Hatimaye Kenya wamempata Magufuli wao

Atafanye yote lakini sio kusigina katiba..

MK254 pingli-nywee
Hapo sasa, akipenda anaweza akaingia hadi studio achomoe wimbo wa 'kutoboa' hayo yote anayoyazungumzia mleta mada. Ila mwisho wa siku kama hatakuwa amekiuka sheria yeyote kikatiba, atajibiwa kwa mtindo huo huo. Tena kunao wengine wengi madomo zege zaidi yake na hataweza kuwafanya lolote. Ndio siasa za kidemokrasia hizo.
 
Sijui aliokotwa wapi huyu, simpendi kwa kweli na atawajibishwa hivi karibuni maana katiba itambana, anaropokwa kishenzi.

Sasa Gachagua ndio Rais mzuri na atamsukuma Ruto kufanya mambo ya msingi sana , straight leaders on articulation hua ni wakweli na wanajiamini. Mkipata kiongozi wa aina hiyo maendeleo lazima japo kuna kundi litaonja joto la jiwe
 
Sijui aliokotwa wapi huyu, simpendi kwa kweli na atawajibishwa hivi karibuni maana katiba itambana, anaropokwa kishenzi.
Kila kitu kuhusu Rigathi kina udhi, zaidi ya maelezo, sio domo lake tu. Hata jina lake la utani ambalo walimpa, eti Riggy G, linatia kinyaa kweli kweli. Huwa najiuliza kila mara ilikuwaje hadi huyu jamaa akawa naibu rais wetu. Anachoweza huyu ni kudensi tu, akiingia dance floor labda mchawi tu ndio anaweza akachukia. πŸ˜„
 
Mbona kama anaonekana ni mwenzetu/mshiriki
 
Sasa Gachagua ndio Rais mzuri na atamsukuma Ruto kufanya mambo ya msingi sana , straight leaders on articulation hua ni wakweli na wanajiamini. Mkipata kiongozi wa aina hiyo maendeleo lazima japo kuna kundi litaonja joto la jiwe

Kuropokwa ropokwa sio uongozi, hilo neno "articulative" umelitumia pabaya, nafikiri Ruto alikua na sababu za kimkakati kumuweka hapo, awe anamtumia kama chombo cha kuropokwa vitu vya hovyo, vitu ambavyo yeye akivisema vitaitia doa serikali, ni kama leo mumpe umakamu yule mbunge wenu anayeitwa Musukuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…