Hatimaye Fadlu Davids atangazwa kuwa Kocha wa Simba SC. Hizi hapa takwimu zake

Hatimaye Fadlu Davids atangazwa kuwa Kocha wa Simba SC. Hizi hapa takwimu zake

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Klabu ya Simba ya Tanzania imemtangaza rasmi Kocha wa zamani wa Orlando Pirates, Fadlu Davids (43) ambaye ameachana na nafasi yake ya Kocha Msaidizi wa Klabu ya Raja Casablanca kuja kuinoa miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Davids, pamoja na kocha wa zamani wa Orlando Pirates Josef Zinnbauer, walisaidia Raja Casablanca kushinda Ligi ya Morocco ya Botola Pro bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Soma: Tetesi: - Huyu hapa kocha mpya wa Simba SC

Hata hivyo, haikuwa hivyo tu kwani Davis pia aliisaidia timu hiyo kutwaa Throne Cup, kwa kuifunga AS FAR ambayo iliongozwa na Kocha anayeenda kuinoa Kaizer Chief, Nasreddine Nabi.

Wana Msimbazi wana matumaini kuwa Davids kwamba ataweza kupata aina ile ile ya mafanikio ambayo aliweza kupata huko Morroco.

Hata hivyo, hilo linaweza lisiwe rahisi, kwani wapinzani wa Simba, Young Africans, wamekuwa na nguvu kubwa katika soka la Tanzania na hivi karibuni walitawazwa kuwa mabingwa wa ligi.

IMG_0583.jpeg


IMG_0584.jpeg

IMG_0585.jpeg

IMG_0586.jpeg
 
Kocha hata awe mzuri vipi sijui amefundisha Real Madrid au Brazil akienda tu kolokoloni basi mbumbumbu wa hovyo sana watamshusha cv yake kwa kumpa wachezaji wazee hawafundishiki basi kocha atatupiwa zigo la lawama kwa kufungwa na kila striker mkali kama Koplo Samson Mbangula wa Prison au Shentembo Waziri Junior wa KMC.

Huyu kocha mpya aliekuwa kocha msaidizi wa Raja nae ahesabu siku tu coz watamtimua baada ya kupokea kichapo kinachokuja cha 7-0 toka jangwani, huku Chama akifunga magoli 2, Dube 3 na Aziz Ki 2!!

Huyo kocha tumemfuatilia tangu mtoto mdogo tumejiridhisha hamna kitu na msimu huu mpya Simba itashika nafasi ya nne na itapendeza sana hapo! Chief Mangungo ni mtu na nusu msimu ukiisha atahamia Yanga kama Senzo maana nabii hakubaliki nyumbani kwao!!

Uchawi sio lazima kuruka na ungo usiku hata sisi mashabiki uto lia lia kuiombea simba kucheza kombe la loosers na kufanikiwa , pale tuliwachawia makolo ila ni baada ya wao kututukana sana eti sisi uto ni wa matopeni, leo kibao kimegeuka!!Simba imekuwa ndondo club ni kujipigia tu!!
 
Back
Top Bottom