Hatimaye Halima Mdee na Wenzake wafungua kesi ya Kupinga kuvuliwa uanachama Mahakama Kuu

achia haki itamalaki mapema tujue nani kawapeeka bungeni kinyemela lazima tutafahamu nani aliandika barua ya kuwateua, na nani aliamrisa akina nusrati watoewe magereza usiku , hili shauri liatawaacha uchi NEC na Ofisi ya Bunge.
Mahakama sasahivi aina longolongo za ucheleweshaji wa hukumu subiri uone
Ikusaidie nini? Je, wewe utapata huo ubunge? au dada yako ataupata? Waache wajivinjari mabinti wa watu
 
acha kukomenti utumbo wewe , hunijui sikujui,sikubaliani kabisa na upuuzi wa watu kutumia kodi yangu nayolipa kinyume cha sheria na utaratiu
 
Huenda wameshapewa Maelekezo toka juu! Vile vile huenda Jaji,DPP,NEC,Mwanasheria Mkuu nao wameshapewa Maelekezo!
Kesi itaharakishwa na kesi watashinda asubuhi tu .
 
acha kukomenti utumbo wewe , hunijui sikujui,sikubaliani kabisa na upuuzi wa watu kutumia kodi yangu nayoipa kinyume cha sheria na utaratiu
Unaumwa si bure! Sema wewe ni Chadema na kwa vile Lissu hawapendi ndiyo maana unapayuka ovyo
 
Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    23.4 KB · Views: 3
😁😁😁 kumbe vita bado mbichi ?

hapo ni zengwe mpaka muda wa ubunge uishe .

chezea Tanzania wewe ?
 
Waliokuwa wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18, tayari wamefungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua shauri hilo siku 13 baada ya kupata kibali cha mahakama hiyo.

Mahakama hiyo imewaruhusu Mdee na wenzake kufungua shauri hilo Julai 8, 2022 baada ya kukubaliana na hoja zao katika maombi waliyokuwa wameyafungua wakiomba ridhaa hiyo.

Mawakili wa kina Mdee, Ipilinga Panya na Aliko Mwamanenge wameieleza Mwananchi Digital kwa nyakati tofauti kuwa walifungua shauri hilo jana Alhamisi Julai 21, 2022 na kwamba mpaka jioni lilikuwa limeshasajiliwa baada ya nyaraka walizoziwasilisha mahakamani hapo kufanyiwa ukaguzi na mahakama kujiridhisha kuwa zimekamilika na taratibu zimefuatwa kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la maombi ya mapitio ya Mahakama, Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawache wa chama hicho (Bawacha) na wenzake wanapinga uamuzi wa kufukuzwa uanachama uliotolewa na Baraza Kuu la Chadema Mei 11, 2022.

Katika uamuzi huo, Baraza hilo lilitupilia mbali rufaa zao walizozikata wakipinga uamuzi wa awali wa kuwavua uanachama uliotolewa na Kamati Kuu ya Chadema Novemba 27, 2020. Badala yake Baraza hilo liliunga mkono uamuzi huo wa Kamati Kuu.

Kamati Kuu iliwavua uanachama baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kukubali na kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho.

Kufuati uamuzi huo walifungua maombi Mahakamani hapo wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga uamuzi huo, pamoja na mambo mengine wakidai kuwa mchakato na uamuzi wa kuwavua uanachama haukufuata taratibu na misingi ya kisheria kwa kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa.

Mahakama ilikubaliana na maombi yao baada ya kuridhika kuwa walikuwa wamekidhi matakwa na vigezo vya kisheria kustahili kupewa ridhaa hiyo.

Baada ya kupata ridhaa hiyo walitakiwa kufungua shauri hilo ndani ya siku 14 kwa mujibu wa sheria, tangu tarehe ya uamuzi wa maombi ya ridhaa, ambazo zinaisha leo Julai 22, 2022.

Baada ya kukamilisha hatua hiyo, ya kufungua shauri hilo, sasa wanasubiri tatatibu nyingine za kimahakama ikiwa ni pamoja kupangiwa jopo la majaji watakaosiliza shauri lao hilo na tarehe ya kutajwa na Kisha tarehe ya usikilizwaji baada ya taratibu zote kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
Eti wanasemaje!!?

Wanapinga kufukuzwa kwao uanachama kwa sbb hawakupewa nafasi ya kusikilizwa...?

Naamini wanaposema "hawakupewa nafasi ya kusikilizwa" nadhani wana maana sawa na kusema "hawakupewa nafasi ya kujitetea", au siyo jamani...?

Kama wana maana hii, basi hawa kinadada ni waongo sana...!

