15 November 2024
Uchafuzi wa Uchaguzi Msumbiji 2024: Ghasia za baada ya uchaguzi na ukandamizaji lazima zikome, wanasema wataalam wa Umoja wa Mataifa
9:34 | 15 Nov 2024
Picha: OHCHR
Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa* leo wamezitaka mamlaka nchini Msumbiji kuzuia na kukomesha mara moja unyanyasaji na ukandamizaji wa waandishi wa habari, wanasheria, watetezi wa haki za binadamu na waandamanaji na kuhakikisha waliohusika wanachunguzwa na kufunguliwa mashtaka.
Kufuatia uchaguzi wa tarehe 9 Oktoba 2024 nchini humo, ripoti thabiti zinaonyesha ghasia na hatua za ukandamizaji zilizotumiwa dhidi ya waandamanaji katika maandamano ya amani, ambayo yaliendelea na kutolewa ripoti hadi tarehe 7 Novemba 2024, yalisababisha vifo vya watu 30, kujeruhi watu 200 na kupelekea kukamatwa kwa angalau 300.
"Ukiukwaji wa haki ya kuishi, ikiwa ni pamoja ya watoto, mauaji ya makusudi ya waandamanaji wasio na silaha na utumiaji nguvu kupita kiasi wa polisi waliotumwa kutawanya maandamano ya amani kote Msumbiji ni jambo la kustusha sana," wataalam walisema.
"Tunatoa wito kwa mamlaka za Msumbiji kuchunguza kwa haraka na bila upendeleo mauaji yote kinyume cha sheria."
Maandamano kadhaa katika wiki za hivi karibuni kupinga kukosekana uadilifu katika mchakato wa uchaguzi.
"Mamlaka zinahitaji kuchukua hatua kukomesha ghasia na kuhakikisha mazingira ambayo wananchi wote wa Msumbiji, ikiwa ni pamoja na wanawake na wasichana, wanaweza kushiriki kikamilifu na kwa usawa katika michakato ya kisiasa na kujieleza bila woga," wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa walisema.
"Wasimamizi wa sheria wana jukumu la kuheshimu na kulinda wale wanaotumia haki yao ya kukusanyika kwa amani, na maafisa lazima wawe na msimamo na kutopendelea wakati wa maandamano yoyote, kuzuia madhara na kulinda haki ya kuishi, uhuru na usalama wa watu wanaohusika katika maandanano."
Wataalamu hao walisema kutoweka kwa usalama atika muktadha wa ghasia za uchaguzi kuna athari ya kudumu kwa mfumo wa kidemokrasia wa Mataifa.
Vikwazo kwa uhuru wa vyombo vya habari pia vimeripotiwa sana, ikiwa ni pamoja na mashambulizi, vitisho na unyanyasaji wa wanahabari, na mtandao wa intaneti kuzimwazimwa na vizuizi vya mara kwa mara kwa huduma za mtandao wa simu za viganjani.
Watetezi wa haki za binadamu wanaoripoti kuhusu ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi, uchafuzi wa chaguzi au ripoti za kushiriki maandamano wametishwa na hivyo kuingia hofu.
"Tunaziomba mamlaka za Msumbiji kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa wote na tunalaani usumbufu mkubwa wa huduma za mtandao, ambao umeripotiwa sanjari na maandamano na maandamano yaliyotangazwa," wataalam hao walisema.
Wataalamu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wapo katika mazungumzo na mamlaka ya Msumbiji kuhusu masuala haya na wanafuatilia kwa karibu hali hiyo.
*Wataalamu hao: Gabriella Citroni (Mwenyekiti-Rapporteur), Grażyna Baranowska (Makamu Mwenyekiti), Aua Baldé, Ana Lorena Delgadillo Pérez na Mohammed Al-Obaidi, Kikundi Kazi cha Kutoweka kwa Kutekelezwa au Kutoweka kwa Hiari; Irene Khan , Ripota Maalum kuhusu ukuzaji na ulinzi wa haki ya uhuru wa maoni na kujieleza; Gina Romero , Ripota Maalum kuhusu haki za uhuru wa kukusanyika kwa amani na kujumuika; George Katrougalos, Mtaalamu wa Kujitegemea juu ya kukuza utaratibu wa kimataifa wa kidemokrasia na usawa; Mary Lawlor , Mwandishi Maalum wa watetezi wa haki za binadamu; Reem Alsalem , Ripota Maalum kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na wasichana; Margaret Satterthwaite , Mwandishi Maalum kuhusu uhuru wa majaji na mawakili; Morris Tidball-Minz , Ripota Maalum juu ya utekelezaji usio wa kisheria, muhtasari au unyongaji kiholela; na Alice Jill Edwards , Ripota Maalum wa Mateso na Adhabu au Adhabu nyingine za Kikatili, Kinyama au za Kushusha hadhi.
Wanahabari Maalum ni sehemu ya kile kinachojulikana kama Taratibu Maalum za Baraza la Haki za Kibinadamu. Taratibu Maalum, chombo kikubwa zaidi cha wataalam huru katika mfumo wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, ni jina la jumla la mifumo huru ya Baraza la kutafuta ukweli na ufuatiliaji ambayo inashughulikia ama hali maalum za nchi au masuala ya mada katika sehemu zote za dunia.
Wataalam wa Taratibu Maalum hufanya kazi kwa hiari; wao si wafanyakazi wa UN na hawapati mshahara kwa kazi zao. Wako huru dhidi ya serikali au shirika lolote na wanahudumu kwa nafasi zao binafsi.
Chanzo: Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu (OHCHR) / Taarifa kwa Vyombo vya Habari. Geneva.