Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Nyie Pro- Gadaffi mnatumia ufalme wa Uingereza (Malkia) ambaye ni nembo ya utamaduni na alama ya taifa na sio kiongozi wa serikali kuhalalisha udikteta wa Marehemu Gadaffi.

Hata Canada inaongozwa na waziri mkuu mwenye mamlaka yote ya serikali ila ufalme wa Uingereza (Malikia Elizabeth) unasimama kama alama au nembo ya taifa lao maana ilishawahi kuwa himaya ya Uingereza.

Hata kiongozi wa nchi za jumuiya ya madola ni Malkia Elizabeth kwa sababu nchi hizo ziliwahi kuwa chini ya himaya ya Uingereza kabla hazijapata Uhuru, hivyo Malkia amesimama kama nembo au alama ya utamaduni tu.
 
Hujui kitu! Malkia wa Uingereza ndiyo mwamuzi wa mwisho wa mambo yote ya taifa la Uingereza na wala si Waziri Mkuu ama Bunge, Malkia akikataa kitu ndiyo mwisho hakuna wa kuhoji.
 
Malkia wa Uengereza ndie anaetia saini kuwa apeleke jeshi nchi yyte, bila ya saini yake uk wasingeshiriki vita Iraq na Libya au Syria
 
Kwa kweli but. ... Nadhani Sasa taratiibu walibya wanakula mazao ya kuisaka demokrasia. Demokrasia ambayo wamarekani wameshindwa kuitekeleza kwa urhabiti nyumbani kwao
 
Demokrasia kwa nchi za kiarabu haiwezekani . Wao walishazoea utawala wa kifalme! Kilichofanyika dahari kwa dahari ni mapinduzi ya ghafla ya kuondoa tawala hizi kwa namna ya haraka bila Vita nzito country wide rejea Misri , Libya , Sudan, Saudia,
 
Hujui kitu! Malkia wa Uingereza ndiyo mwamuzi wa mwisho wa mambo yote ya taifa la Uingereza na wala si Waziri Mkuu ama Bunge, Malkia akikataa kitu ndiyo mwisho hakuna wa kuhoji.
Punguza uongo ndugu waziri mkuu was Uingereza alitia saini kulipeleka likizo bunge na malkia alikubali lakini bunge likapinga na vikao vya bunge vikaendelea kama kawaida sasa jiulize jambo kama hilo linaweza kutokea kwenye kama Morocco, Swaziland au Saudi Arabia?
 
Ishu nikwamba yeye pekee ndio anahaki yakuiongoza hio UK kuliko wengine ?! Mpaka anamiaka 40 sasa mamlakani bila kupisha wengine ?! Kua namamlaka ama kutokua nayo wala sio ishu ishu nikwamba wengine hawana uwezo wakua ceremonial leader isipokua wao tu ?!...
 
Bora wateseke maana huo ulikuwa uchaguzi waliouona unafaa..
 
Kwahiyo Malkia hana hata chembe ya mamlaka pale uingereza yeye anakula mema ya nchi tu basi hadi kufa kwake?
 


Tangu lini mabeberu weusi ama wayahudi weusi mkamsapoti Muislamu/Muarabu, na isitoshe ndani ya bara letu! never never never na haitatokea kwenu kuwa upande wao mpaka mtakapozinduka. Nyie viumbe msio na imani wala huruma mnachoangalia ni dini/rangi ya mtu ndio kigezo chenu,, mfano mdogo tu kwa huyo RAISI "GADAFI" Lau mauwaji hayo yangefanyika kwa Raisi asie muislamu/mwarabu iwe kwa south afrika, Kenya, uganda ama marekani yani ingewagusa sana sana nyie watu. ila wapo wachache tu wenye kujitambua,wenye imani na huruma zao.
 

Wenyewe wanakuambia Mzungu hakoseagi 😁
 
Hujajibu swali
 
Hujui kitu! Malkia wa Uingereza ndiyo mwamuzi wa mwisho wa mambo yote ya taifa la Uingereza na wala si Waziri Mkuu ama Bunge, Malkia akikataa kitu ndiyo mwisho hakuna wa kuhoji.
Una uhakika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…