Kwa yaliyojiri kesi ya ubakaji kwa Emmanuel mbasha, halafu Flora alisema kipindi kile mbasha alitaka kumuua na baada ya hapo alijua atanyea debe miaka 30, lakini mbasha alisema Mungu atanitetea na ukweli amemtetea.
Cha ajabu Flora anaondoa madai ya talaka aliyoitaka alipokua na uhakika mbasha atafungwa na kusema anampenda kwa magoti. Yaani mbasha atamwamini vipi tena? Bora angeomba talaka wakati ashafungwa lakini unachukua urithi kabla mwenyewe hajafa!
Biblia inasema katika mithali ya mwisho kabisa, "mke mwema, hufanya moyo wa mume kumwamini... Lakini hii! Kama ingekuwa ni mimi namsamehe mbele za Mungu lakini harudi, maana talaka ukishaomba ni kama Sala kwa Mungu aombaye hupokea.
Ndoa ndoano