Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Mkuu Yaani wanataka eti wafanye miujiza wahindi matajiri wote watalazimishwa kujenga hotel Chato, na Nation housing, Veta walalazimishwa wajenge nyumba na Hotel pia NSSF na mashirika mengineyo watalazimishwa kuijenga Chato.

Yaani Chato itajengwa kwa lazima kwa Amri amri bila kupenda.
Mwache wivu wa kijinga. Yeah miji ya kwenu ikijengwa mnaona sawa ya wenzenu mnapata nongwa!!!
 
Mkuu barafu shikamoooo
Ninapenda uandikaji wako...hutukani mtu wala kukashifu,lkn kwa namna ulivyojibiidisha kuzisifia Pangaboi na kuwa kama msemaji wa ATCL/Serikali humu JF,ukosoaji wako unapata uhalali...japo kuna makada wanakutupia matusi na kusahau kuwa uliwabeba sana humu enzi za mijadala ya pangaboi

Heri ya mwaka mpya mkuu,ila urudi tena humu,bado tunahitaji michango yako mkuu
 
Tusianze kulaumu tu bila ya kuwa na facts za kutu-back up, cha kujiuliza kwanza ,je, Serikali au tuseme uwamu iliyopita waliwahi kuwa na mpango wa kujenga kiwanja cha ndege CHATO? pili ,je, uwanja huo umejengwa strategically kwa masuala ya ulinzi wa nchi - haya ndiyo maswali ya kujihoji kwanza kabla ya kuanza kumlaumu JPJM bila sababu za msingi.
 
Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Watawala walichowaweza watanzania ni kuwaharibia elimu...ni wewe ni moja ya matunda ya elimu yetu mbovu
 
Nimeona picha za Rais akiwa ameenda kuwafariji jirani zake, kwenye Gazeti la leo 30.12.2016 Mwananchi.

Ni aibu sana, jirani zake wanaishi kwenye nyumba duni sana, za tope

Sijui Rais anajisikiaje kujenge kiwanja cha ndege kwa Nyumba kama hizo za jirani zake.

Lakini pia yale matamko yake anajisikiaje akiwa na jirani zake wa hali hiyo?

Time will tell
Hacha uchochezi wewe ushawajengea majirani zako nyumba??
 
Mkuu barafu, iwapo serikali ingechukua hata nukta ya ushauri wako basi isingejuta kufanya hyo.

Mwanza is a Central of East African country! Kutoka Mwanza kufika Serengeti ni masaa yasiyozidi 2, hvyo kuwa na International airport mwanza hakika uchumi wa mwanza na nchi ungepaa Sana...maana wageni wengi wangetua na kwenda Masai zaidi kuliko hivi sasa sisi ndio vinara wa kwenda kupokea kwenye border ya isbania!!!
Mwanza sio center ya eac states bhana...that should be kagera....which boarders all said states..labda kama kigezo chako ni kuwa kalibu na serengeti
 
Mnaweza kuweka uchambuzi mzuri sana ila ukakosa mashiko kwa kuwa tu una lengo la kiitikadi zaidi.

Mimi huwa najiuliza, je suppose tungechagua huko, kwa bahati mbaya sana umeshindwa kujiendesha wenyewe mkaamua kuturudishia walewale waliokimbia huku baada ya kukatwa je mngeweza kutujengea nchi kweli?, au mngeishia kuandika uchambuzi kama huu wakati mkishuhudia barabara ya Chalinze-Moshi ikiwekwa 4 ways, na kiwanja kama hicho cha chato kikijengwa Hai au Monduli?

Maana wenzetu wa upinzani mmekuwa mabingwa ya kuchambua msivyoviweza, mmekuwa wazuri theoretically but you are not practically oriented, mambo yenu mengi yanakwenda kinyume lakini kwa vile kafanya yule, basi you keep quite kama vile hamuoni huku ukisubiri uongee likifanyika upande wa pili.

Kaskazini ilijengeka mapema kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,
mkuu haujafikiri kwa usahihi.
 
Tusianze kulaumu tu bila ya kuwa na facts za kutu-back up, cha kujiuliza kwanza ,je, Serikali au tuseme uwamu iliyopita waliwahi kuwa na mpango wa kujenga kiwanja cha ndege CHATO? pili ,je, uwanja huo umejengwa strategically kwa masuala ya ulinzi wa nchi - haya ndiyo maswali ya kujihoji kwanza kabla ya kuanza kumlaumu JPJM bila sababu za msingi.

Mkuu nadhani tatizo like hapo watanzania wamekuwa walalamishi Kama watoto wadogo. Hawajajisumbua hata kuangalia budget ya Mwaka wa fedha Kama kipaumbele hicho kilikuwepo, pia kuangalia Kama 5years strategic plan ya nchi ilitaja mradi huo.Kulaumu bila data ni makosa. Labda tufanye home work ya kupitia budget ya mwaka wa fedha kwanza halafu tune na majibu
 
Hacha uchochezi wewe ushawajengea majirani zako nyumba??
Mkuu,
Rais ana jukumu la kuhakikisha si majirani zake tu bali taifa zima linapata makazi bora, ni jukumu lake kutoa umasikini, Maradhi na Ujinga TANZANIA.

Sasa kwa Kujenga huo uwanja hivyo vitu vitatu Umasikini, Maradhi na Ujinga vitapungua hapo Chato.

Lakini pia angewauliza hao majirani zake sina hakika kama watasema awajengee uwanja wa ndege.
 
Watawala wetu karibu wote ni wabinafsi na wakabila,Kiongozi ambaye hakupendelea kwao alikuwa mmoja tu JKN wengine wote waliobaki walipendelea kwao na kupeleka miradi mikubwa huko.

Tumeona Bandari ikitolewa mitaa ya Posta ikapelekwa Bwagamoyo,leo tunaacha kuutengeneza Uwanja wa Mwanza ambao ni VALUE FOR MONEY ,tunaenda kutengeneza Chato sababu ni kwetu.

Tusiwasingizie watendaji,mtendaji hawezi akafanya uamuzi mkubwa hivyo,na kwa Kiongozi mwenye nia njema na uchumi wa Taifa lake angelipigia kelele sana,kwamba usiwekwe huko.

Na ameanza mapema sababu anajua akichelewa yatamfika ya JK ambapo Bandari iliishia kwenye upembuzi yakinifu.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Chato kuna barabara nzuri mpaka taa za kuongozea magari ambazo moshi hazipo!!!hahaha
 
nina umri wa miaka 73, nimetokea kwenye familia yenye watoto wengi sana , ila cha kuskitisha katika familia yetu ama ukoo wetu kwa ujumla hakuna hata 1 aliyewah kupanda ndege
Shauri yenu mlimwacha elimu akaenda zake. Wacha wajenge ssie tutapanda kuja chato. Hatutaki ujinga
 
Mkuu nadhani tatizo like hapo watanzania wamekuwa walalamishi Kama watoto wadogo. Hawajajisumbua hata kuangalia budget ya Mwaka wa fedha Kama kipaumbele hicho kilikuwepo, pia kuangalia Kama 5years strategic plan ya nchi ilitaja mradi huo.Kulaumu bila data ni makosa. Labda tufanye home work ya kupitia budget ya mwaka wa fedha kwanza halafu tune na majibu

Mkuu,
Si budget tu na Mpango wa miaka Mitano Bali hata kwenye kitabu cha llani ya CCM 2015 to 2020 Hakuna kitu kama hicho Kujenga uwanja wa Ndege Chato.

Kuna viwanja vimetamkwa kwenye ilani wanavitambua
 
Back
Top Bottom