Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Nasisitiza kuwa lengo la Ghadafi kuvamiwa sio hoja ya demokrasia, wakubwa hawakunyonya mafuta bure. Mbona Saud Arabia hakuna hiyo demokrasia? Kwa nini wasiwavamie sasa wapeleke hiyo demokrasia?
Mbona Venezuela Wana demokrasia nzuri tu, kwa nn wanamsumbua Madulo?
Mbona hawamvamii M7?
Kama wanakupa kwako wanapiga kimya tu.
Africa tuamke
Hapa kwetu Tanzania tangu 95 Multipartism imefeli vibaya. Vyama kibao vya kijinga tupu. Kwa nini tusiamue sisi wenyewe kuwa na vyama viwili tu Tena kikatiba halafu tukapambana kwa hoja na kukubali kubadilisha madaraka kwa amani?
gadafi alivamiwa kwa kivuli cha demokrasia ila uhalisia ni mafuta. Maduro anang'ang'aniwa kule kwa kivuli cha demokrasia ila uhalisia ni mafuta tu
 
Libya walikua na zaidi ya reserve $150 billion yaani zaidi ya trillion 300 za kibongo hatari sana
 
Tunapoelekea libya itakuwa zaidi ya syria,,sababu uturuki wamekita mizizi,,waarabu wamepagawa sana,,kama ujuavyo nchi nyingi za kiarabu zilipigana na uturuki ndo zikapata uhuru,
Sasa wanaona uturuki anazidi kujitanua,mturuki kakamata ardhi syria,anajongea iraq,,ana kambi za jeshi Qatar,somalia na sasa libya,,
Halmark zote za uturuki kutaka kujitanua na kurudisha himaya ya ottoman,ziko wazi,
So waarabu sasa wanaungana wakuongozwa na Egypt dhidi ya uturuki nchini libya,
Kama vita itazuka hii itakuwa kiboko,
Uturuki yuko na Qatar, italy,na US kwa mbali,dhidi ya Egypt,Uae, Russia,france,saud na wapambe wao,mambo ni fire,,inaonekana mturuki yuko mafuta vibaya,,nani atamfunga breki ndo suala wanajiuliza,
Marekani anamgwaya,Russia hawajui la kufanya,,ulaya wamepaniki
Waarabu waliungana na Uturuki kumhujumu mwarabu mwenzao Syria (Assad).

Kitendo cha Uturuki kujiingiza Libya kimewachukiza waarabu na wamegundua walikosea huko Syria kwani Uturuki sio mshirika mwenye nia nzuri zaidi ya kujitanua kwenye ardhi ya waarabu na kurudisha ushawishi kwenye maeneo yaliyokuwa sehemu ya himaya yake (Ottoman).

Ndiyo maana nchi zote za kiarabu (isipokuwa Qatar) zimejiondoa kufadhili waasi Syria na kumuachia mzigo wote Uturuki.
 
Inauma lakini tatizo kubwa la viongozi wa ki Africa na hata za ki Arab ni kung'ang'ania madarakani kwa njia moja ama nyingine.

Huwezi kuwatawala watu wenye akili na ufahamu kwa zaidi ya miaka 42 na bado ukataka mwanao akurithi !!. Watakufanyia fitna tu.
Siyo lazima kila mtu awe kiongozi au mtawala, kuna wengine lazima waongozwe.
Kuna faida na hasara gani hapo wamepata baada ya kumtoa Ghadaf?

Na hapa Tanzania wapinzani wenye tamaa mbaya ya madaraka wanaelekea kutuingiza nchi yetu kwenye janga kama hili.
Tujifunze kwa walibya sasa wanajuta hata robo ya kile walichokuwa wanapewa na serikali ya Ghadaf hawakipati sasa.
 
