Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

gadafi alivamiwa kwa kivuli cha demokrasia ila uhalisia ni mafuta. Maduro anang'ang'aniwa kule kwa kivuli cha demokrasia ila uhalisia ni mafuta tu
 
Libya walikua na zaidi ya reserve $150 billion yaani zaidi ya trillion 300 za kibongo hatari sana
 
Waarabu waliungana na Uturuki kumhujumu mwarabu mwenzao Syria (Assad).

Kitendo cha Uturuki kujiingiza Libya kimewachukiza waarabu na wamegundua walikosea huko Syria kwani Uturuki sio mshirika mwenye nia nzuri zaidi ya kujitanua kwenye ardhi ya waarabu na kurudisha ushawishi kwenye maeneo yaliyokuwa sehemu ya himaya yake (Ottoman).

Ndiyo maana nchi zote za kiarabu (isipokuwa Qatar) zimejiondoa kufadhili waasi Syria na kumuachia mzigo wote Uturuki.
 
Siyo lazima kila mtu awe kiongozi au mtawala, kuna wengine lazima waongozwe.
Kuna faida na hasara gani hapo wamepata baada ya kumtoa Ghadaf?

Na hapa Tanzania wapinzani wenye tamaa mbaya ya madaraka wanaelekea kutuingiza nchi yetu kwenye janga kama hili.
Tujifunze kwa walibya sasa wanajuta hata robo ya kile walichokuwa wanapewa na serikali ya Ghadaf hawakipati sasa.
 
Kura au chochote kisingesaidia Libya ilikuwa kwenye rada za CIA na MI5 kitambo sana kama Iraq Afghan na Syria hata ingekwepa vipi ilikuwa lazima itokee
 
Huu ndio uhalisia ukweli ni kwamba Gaddafi hajauliwa sababu ya demokrasia hicho kilikuwa ni kichaka tu,mipango ya Gaddafi kwa Libya na afrika ilikuwa tishio hasa ile pesa aliyotaka kuweka kwenye bank of Africa na kubadili medium of exchange kwenye oil iwe dinar badala ya dollar fujo zikaanza na ziara ya condoleza rice ndio kabisa iliua kila kitu
 
Mimi naamini kabisa walibya wengi wameingizwa tu kwenye hii vita na wachache walio kuwa well trained na Europeans (refer ISIS) ila wao kama wao hawakutaka ila unajua hao wanaotaka madaraka huwa wana sauti kubwa sana wanakuchanganya na maneno mengi na ahadi ahadi hadi unaingia kwenye mkenge ukijua ni vijimaandamano tu kumbe ndio mwanzo wa vita
 
Kwanini useme si kila mtu lazima awe kiongozi !!.: Umempima kwa uzani gani ?! Wenye nchi ni wananchi . Wakiamua utoke unatoka Tu usimdharau yeyote.

Wapinzani wapo kikatiba na wakipewa ridhaa na wananchi wanaongoza tu. Haitazuia jua kuchomoza wala kuzama
 
Mnaosema kuwa Malkia wa Uingereza ni dikteta, rudini mkasome vizuri kuhusiana na udikteta na zaidi pateni kuufahamu vizuri mfumo wa kiutawala uliopo Uingereza.

Ni dhahiri kuwa wengi wenu hamfahamu vyema nini maana ya udikteta. Hamuufahamu 'Udikteta'.

Acheni uvivu, someni, rudini katika historia, fanyeni tafiti.
 
Tukasome nini malkia anachaguliwa nanani ?!
 
Shida sio KUNG'ANG'ANIA MADARAKA.
mbona uingereza hyo demokrasia hamna?.
Uingereza wanaongozwa na malikia.
Kwanini wamarekani na wazungu waone kuwa gaddafi hafai?
Mtu unajiita "mjingamimi" !! Unajua mifumo ya tawala ulimwenguni ?! Ukielezwa uielezee utaitoa kasoro ipi kwa mfumo huo wa UK ?! Kumbuka malkia ni ceremonial. Na si kiongozi wa serikali inayohusika na maisha ya wananchi.
 
Mtu unajiita "mjingamimi" !! Unajua mifumo ya tawala ulimwenguni ?! Ukielezwa uielezee utaitoa kasoro ipi kwa mfumo huo wa UK ?! Kumbuka malkia ni ceremonial. Na si kiongozi wa serikali inayohusika na maisha ya wananchi.
Anachaguliwa nanani ?!

Ama hakuna mwengine anaetamani kua ceremonial leader kama yeye ?!

Nakama hana mamlaka yeyote anakaa pale alipo kufanya nini wakati hana mamlaka yeyote ?!.


Ila ishu kubwa hapa anachaguliwa nanani ?!.
 
Tatizo suala la Gadafi kila mtu anaongea lake ila cha muhimu ni kwamba wakubwa wa dunia hawakumtaka tu hakuwa akienda nao sawa na wao ndio waliyofanikisha hilo zoezi,na mwenyewe Gadafi alipata kueleza hili mwishoni mwishoni.

Ila mie nitawaalaumu sana wananchi maana kama Gadafi alikuwa ni tatizo kwao basi walishindwa kutumia njia sahihi za kutatua tatizo lao matokeo yake wamesababisha tatizo kubwa zaidi kuliko tatizo walilokuwa nalo mwanzo.
 
Mtu unajiita "mjingamimi" !! Unajua mifumo ya tawala ulimwenguni ?! Ukielezwa uielezee utaitoa kasoro ipi kwa mfumo huo wa UK ?! Kumbuka malkia ni ceremonial. Na si kiongozi wa serikali inayohusika na maisha ya wananchi.
Ila wanakula mema ya nchi peke yao.
 
Anachaguliwa nanani ?!

Ama hakuna mwengine anaetamani kua ceremonial leader kama yeye ?!

Nakama hana mamlaka yeyote anakaa pale alipo kufanya nini wakati hana mamlaka yeyote ?!.


Ila ishu kubwa hapa anachaguliwa nanani ?!.
Argument zako tangu asubuhi sijui unalenga nini ?!. - Je wa UK wamelalanikia mfumo wao ?!
Viongozi wa kuchaguliwa ni wa vyama vinavyounda serikali .
Na si England tu , tunayo Netherlands, German, nk . Kikubwa ni kuwa katiba zao walizokubaliana zinaheshimiwa. Tofauti na Libya Gadhafi was everything
 
Ila wanakula mema ya nchi peke yao ni sawa na Gadafi alivyokuwa anakula mema ya nchi peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…