Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Mkuu yule saint akiamua kaamua..anakwenda sana off budget

Ova
Ikafanye nini kule?

Tatizo la mitanzania ni zile fikra za kimaskini na choyo, mtu yuko radhi apiganie uwanja wa ndege usio na faida yoyote ili mradi tu uko kwao. Viwanja kama Kia, JNIA, Arusha, Mbeya na Mwanza hivi vimeendelea na kuwa vitega uchumi.

Ticket yangu ya ndege kutua Songwe inaonyesha kodi shilingi 13,000- ninaposafiri. Abiria 1,000 wakishukia uwanja mmoja kwa siku shilingi milioni 13 zinaingia na kusaidia kulipa bili, wafanyakazi na gharama zingine za uendeshaji na faida kidogo.

Pia angalia maduka na biashara pale uwanjani. Faida plus plus. Je Chato pale uwanja huo utaingiza hata senti. Nishuke kwenye ndege nikalale Marine Lodge? Jamani jamani jamani Mungu anawaona.

Tunaolalamika hoja yetu ni kuwa kwa sasa nchi yetu bajeti haitoshi tungekuwa na vipaumbele kwa viwanja vyenye uwezekano wa kutatua matatizo ya sasa na kuleta kakipato kidogo, Chato sio kipaumbele.
 
Chato kwenyewe baiskeli ni nyingi kuliko gari still kuna traffic light.... Sasa unajenga uwanja wakati hakuna umuhimu wowote nani atakwenda bush kule kufanya nn labda, JK katuachia matatizo makubwa sn aise
 
Sasa ni dhahiri kuwa, kuanzia mwezi Aprili katika mapumziko ya Pasaka, Mkuu wetu atakuwa na uhakika wa kwenda mapumzikoni kwa kutumia uwanja wa ndege mpya wa Chato, yaani Chato Airport.

Kwa sasa uwanja huo unaotegemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili upo ktk kiwango cha vumbi na unaendelea kufanyiwa matengenezo hadi kiwango cha lami. Tayari ndege ndogo aina ya Beech Craft(King Air) mali ya kampuni binafsi ya TanzanAir imetua kwa mara ya kwanza ktk uwanja wa ndege wa Chato na hivyo kutoa uhakika kuwa sasa Chato inaenda kupokea ndege bila wasiwasi wowote.

Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.

Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".

Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".

Hatuididimizi dhamira ya Mkuu kujenga kiwanja chenye ubora Chato, bali tunahoji kwa uelewa mdogo tu wa kanuni za Uchumi. Kwamba kiwanja hiki huko Chato kinaweza kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi kama ambavyo wangeweza kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza?

Tunauhitaji Uwanja wa Mwanza kuliko ule wa Chato kwa sababu za kiuchumi ktk sekta ya Utalii. Tumekuwa tukilalamika sana kwa mbuga yetu ya Serengeti kukosa watalii wa kutosha kisa njia za usafiri kufika huko zilivyokuwa duni kushinda majirani zetu tunaopakana na mbuga ya Maasai Mara.

Uwanja pekee unaohudumia mbuga ya Serengeti kwa njia ya anga ni "Seronera Aistrip" ambapo huwa busy sana na huchukua ndege ndogo zenye abiria wasiozidi 50. Hii ndio moja kati ya "busiest Airstrip" kwa Tanzania.

Ili ufike Serengeti kupitia uwanja wa KIA unahitaji kutembea kilomita 284 kwa gari toka uwanjani, kwa kupitia uwanja wa ndege wa Arusha inakupasa utembee kwa gari umbali wa kama kilomita 226 wakati kwa kupitia Uwanja wa Mwanza,mtalii anatembea kilomita 166 hadi kufika geti la Ndabaka(?).

Kwa mahesabu hayo,kama ujenzi wa Uwanja wa ndege Serengeti ulishindikana,basi Uwanja wa ndege wa Mwanza ndio suluhisho la haraka ktk kuwafikisha watalii kwa urahisi ktk mbuga hiyo.Tukiusahau uwanja huo na kutazama zaidi ule wa Chato, tunaweza kuhoji dhamira hii ya maendeleo ktk kufika uchumi wa kati. Na kuhoji kwetu kusiababishe "hasira" kwa wenye mamlaka, bali ichukuliwe ni kama changamoto za raia kwa serikali yao.

Ukisefu wa usafiri wa uhakika na hasa ule wa njia ya anga, ndio unatukosesha mapato na kupunguza idadi wa Watalii ktk mbuga yetu ya Serengeti na hivyo wengi kuishia Maasai Mara.

