Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Klabu ya Simba ya Tanzania imemtangaza rasmi Kocha wa zamani wa Orlando Pirates, Fadlu Davids (43) ambaye ameachana na nafasi yake ya Kocha Msaidizi wa Klabu ya Raja Casablanca kuja kuinoa miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Davids, pamoja na kocha wa zamani wa Orlando Pirates Josef Zinnbauer, walisaidia Raja Casablanca kushinda Ligi ya Morocco ya Botola Pro bila kupoteza mchezo hata mmoja.
Soma: Tetesi: - Huyu hapa kocha mpya wa Simba SC
Hata hivyo, haikuwa hivyo tu kwani Davis pia aliisaidia timu hiyo kutwaa Throne Cup, kwa kuifunga AS FAR ambayo iliongozwa na Kocha anayeenda kuinoa Kaizer Chief, Nasreddine Nabi.
Wana Msimbazi wana matumaini kuwa Davids kwamba ataweza kupata aina ile ile ya mafanikio ambayo aliweza kupata huko Morroco.
Hata hivyo, hilo linaweza lisiwe rahisi, kwani wapinzani wa Simba, Young Africans, wamekuwa na nguvu kubwa katika soka la Tanzania na hivi karibuni walitawazwa kuwa mabingwa wa ligi.