Hatimaye Makamu Rais wa Shirikisho la Riadha John Bayo ajiuzulu

Hatimaye Makamu Rais wa Shirikisho la Riadha John Bayo ajiuzulu

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Hatimaye Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (AT) John Bayo Ajiuzulu.

John Bayo amejiuzulu baada ya kusakamwa na Sakata la Vyeti Feki, ingawa yeye amedai amejiuzulu ili awe busy na familia na biashara zake.

Rais wa RT, Silas Isangi amekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa makamu wake.

Ameongeza kuwa wanatarajia kufanya uchaguzi mwingine ili kuziba mapengo mawili, hiyo ya makamu na ya mjumbe wa Kanda aliyejiuzulu pia.

Ikumbukwe , Katiba inasema kugombea nafasi ya makamu wa rais wa RT lazima uwe na Elimu kuanzia Diploma, katika chuo kinachotambulika.
 
Mambo mengine ni kubaniana tu, sifa ya elimu ya mtu anayetaka kugombea ubunge ni kujua kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza. Haya mambo ya Diploma, degree mara masters at times yana ubabaishaji wake.
 
Huyo jamaa kuna kipindi alikua analalama sana sijui kama ashaacha
Hawezi kuacha, juzi nimemsikia BBC anazungumzia Tanzania kupeleka wanariadha watatu wakati nchi ina watukaribia milioni 60, yule jamaa ana exposure tatizo nchi yetu magumashi sana.
 
Hawezi kuacha, juzi nimemsikia BBC anazungumzia Tanzania kupeleka wanariadha watatu wakati nchi ina watukaribia milioni 60, yule jamaa ana exposure tatizo nchi yetu magumashi sana.
Weeee hamna cha exposure wala nini. Yule ni maugomvi wamezidiana mipigo tu. Mjanja sana yule ukimuuliza Filbert Bayi anamjua vizur
 
Hawezi kuacha, juzi nimemsikia BBC anazungumzia Tanzania kupeleka wanariadha watatu wakati nchi ina watukaribia milioni 60, yule jamaa ana exposure tatizo nchi yetu magumashi sana.
Mwanae ni mwanariadha akiwakilisha marekani
 
Mmemsagia kunguni hadi ametoka, wabongo sio watu wazuri.
 
Back
Top Bottom