Kura au chochote kisingesaidia Libya ilikuwa kwenye rada za CIA na MI5 kitambo sana kama Iraq Afghan na Syria hata ingekwepa vipi ilikuwa lazima itokee
Hapo ndipo ukweli huwa hausemwi, ukiwa km kiongozi lazima usome nyakati na unachokijenga ili kiwe faida kwa wengine lazma kuwe na kiasi. Binadamu ni mtu asiyerizika kwa hiyo watu walibya waliamini wangepata zaidi na haiwezekani mtu mmoja aongoze nchi kwa zaidi ya miaka arobaini na bado anataka kurithisha mtoto. Gadafi ilibidi aachie madaraka pale alipoanza kuona upingamizi juu yake ampe madaraka kwa mtu mwingine aliyemuamini hata km ingekuwa kwa sanduku la kura then baadae uwezekano wa mwanae kupata uraisi ungeweza kuja na heshima yake ingebaki na nchi ingekuwa salama. Lakini kushupaza shingo akakosa vyote uhai na utajiri wa nchi.
 
Huu ndio uhalisia ukweli ni kwamba Gaddafi hajauliwa sababu ya demokrasia hicho kilikuwa ni kichaka tu,mipango ya Gaddafi kwa Libya na afrika ilikuwa tishio hasa ile pesa aliyotaka kuweka kwenye bank of Africa na kubadili medium of exchange kwenye oil iwe dinar badala ya dollar fujo zikaanza na ziara ya condoleza rice ndio kabisa iliua kila kitu
Tukubali tu kuwa watu wenye asili ya kiarabu uongozi wa kifalme ndo njia sahihi, wangeuboresha tu Basi,mfano angalia Iraq demokrasia wapi na wapi?
Ni kweli Ghadafi alikaa sana madarakani, na Hawa wazungu hawajamtoa kisa demokrsia, sio, he was a big threat to their economic interests.
Huoni walivyo muua demokrasia iko wapi?
Wenye maono ya kitaifa wanataka kiongozi bora na sio uchaguzi wa Kila Mara. China wamepata mwamba Xi na Ususi wamepamata mtaalamu Vladimir Putin
Linganisha hao na sisi ambao Kila Mara tunawaza uchaguzi hamna kitu
 
Mimi naamini kabisa walibya wengi wameingizwa tu kwenye hii vita na wachache walio kuwa well trained na Europeans (refer ISIS) ila wao kama wao hawakutaka ila unajua hao wanaotaka madaraka huwa wana sauti kubwa sana wanakuchanganya na maneno mengi na ahadi ahadi hadi unaingia kwenye mkenge ukijua ni vijimaandamano tu kumbe ndio mwanzo wa vita
Ila duniani kuna vitu vya ajabu sana,yani kwamba wananchi Libya wameona bora waingize nchi vitani kwa sababu ya Gadaffi hataki kuwaachi nafasi na wenzake nao watawale walibya.

Yani kama Tz wananchi tuingize nchi vitani kwa sababu tunataka ccm itoke madarakani imekaa sana hivyo ni zamu ya Chadema au Act nao watutawale.
 
Siyo lazima kila mtu awe kiongozi au mtawala, kuna wengine lazima waongozwe.
Kuna faida na hasara gani hapo wamepata baada ya kumtoa Ghadaf?

Na hapa Tanzania wapinzani wenye tamaa mbaya ya madara wanaelekea kutuingiza nchi yetu kwenye janga kama hili.
Tujifunze kwa walibya sasa wanajuta hata robo ya kile walichokuwa wanapewa na serikali ya Ghadaf hawakipati sasa.
Kwanini useme si kila mtu lazima awe kiongozi !!.: Umempima kwa uzani gani ?! Wenye nchi ni wananchi . Wakiamua utoke unatoka Tu usimdharau yeyote.

Wapinzani wapo kikatiba na wakipewa ridhaa na wananchi wanaongoza tu. Haitazuia jua kuchomoza wala kuzama
 
Mnaosema kuwa Malkia wa Uingereza ni dikteta, rudini mkasome vizuri kuhusiana na udikteta na zaidi pateni kuufahamu vizuri mfumo wa kiutawala uliopo Uingereza.

