Hatimaye Eng. Hersi ameamua kuivua Yanga ubingwa wa ligi kuu

Hatimaye Eng. Hersi ameamua kuivua Yanga ubingwa wa ligi kuu

Yanga wana shida nyingi ila mwanasheria wao anawarudisha nyuma sana mtu anavunja mkataba kama anavunja kikombe aisee yule jamaa atakuwa ni ndugu na engineer hersi ngoja niishie hapo kwanza.
Katika mambo ya sheria za mikataba uongozi wa Yanga umedhihirisha kuwa ni weupe sana vichwani. Hapa Eng. Hersi kafeli pakubwa sana.
 
Ramovic ilikuwa lazima aondoke, kipimo cha kocha Yanga ni CAF champions league
Na Gamondi? Hii Yanga CAF mmeanza kushiriki lini kwani mpaka iitumie kama kigezo cha kufukuza makocha?
 
Imekwisha Yanga
Mpira una njia na taratibu zake, hakuna maajabu yanayoweza kutokea tena baada ya uongozi wa Yanga kurudia kosa kwa mara ya pili mfululizo. Timu ilifanyiwa mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kuja Ramovic, timu ili struggle kwa mechi kadhaa ila ikaja kutulia baadae, bahati nzuri mechi za klabu bingwa ndizo zilizotangulia kuliko ligi kuu hivyo ligi kuu ilichezwa wakati Yanga ikiwa imeanza kurejea kwenye kiwango chake.

Timu ilishakaa sawa na tuliona Yanga ikiwa inapata ushindi mnono wa magoli 3+ mnakuja kuleta kocha mpya nae aanze na upya kabisa kuweka falsafa zake huku timu ikikabiliwa na mechi back to back za ligi kuu.

Kuna shida kubwa sana katika mambo ya kimkataba kwa huu uongozi wa Yanga, kocha anaondoka kirahisi tu kisa kapata timu nyingine yenye maslahi zaidi yaani ni ovyo sana katika mambo ya sheria za kimkataba na ndio maana kesi zote uongozi unashindwa hovyo hovyo.

Kwa hapa Simba apewe tu kombe la NBC Hersi hayuko serious kabisa na njia za mpira kwa msimu huu.
 
Kosa alifanya alinunua wachezaji wabovu dube , baleke , akaaingia mkataba mbovu na aziz ki alieshuka kiwango wakati kuna wachezaji wazuri Kwenye timu hawafiki Hata Robo ya malipo ya aziz ki morali ikashuka .
Jumba bovu akaangushiwa Mzee wa watu gamondi kilichobaki ni kutapatapa hakuna ela ya kuleta ya kuleta kocha wa maana ni kuokoteza yoyote bila ya vetting Kama awali .
Ubabaishaji katika ubora wake.
 
Bado mechi 12 uje uongee ayo mwisho wa msimu sio sasa,,aluta continua mapambano yanaendelea
Unasubiri miujiza, ujenge nyumba kisha ubomoe kila mara halafu uje ushindane na aliyejenga pasipo kubomoa tena kazi yake ni kuziba viraka sehemu zenye mapungufu tu. Hapo uongozi umebeti pakubwa sana na ubingwa hauwezi kupatikana tena. Ligi imeisha hiyo
 
Back
Top Bottom