Wao ndiyo walikuwa hawataki wajitetee/wasikilizwe utetezi wao juu ya tuhuma zinazowakabili. Maana kama ni ishu ya kupewa nafasi, walipewa kote kote kule KK na katika BK...

Lakini ni ukweli ulio wazi kuwa, wao ndo walikataa/ walishindwa kuitumia nafasi hiyo kujitetea ili wasikilizwe na ili kuwezesha watu (wajumbe) kutoa maamuzi yao....

To cut the story short, it absolutely true to say that, all the evidence is pointing against them...

Mfano, juzi kati tu hapa kwenye kikao cha Baraza Kuu (BK), Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa uwazi kabisa huku camera za TV zikionesha kila kitu, kabla ya kura ya maamuzi kupigwa alitoa nafasi hiyo kwa kina mama hawa, kwa yeyote kusema lolote kama alikuwa na cha kusema ikiwemo kujitetea...

Bahati mbaya sana kwa kina dada hawa, hakuna aliyesimama kusema lolote ikiwa ni pamoja na kujitetea kama walikuwa na utetezi wowote...

Ni nini hasa kina dada hawa wanataka...?
 
sw
Waliokuwa wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18, tayari wamefungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Mdee na wenzake wamefungua shauri hilo siku 13 baada ya kupata kibali cha mahakama hiyo.

Mahakama hiyo imewaruhusu Mdee na wenzake kufungua shauri hilo Julai 8, 2022 baada ya kukubaliana na hoja zao katika maombi waliyokuwa wameyafungua wakiomba ridhaa hiyo.

Mawakili wa kina Mdee, Ipilinga Panya na Aliko Mwamanenge wameieleza Mwananchi Digital kwa nyakati tofauti kuwa walifungua shauri hilo jana Alhamisi Julai 21, 2022 na kwamba mpaka jioni lilikuwa limeshasajiliwa baada ya nyaraka walizoziwasilisha mahakamani hapo kufanyiwa ukaguzi na mahakama kujiridhisha kuwa zimekamilika na taratibu zimefuatwa kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la maombi ya mapitio ya Mahakama, Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawache wa chama hicho (Bawacha) na wenzake wanapinga uamuzi wa kufukuzwa uanachama uliotolewa na Baraza Kuu la Chadema Mei 11, 2022.

Katika uamuzi huo, Baraza hilo lilitupilia mbali rufaa zao walizozikata wakipinga uamuzi wa awali wa kuwavua uanachama uliotolewa na Kamati Kuu ya Chadema Novemba 27, 2020. Badala yake Baraza hilo liliunga mkono uamuzi huo wa Kamati Kuu.

Kamati Kuu iliwavua uanachama baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kukubali na kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho.

Kufuati uamuzi huo walifungua maombi Mahakamani hapo wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga uamuzi huo, pamoja na mambo mengine wakidai kuwa mchakato na uamuzi wa kuwavua uanachama haukufuata taratibu na misingi ya kisheria kwa kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa.

Mahakama ilikubaliana na maombi yao baada ya kuridhika kuwa walikuwa wamekidhi matakwa na vigezo vya kisheria kustahili kupewa ridhaa hiyo.

Baada ya kupata ridhaa hiyo walitakiwa kufungua shauri hilo ndani ya siku 14 kwa mujibu wa sheria, tangu tarehe ya uamuzi wa maombi ya ridhaa, ambazo zinaisha leo Julai 22, 2022.

Baada ya kukamilisha hatua hiyo, ya kufungua shauri hilo, sasa wanasubiri tatatibu nyingine za kimahakama ikiwa ni pamoja kupangiwa jopo la majaji watakaosiliza shauri lao hilo na tarehe ya kutajwa na Kisha tarehe ya usikilizwaji baada ya taratibu zote kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
swali langu ni jee!! endapo mahakama itakubali na kuwazuia wasifukuzwe uanachama na watabaki kuwa wanachama.. vipi nafazo zao za uongozi wataziteteaje... je kwa chama CDM wanachama ambao ni wajumbe na viongozi katika mabaraza ya chama wasipoonekana kuhudhuria mijadala ya chama je chama kinapaswa kuchukua hatua gani tena nyingine?
 
Wewe ni nani? Acha makasiriko, hao wapo hadi 2025
Na wewe ni nani ambaye hutaki mahakama ifanye maamuzi mapema shauri hilo.
Inaonyesha huna akili kabisa " justice delayed justice denied.
Wewe nazani kichwani kwako kuna matope hakuna hata ubongo
 
Nakueleza hali halisi ilivyo. Wewe unaleta U Tundu Lissu. Hao unao hadi 2025
 
Back
Top Bottom