Licha ya kuwa Serengeti ina ukubwa mara sita ya Maasai Mara,lakini bado "Vitanda" vya kupokea watalii katika hotel za Serengeti hivizidi 970 wakati wenzetu Maasai Mara ktk mbuga yao, kuna "Vitanda" zaidi ya 4,700. Hakika kupanga ni kuchagua.

Mpaka sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania inamiliki viwanja vya ndege 58(ukijumlisha na Chato itakuwa 59),na wakati Uwanja wa ndege wa KIA ukiwa mikononi mwa Kampuni ya KADCO. TANAPA inamiliki karibu viwanja 26(Vingi vikiwa ni Airstrips),NCAA 2 na viwanja binafsi 93.

Katika hivi vya binafsi,vingi vinamilikiwa na wawekezaji toka nje ambao huvitumia kufanya udanganyifu ktk maliasili zetu.Uwanja wa ndege wa mgodi wa Geita(Mchauru) na Uwanja wa ndege wa Tishwa(HTSW) kule Loliondo unaomilikiwa na mtoto wa mfalme wa UAE ni moja kati ya viwanja vinavyopswa kutazamwa vizuri na serikali hii.

Uwanja huu wa Tishwa Loliondo ndio "unatisha", kwani huku ndege za familia ya mfalme hushuka moja kwa moja na kunyanyuka na mali nyingi. Umejengwa kiasi cha kuweza kutua na kuruka ndege kubwa.

Huu ndio uwanja ulio ktk eneo ambapo ukifika na kuwasha simu unakutana na meseji inasema "Dear Guest,Welcome to the UAE.Enjoy the best network coverage and other unmatched services only with Etisalat.Please use <+> or <00> before the country code for international calls.For directory services call 181,for availability of GPRS,MMS 3G roaming services call Etisalat Travellers help line 8002300 & for inquiries on Tourism,entertainment,shopping,etc call 7000-1-7000(Roaming rates apply).Have a pleasant stay in the UAE"

Labda wengine hatuna utaalamu wa Telecomunication, lkn kweli inawezakana hii kitu iingie tu kwenye simu yako wakati hujafanya "roaming". Haya ndio mambo ya TCRA kututoa tongotongo, sio zile mambo zao za .co.tz

Tunatakiwa tuwekeze ktk usafiri wa anga,lakini tuwekeza kimkakati na kwa faida za uchumi wa pamoja kama Taifa.Tukipewa sababu za kiuchumi zinazoupeleka uwanja wa ndege Chato wenye "Aerodrome Reference Code 4D" hatutakuwa na maswali.Tusipapata majibu yenye faida za kiuchumi,tutaendelea kuhoji hata tukiwa mafichoni.

Tukumbusha umuhimu wa Mwanza ktk kuihudumia Serengeti National Park, tutawakumbusha kuwa mlikuwa na mradi wa kujenge Uwanja wa ndege Serengeti,ila mkapambana na wanaharakati wa Ikolojia. Uwanja wa Serengeti ulipaswa kujengwa kati wa Kiwanja cha Ndege pale Mgumu.

Serengeti International Airport ilikuwa ni Code 4F, ilipaswa kuwa na runway ya mita 3,800 hadi mita 4,200.Mradi huo ulififia,sasa "tumefufukia" Chato na Uwanja wa "Code 4D".Je huku ndio kupanga na kuchagua??

Wakuu ukiyatafakari sana mambo ya nchi hii unaweza kuwa kichaa. Tuishukuru [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG], inatupa wasaa wa kuhoji haya nyuma ya "keyboard". Mambo haya enzi za Waziri wa Maliasili Aboubakari Mgumia yaliondoa maisha ya Ndugu Stan Katabaro. Tunapouanza mwaka mpya, tuzame katika sala na maombi. Ili wale wanaoomba tuwaombee kila siku,tusiwaombee tu wawe na afya njema..Bali walegeze mioyo ktk kuishughulikia mitandao kama mtandao wetu pendwa wa [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG].

