mtimkav
JF-Expert Member
- Aug 28, 2013
- 1,034
- 662
kwani sudan ndio kunakaa nyani?Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwani sudan ndio kunakaa nyani?Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Kwanza Nikiona post za dizaini hii huwa nakuwa disapoited sana. Hivi mnadhani kila mtu ameshikiliwa akili zake na watu wengine? Kwanini kila nayeeleza mapungufu ya kitu fulani kwenye serikali laziama apewe jina la upinzani? Hivi kwakuwa wewe ni mtu wa kusifia hata pale ambapo mapungufu ni shahiri dhahiri unadhani kila mtu yupo hivyo?Mnaweza kuweka uchambuzi mzuri sana ila ukakosa mashiko kwa kuwa tu una lengo la kiitikadi zaidi.
Mimi huwa najiuliza, je suppose tungechagua huko, kwa bahati mbaya sana umeshindwa kujiendesha wenyewe mkaamua kuturudishia walewale waliokimbia huku baada ya kukatwa je mngeweza kutujengea nchi kweli?, au mngeishia kuandika uchambuzi kama huu wakati mkishuhudia barabara ya Chalinze-Moshi ikiwekwa 4 ways, na kiwanja kama hicho cha chato kikijengwa Hai au Monduli?
Maana wenzetu wa upinzani mmekuwa mabingwa ya kuchambua msivyoviweza, mmekuwa wazuri theoretically but you are not practically oriented, mambo yenu mengi yanakwenda kinyume lakini kwa vile kafanya yule, basi you keep quite kama vile hamuoni huku ukisubiri uongee likifanyika upande wa pili.
Kaskazini ilijengeka mapema kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,
Mbona uwanja wa Mtwara ni mzuri na umeboreshwa fresh, hapa kinachofanyika ni siasa hizi nyingine ni mbwembwe tu.mkuu kwa hiyo maeneo mengine yasiyo na kiongozi yatafaidika vipi, kwa mfano maeneo ya kusini lini watajengewa huo uwanja wa ndege?
Hakuna dhambi mbaya kama ubaguzi kamwe.
Mkuu nadhani tatizo like hapo watanzania wamekuwa walalamishi Kama watoto wadogo. Hawajajisumbua hata kuangalia budget ya Mwaka wa fedha Kama kipaumbele hicho kilikuwepo, pia kuangalia Kama 5years strategic plan ya nchi ilitaja mradi huo.Kulaumu bila data ni makosa. Labda tufanye home work ya kupitia budget ya mwaka wa fedha kwanza halafu tune na majibu
Wakati KIA inajengwa Boma la Ng'ombe kulikuwa na nini?Mimi sikubaliani na wewe kabisa. Inawezekana unatoka Chato na una akili mgando kama ndugu yako. Huwezi kufikiria kujenga uwanja wa ndege wenye kiwango cha 4D Chato labda uwe mwandawazimu. Kwa mtu makini huwezi kuwaza hivyo, after all Chato sio makao makuu ya Mkoa wa Geita ili angalau upate sababu ya kujenga viwanja vya ndege kila mkoa tukianzia na Chato. Chato ni kijiji tu sawa na vijiji vingine. Hivi ndege inaenda kutua Chato kutafuta nini?
Mtu kufanya maamuzi kama hayo lazima awe na akili kama za Paul Kagame wa Rwanda au za Nkurunziza wa Burundi otherwise huwezi, ni aibu na inatia kinyaa.
Kwani mkoa wa geita una uwanja wa ndege? Kujengwa uwanja wa ndege mkoa wa geita imekuwa shida? Mbona hamjasema kuhusu uwanja wa songweRudi kwenye hoja...Matusi ni dalili ya kuupumzisha ubongo kufanya kazi yake.Utendee vema ubongo wako
Wakati KIA inajengwa Boma la Ng'ombe kulikuwa na nini?
Nimeuliza hivi "kwani chato ipo sudan"? Angalia matumizi ya vituo na komakwani sudan ndio kunakaa nyani?
Fortunately huu utakuwa na shughuli za kiuchumi. kuna national parks pale
Ikiwezekana,***
baeleze....hata soko kuu la tz lijengwe chato..😛
kama hiyo mbuga ni Serengeti au yenye equal status basi itakuwa sahihi ..,.maana hizi mbuga hata bila serekali TANAPA huwa wakiona hata huwa wanajenga AIRSTRIPS ...
