Hatimaye Kenya wamempata Magufuli wao

Hatimaye Kenya wamempata Magufuli wao

Atafanye yote lakini sio kusigina katiba..

MK254 pingli-nywee
Hapo sasa, akipenda anaweza akaingia hadi studio achomoe wimbo wa 'kutoboa' hayo yote anayoyazungumzia mleta mada. Ila mwisho wa siku kama hatakuwa amekiuka sheria yeyote kikatiba, atajibiwa kwa mtindo huo huo. Tena kunao wengine wengi madomo zege zaidi yake na hataweza kuwafanya lolote. Ndio siasa za kidemokrasia hizo.
 
Sijui aliokotwa wapi huyu, simpendi kwa kweli na atawajibishwa hivi karibuni maana katiba itambana, anaropokwa kishenzi.

Sasa Gachagua ndio Rais mzuri na atamsukuma Ruto kufanya mambo ya msingi sana , straight leaders on articulation hua ni wakweli na wanajiamini. Mkipata kiongozi wa aina hiyo maendeleo lazima japo kuna kundi litaonja joto la jiwe
 
Sijui aliokotwa wapi huyu, simpendi kwa kweli na atawajibishwa hivi karibuni maana katiba itambana, anaropokwa kishenzi.
Kila kitu kuhusu Rigathi kina udhi, zaidi ya maelezo, sio domo lake tu. Hata jina lake la utani ambalo walimpa, eti Riggy G, linatia kinyaa kweli kweli. Huwa najiuliza kila mara ilikuwaje hadi huyu jamaa akawa naibu rais wetu. Anachoweza huyu ni kudensi tu, akiingia dance floor labda mchawi tu ndio anaweza akachukia. 😄
 
Nakumbuka kipindi fulani Magufuli akiwa Rais basi tukasikia habari kuwa Wakenya wanamfagilia mbaya na wangetamani kuwa na Rais wa aina hiyo. DP wao ndio Magufuli, sio Ruto kama wengi walivyodhani

Sasa kuna huyu jamaa, Kaimu wa Rais, Rigathi Gachagua, ndio wakenya wana experience Magufuli wao

Jamaa anatiririka bila kuchuja maneno, yaani ustaarabu wa uongozi ni zero
Ukisikia akiongea ni burudani tu [emoji16][emoji16]

Picha lilianza siku ya kuapishwa anaanza kumnanga Uhuru palepale kuwa wameifilisi serikali

Siku nyingine namsikia akiwaambia wananchi wa kabila la Wakamba kuwa aligombana na Ruto kuteua waziri kutoka kwenye kabila lao maana walipigia kura upinzani

Juzi nimesikia tena akimuambia Ruto amuachie Raila ili aonyeshe namna ya kumnyoosha [emoji1787]

Jamaa akiwa kanisani huko Mlima Kenya nafikiri, akaanza kuwananga waliompigia kampeni Raila, mara akamfokea mwanamuziki anaitwa Ben Gitae kwa kumuimbia nyimbo Raila

Kisha akasema kamsamehe na kuagiza palepale apewe kazi Ikulu, jamaa kama vile Ikulu ni kioski chake binafsi vile[emoji1787]

Halafu jamaa ana mind sana watu wa kabila lake kuwa upande wa Raila, anaona kama usaliti wa hali ya juu

View attachment 2493664

View attachment 2493665
View attachment 2493663

Mbona kama anaonekana ni mwenzetu/mshiriki
 
Sasa Gachagua ndio Rais mzuri na atamsukuma Ruto kufanya mambo ya msingi sana , straight leaders on articulation hua ni wakweli na wanajiamini. Mkipata kiongozi wa aina hiyo maendeleo lazima japo kuna kundi litaonja joto la jiwe

Kuropokwa ropokwa sio uongozi, hilo neno "articulative" umelitumia pabaya, nafikiri Ruto alikua na sababu za kimkakati kumuweka hapo, awe anamtumia kama chombo cha kuropokwa vitu vya hovyo, vitu ambavyo yeye akivisema vitaitia doa serikali, ni kama leo mumpe umakamu yule mbunge wenu anayeitwa Musukuma.
 
Back
Top Bottom