Ni dhahiri kuwa wengi wenu hamfahamu vyema nini maana ya udikteta. Hamuufahamu 'Udikteta'.

Acheni uvivu, someni, rudini katika historia, fanyeni tafiti.
 
Tukasome nini malkia anachaguliwa nanani ?!
 
Shida sio KUNG'ANG'ANIA MADARAKA.
mbona uingereza hyo demokrasia hamna?.
Uingereza wanaongozwa na malikia.
Kwanini wamarekani na wazungu waone kuwa gaddafi hafai?
Mtu unajiita "mjingamimi" !! Unajua mifumo ya tawala ulimwenguni ?! Ukielezwa uielezee utaitoa kasoro ipi kwa mfumo huo wa UK ?! Kumbuka malkia ni ceremonial. Na si kiongozi wa serikali inayohusika na maisha ya wananchi.
 
Anachaguliwa nanani ?!

Ama hakuna mwengine anaetamani kua ceremonial leader kama yeye ?!

Nakama hana mamlaka yeyote anakaa pale alipo kufanya nini wakati hana mamlaka yeyote ?!.

Ila ishu kubwa hapa anachaguliwa nanani ?!.
 
wote hawakusoma alama za nyakati na kutokufikirisha bongo zao juu ya madhara wanachokifanya.

1;GADAF alipaswa angejitoa mapema kabisa baada ya kuona kelele zinaanza kuliko kuanza kushindana na kelele

2:Raia nao hawakufikiria kwa kina kwa hiki tunachoenda kukifanya na kutambua madhara yake hapo abadae
Tatizo suala la Gadafi kila mtu anaongea lake ila cha muhimu ni kwamba wakubwa wa dunia hawakumtaka tu hakuwa akienda nao sawa na wao ndio waliyofanikisha hilo zoezi,na mwenyewe Gadafi alipata kueleza hili mwishoni mwishoni.

Ila mie nitawaalaumu sana wananchi maana kama Gadafi alikuwa ni tatizo kwao basi walishindwa kutumia njia sahihi za kutatua tatizo lao matokeo yake wamesababisha tatizo kubwa zaidi kuliko tatizo walilokuwa nalo mwanzo.
 
Mtu unajiita "mjingamimi" !! Unajua mifumo ya tawala ulimwenguni ?! Ukielezwa uielezee utaitoa kasoro ipi kwa mfumo huo wa UK ?! Kumbuka malkia ni ceremonial. Na si kiongozi wa serikali inayohusika na maisha ya wananchi.
Ila wanakula mema ya nchi peke yao.
 
Anachaguliwa nanani ?!

Ama hakuna mwengine anaetamani kua ceremonial leader kama yeye ?!

Nakama hana mamlaka yeyote anakaa pale alipo kufanya nini wakati hana mamlaka yeyote ?!.

Ila ishu kubwa hapa anachaguliwa nanani ?!.
Argument zako tangu asubuhi sijui unalenga nini ?!. - Je wa UK wamelalanikia mfumo wao ?!
Viongozi wa kuchaguliwa ni wa vyama vinavyounda serikali .
Na si England tu , tunayo Netherlands, German, nk . Kikubwa ni kuwa katiba zao walizokubaliana zinaheshimiwa. Tofauti na Libya Gadhafi was everything
 
Mnaosema kuwa Malkia wa Uingereza ni dikteta, rudini mkasome vizuri kuhusiana na udikteta na zaidi pateni kuufahamu vizuri mfumo wa kiutawala uliopo Uingereza.

Ni dhahiri kuwa wengi wenu hamfahamu vyema nini maana ya udikteta. Hamuufahamu 'Udikteta'.

Acheni uvivu, someni, rudini katika historia, fanyeni tafiti.
Ila wanakula mema ya nchi peke yao ni sawa na Gadafi alivyokuwa anakula mema ya nchi peke yake.
 
Back
Top Bottom