Vipi kama meli ikinunuliwa na kupelekwa Iringa?
Kama hivyo ndivyo ulivojibu hoja hiyo, naona umeishiwa hoja na asubuhi njema.kwa akili yako unaona uwanja wa ndege ni kitu cha ajabu sana!
Huna lolote kinachokusumbua ni wivu tu unajifichia kwenye uchumi nani amekwambia wa Mwanza hautajengwa??? utakapojengwa wewe mwenyewe utasema wanajenga tu kanda ya ziwa!!! unataka Kiongozi wa nchi aende kwa baiskeli nyumbani kwake???? mbona hatujakusikia ukihoji barabara zilizojengwa tena siku nyingi na miundo mbinu ya umeme hadi huko polini ambako hata watu wanaenda kwa msimu!!!!Sasa ni dhahiri kuwa, kuanzia mwezi Aprili katika mapumziko ya Pasaka, Mkuu wetu atakuwa na uhakika wa kwenda mapumzikoni kwa kutumia uwanja wa ndege mpya wa Chato, yaani Chato Airport.
Kwa sasa uwanja huo unaotegemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili upo ktk kiwango cha vumbi na unaendelea kufanyiwa matengenezo hadi kiwango cha lami. Tayari ndege ndogo aina ya Beech Craft(King Air) mali ya kampuni binafsi ya TanzanAir imetua kwa mara ya kwanza ktk uwanja wa ndege wa Chato na hivyo kutoa uhakika kuwa sasa Chato inaenda kupokea ndege bila wasiwasi wowote.
Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.
Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".
Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".
Hatuididimizi dhamira ya Mkuu kujenga kiwanja chenye ubora Chato, bali tunahoji kwa uelewa mdogo tu wa kanuni za Uchumi. Kwamba kiwanja hiki huko Chato kinaweza kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi kama ambavyo wangeweza kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza?
Tunauhitaji Uwanja wa Mwanza kuliko ule wa Chato kwa sababu za kiuchumi ktk sekta ya Utalii. Tumekuwa tukilalamika sana kwa mbuga yetu ya Serengeti kukosa watalii wa kutosha kisa njia za usafiri kufika huko zilivyokuwa duni kushinda majirani zetu tunaopakana na mbuga ya Maasai Mara.
Uwanja pekee unaohudumia mbuga ya Serengeti kwa njia ya anga ni "Seronera Aistrip" ambapo huwa busy sana na huchukua ndege ndogo zenye abiria wasiozidi 50. Hii ndio moja kati ya "busiest Airstrip" kwa Tanzania.
Ili ufike Serengeti kupitia uwanja wa KIA unahitaji kutembea kilomita 284 kwa gari toka uwanjani, kwa kupitia uwanja wa ndege wa Arusha inakupasa utembee kwa gari umbali wa kama kilomita 226 wakati kwa kupitia Uwanja wa Mwanza,mtalii anatembea kilomita 166 hadi kufika geti la Ndabaka(?).
Kwa mahesabu hayo,kama ujenzi wa Uwanja wa ndege Serengeti ulishindikana,basi Uwanja wa ndege wa Mwanza ndio suluhisho la haraka ktk kuwafikisha watalii kwa urahisi ktk mbuga hiyo.Tukiusahau uwanja huo na kutazama zaidi ule wa Chato, tunaweza kuhoji dhamira hii ya maendeleo ktk kufika uchumi wa kati. Na kuhoji kwetu kusiababishe "hasira" kwa wenye mamlaka, bali ichukuliwe ni kama changamoto za raia kwa serikali yao.
Ukisefu wa usafiri wa uhakika na hasa ule wa njia ya anga, ndio unatukosesha mapato na kupunguza idadi wa Watalii ktk mbuga yetu ya Serengeti na hivyo wengi kuishia Maasai Mara.
Licha ya kuwa Serengeti ina ukubwa mara sita ya Maasai Mara,lakini bado "Vitanda" vya kupokea watalii katika hotel za Serengeti hivizidi 970 wakati wenzetu Maasai Mara ktk mbuga yao, kuna "Vitanda" zaidi ya 4,700. Hakika kupanga ni kuchagua.