Nawatakia Mwaka Mpya mwema. Ninafunga mwaka na "Chato Interantional Airport".... Panapo majaliwa hapo mwakani. Nitakuwa likizo huko kwetu porini.... Ciaoooo!!!!
Mbona kuna a national park pale? Ukiwa chato unaweza fika Rubondo Island, with very beautiful scenery
 
Kuna national park kubwa sana pale. Rubondo Island
Chato kwenyewe baiskeli ni nyingi kuliko gari still kuna traffic light.... Sasa unajenga uwanja wakati hakuna umuhimu wowote nani atakwenda bush kule kufanya nn labda, JK katuachia matatizo makubwa sn aise
 
Mkuu barafu you are speaking in tongues(aviation jargon) ila nimekuelewa as far as economics is concerned, siku hizi sisikii bwana yule akiomba aombewe, kashaonja vitamu...

Give them an inch they take a yard, give them a yard they take a mile... Tukiongea sana watamrudisha mkuu Melo Keko!!
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gbadolite airport Leo hii umebaki magofu matupu kwakuwa haukujengwa kiuchumi ...bali Kiongozi aliamua tu kuujenga kijijini kwake .....na baada ya kuondolewa umebakia magofu ....kwa kuwa hakuna shughuli ya kiuchumi ya kufanya huo uwanja uendelee
 

Attachments

  • Gbadolite airport DURING MOBUTO.jpg
    Gbadolite airport DURING MOBUTO.jpg
    7.7 KB · Views: 68
  • Gbadolite airport AFTER MOBUTO.jpg
    Gbadolite airport AFTER MOBUTO.jpg
    21.4 KB · Views: 126
Yaani ukisoma mada za humu JF haki ya nani unaweza kupandwa hasira mpaka basi! Itoshe tu kusema sisi ma-Tanzania ni mapumbavvv inawezekana vipi majitu yanatetea ujenzi wa uwanja wa Chato ambao no dhahiri shadri kwamba ni matumizi mabaya ya raslimali fedha? Mkuu Barafu kafafanua vizuri kwamba uwanja wa Chato hautakuwa na manufaa yoyote kiuchumi, labda kama uchumi wenyewe ni kumrahisishia Rais kutua na Ndege yake Mara 4 kwa mwaka! Itoshe tu kusema hapa Rais kaonesha ubinafsi wa hali ya juu, hivi baada ya kipindi chake Ndege gani itaenda Chato jamani? Ni mwananchi gani wa kawaida atapanda Ndege huko Chato? Yale yale ya Gbadolite! Nihitimishe kwa kusema sisi ma-Tanzania ni mang'ombe!
 
Mkuu Barafu baada ya kuleta ile habari ya kwanza ya Uwanja wa NDEGE WA CHATO niliona nifuatilie sababu za Ujenzi wa huo Uwanja na umuhimu wake...

Findings....

Nimeelezwa kuwa, Rais Magufuli amejenga Uwanja huo CHATO ili aweze kuziteka nchi za RWANDA, BURUNDI, na UGANDA, Kwamba, Ndege za kutoka mataifa hayo zitatua CHATO INT. AIRPORT, halafu abiria watapanda Gari zao kutoka CHATO hadi MWANZA ambapo watapanda tena NDEGE kwenda wanapopataka ndani au nje ya nchi, (SIJUI NI AKILI GANI ILIYOTUMIKA HAPA) nimeelezwa kwamba, Rais Magufuli anataka kujenga DARAJA La BUSISI ili kurahisisha usafiri huo wa wageni kuja Mwanza kutoka CHATO INT. AIR.

Nimeelezwa kuwa, Mpango wa Magufuli ni Kuutenganisha mkoa wa GEITA Na CHATO hapo baadae, hivyo anaandaa mazingira ya kushawishi ugawaji wa MIKOA Hiyo, na makao makuu ya mkoa wa CHATO yatakuwa eneo moja linaitwa RUSUNGU hivi kama sijakosea jina, nakubali nirekebishwe maana nimesahau jina lake kwa usahihi.

Nimeelezwa kwamba, Eti CHATO kuna Mbuga ya WANYAMA binafsi ya RAIS Magufuli ila sijawa na uhakika na hili...

Kwa kifupi, hata kama Chato walikuwa na uhitaji wa uwanja wa ndege siyo sasahivi jamani, wewe fikiria, Plan zipo kwenye vitabu miaka mingi juu ya ujenzi wa viwanja kama MWANZA, MUSOMA Nk. lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika kwenye viwanja hivyo, ila hiki cha chato ndo kiwe Urgent?
 
Mwanza sio center ya eac states bhana...that should be kagera....which boarders all said states..labda kama kigezo chako ni kuwa kalibu na serengeti
Yaani centre ya EAC uipeleke Kagera (sijui ulitaka kumaanisha Bukoba) utakuwa na akili wewe?
 
Kipigi,

Naungana na wewe.

