Wakati nchi za wenzetu dira zao zinaamini katika Science,Research and development katika ku-propel and ku-prosper za kwetu bado zinaamini katika mawazo ya viongozi ili ku-propel.
Na wakati mwingine mawazo yao huwa ya kijinga kwa maana viongozi wetu wengi hupenda kusifiwa hata kwa ujinga ili kuonesha hakuna wengine bora zaidi ya wao
Pengine hufanya hivi wapate kibali cha kuendelea kutawala kwa faida zao binafsi.
Kama Marekani ingekuwa Tanzania kwa mfano leo Trump angekuwa Rais Marekani.
Lakini pia kwa yale ya kijinga ya Trump hawakusita kumkemea na kurekebisha.
Hii ndio misingi ya nchi inayoamini katika Facts na sio pompousity ya mtu.
Moja kati ya mambo muhimu yaliyomuharibia Trump credit ni pamoja na jinsi alivyoshughulikia mlipuko wa korona mwanzoni mwa mlipuko.
Jambo ambalo pia ndio msingi wa tatizo lile lile hapa kwetu lakini outcome kwa watu walio-base kwenye science and Facts ni tofauti na sisi tulio-base kwenye busara za viongozi hata kama busara ni primitive, unstandard and uncivillized.
Leo, wataalamu wetu wa afya kwa mfano, wanashindwa kufanya kazi zao kwa sababu kazi zao zinapingana na fikra za kiongozi mmoja asiyeamini katika nisingi ya tiba based on science.
Kesho idara za fedha zinaweza kuingiliwa pia na mtu sababu ni kiongozi na mawazo yake hayapingwi na si mtaalamu wa fedha
Kesho, idara ya kilimo, utafiti n.k vitaingiliwa. Sasa badala vyombo vyetu vimpe ushauri wa kitaalamu, kiongozi ndiye kawa mshauri wa vyombo vyetu.
Mungu wabariki watanzania, akili zao mgando zizidi kufunguka.
Mungu wabariki Waafrica waondokane na ujinga.
Ahsanteni kwa mjadala huu!