Mpaka sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania inamiliki viwanja vya ndege 58(ukijumlisha na Chato itakuwa 59),na wakati Uwanja wa ndege wa KIA ukiwa mikononi mwa Kampuni ya KADCO. TANAPA inamiliki karibu viwanja 26(Vingi vikiwa ni Airstrips),NCAA 2 na viwanja binafsi 93.
Katika hivi vya binafsi,vingi vinamilikiwa na wawekezaji toka nje ambao huvitumia kufanya udanganyifu ktk maliasili zetu.Uwanja wa ndege wa mgodi wa Geita(Mchauru) na Uwanja wa ndege wa Tishwa(HTSW) kule Loliondo unaomilikiwa na mtoto wa mfalme wa UAE ni moja kati ya viwanja vinavyopswa kutazamwa vizuri na serikali hii.
Uwanja huu wa Tishwa Loliondo ndio "unatisha", kwani huku ndege za familia ya mfalme hushuka moja kwa moja na kunyanyuka na mali nyingi. Umejengwa kiasi cha kuweza kutua na kuruka ndege kubwa.
Huu ndio uwanja ulio ktk eneo ambapo ukifika na kuwasha simu unakutana na meseji inasema "Dear Guest,Welcome to the UAE.Enjoy the best network coverage and other unmatched services only with Etisalat.Please use <+> or <00> before the country code for international calls.For directory services call 181,for availability of GPRS,MMS 3G roaming services call Etisalat Travellers help line 8002300 & for inquiries on Tourism,entertainment,shopping,etc call 7000-1-7000(Roaming rates apply).Have a pleasant stay in the UAE"
Labda wengine hatuna utaalamu wa Telecomunication, lkn kweli inawezakana hii kitu iingie tu kwenye simu yako wakati hujafanya "roaming". Haya ndio mambo ya TCRA kututoa tongotongo, sio zile mambo zao za .co.tz
Tunatakiwa tuwekeze ktk usafiri wa anga,lakini tuwekeza kimkakati na kwa faida za uchumi wa pamoja kama Taifa.Tukipewa sababu za kiuchumi zinazoupeleka uwanja wa ndege Chato wenye "Aerodrome Reference Code 4D" hatutakuwa na maswali.Tusipapata majibu yenye faida za kiuchumi,tutaendelea kuhoji hata tukiwa mafichoni.
Tukumbusha umuhimu wa Mwanza ktk kuihudumia Serengeti National Park, tutawakumbusha kuwa mlikuwa na mradi wa kujenge Uwanja wa ndege Serengeti,ila mkapambana na wanaharakati wa Ikolojia. Uwanja wa Serengeti ulipaswa kujengwa kati wa Kiwanja cha Ndege pale Mgumu.
Serengeti International Airport ilikuwa ni Code 4F, ilipaswa kuwa na runway ya mita 3,800 hadi mita 4,200.Mradi huo ulififia,sasa "tumefufukia" Chato na Uwanja wa "Code 4D".Je huku ndio kupanga na kuchagua??
Wakuu ukiyatafakari sana mambo ya nchi hii unaweza kuwa kichaa. Tuishukuru [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG], inatupa wasaa wa kuhoji haya nyuma ya "keyboard". Mambo haya enzi za Waziri wa Maliasili Aboubakari Mgumia yaliondoa maisha ya Ndugu Stan Katabaro. Tunapouanza mwaka mpya, tuzame katika sala na maombi. Ili wale wanaoomba tuwaombee kila siku,tusiwaombee tu wawe na afya njema..Bali walegeze mioyo ktk kuishughulikia mitandao kama mtandao wetu pendwa wa [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG].
Nawatakia Mwaka Mpya mwema. Ninafunga mwaka na "Chato Interantional Airport".... Panapo majaliwa hapo mwakani. Nitakuwa likizo huko kwetu porini.... Ciaoooo!!!!
Chato International Airport ni project ya hovyo hovyo iliyo fanywa kwa kumuogopa Rais Magufuli
Hoja mufilisi na baguzi isiyo na mashiko.Hawa watu wa kasikazini ni shidaaa aisee wanataka maendeleo ya kwao tu
Just imagine ingekuwa ndo Lowassa Rais (angalizo ni mfano tu sina mapenz naye kiasi hicho)alafu akajenga Monduli international Airport badala ya kuendeleza Arusha Airport ungeyaongea haya? Ingepaswa kuuliza monduli sio Tanzania? Ingepaswa kuulizwa kwani wamasai ni nyani?Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?