Pist yake kwangu imekosa mantiki pale aliposema uwanja wa chato usijengwe ili kuboresha wa mwanza wakati anatambua kwamba

1. Maboresho ya uwanja wa mwanza yanaendelea hadi sasa na ujenzi wa uwanja wa chato hauja athiri maboresho ya uwanja wa mwanza.

2. Kuna uhitaji wa kujenga uwanja wa ndege kuhudumia mbuga ya serengeti. Badala ya kupiga debe uwanja huo ujengwe ndani au karibu na mbuga hiyo anashadadia uwanja wa mwanza ndio uhudumie serengeti ilhali upo miles away.

Ni seme tu kwamba badala ya kulalamikia uwanja kujengwa chato. Tusifie na kudai ujenzi na uboreshaji wa viwanja vingine vingi tu vinavyohitajika kote nchini kulingana mahitaji ya sasa na ya baadae.

Lengo isiwe kukataa maendeleo yasiwepo eneo flani bali yapelekwe kwa wakati kulingana na mahitaji na faida zitakazopatijana.
Kwahiyo rasilimali fedha sio tatizo hivyo tujenge tu viwanja vya ndege kila mahali au unamaanisha nini?
 
Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
watu wa hovyo sana, uwanja wa ndege ni jambo la kawaida sana, hata watu binafsi wanavyo, Kasoli Genery kule bariadi wana uwanja wao wa ndege, geita mgodini wanao sasa kuna tatizo gani chato kuwa na uwanja wa ndege? hata mie nimeshanza kujenga uwanja wa kwangu japo sio wa ndege ni wa kuchezea mpira.
 
Mnaweza kuweka uchambuzi mzuri sana ila ukakosa mashiko kwa kuwa tu una lengo la kiitikadi zaidi.

Mimi huwa najiuliza, je suppose tungechagua huko, kwa bahati mbaya sana umeshindwa kujiendesha wenyewe mkaamua kuturudishia walewale waliokimbia huku baada ya kukatwa je mngeweza kutujengea nchi kweli?, au mngeishia kuandika uchambuzi kama huu wakati mkishuhudia barabara ya Chalinze-Moshi ikiwekwa 4 ways, na kiwanja kama hicho cha chato kikijengwa Hai au Monduli?

Maana wenzetu wa upinzani mmekuwa mabingwa ya kuchambua msivyoviweza, mmekuwa wazuri theoretically but you are not practically oriented, mambo yenu mengi yanakwenda kinyume lakini kwa vile kafanya yule, basi you keep quite kama vile hamuoni huku ukisubiri uongee likifanyika upande wa pili.

Kaskazini ilijengeka mapema kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,
Kwa nini kila kitu mnapenda kuitumia kaskazini ili muweze kuhalalisha madudu yanayofanyika !!!!!.........

Mimi si mtu wa kaskazini lakini je, ni hekima nchi kuiendesha kiswahili Kama unavyojiaminisha na ni aibu kubwa pia kuona tunataka kuiendesha nchi Kama ndoa za mitala yaani kila mtu analalama kuhusu zamu yake ( no wonder we are still poor)

Brother Kama hujui ni kuwa usafiri wa anga ni mgumu ndio maana mashirika mengi yanaendeshwa kwa hasara hivyo, Kama nchi tunatakiwa kuwa makini na kila uwekezaji tutakaoufanya maana chato haina potential kwa route za ndani na nje

Uwanja ungejengwa popote lakini kwa. Hoja zenye mashiko kwa mfano uwanja wa iringa ama dodoma ungejengwa vyema kwa ajili ya kurahisisha connectivity ndani ya nchi na kufungua kanda ya utalii ya kusini bado ingeleta mantiki lakini kuna hoja gani chato !!!!!.......

Brother badili mtazamo wako ili nchi yetu iendelee , aviation industry kwa tz bado ni changa kwa kutegemea route za ndani hivyo za nje ndio kimbilio ambapo huko ndipo kuna ushindani hivyo maamuzi yoyote ya kipuuzi yatatugharimu
 
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gbadolite airport Leo hii umebaki magofu matupu kwakuwa haukujengwa kiuchumi ...bali Kiongozi aliamua tu kuujenga kijijini kwake .....na baada ya kuondolewa umebakia magofu ....kwa kuwa hakuna shughuli ya kiuchumi ya kufanya huo uwanja uendelee
Fortunately huu utakuwa na shughuli za kiuchumi. kuna national parks pale
 
Back
Top Bottom