala ya kuendeleza Arusha Airport ungeyaongea haya? Ingepaswa kuuliza monduli sio Tanzania? Ingepaswa kuulizwa kwani wamasai ni nyani?
Just imagine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…