Hatimaye makazi ya baadhi ya wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B (Dar es Salaam) yavunjwa

Hatimaye makazi ya baadhi ya wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B (Dar es Salaam) yavunjwa

Hapo kwa nyerere tu zamani kulikuwa na vijiji mzee alipotoka tu watu wakawahamisha kistyle

Ova
Walikuwa Wamiliki wa maeneo hayo na waliyauza kwa hiari yao; Hawa kuwa wavamizi kama Hawa wa Mbezi beach!
 
Kwani si walisema wanaleta mganga wao awafanyie zindiko wasibomolewe!
Vipi naye kachomoa betri?
Kuna mlinzi wa kiwanja cha mama Maria Nyerere huko Mbezi beach. Huyu bwana amejimilikisha sehemu hii na kujenga mabanda mengi na kuyapangisha bila ya kujenga vyoo hivyo wapangaji kutumia mifuko kujisaidia na kutupa vinyesi barabarani kitu ambacho ni hatari kwa afya ya wakazi!
Inasemekana nae anaamini kuwa waganga wa kienyeji ndio wamemfanya aendelee kuishi hapo kwa kuwapumbaza ukoo wa Nyerere wasahau kuhusu kiwanja hicho!
Huyu Mlinzi licha ya ushirikina huo, anavunja sheria kwa kukitumia hicho kiwanja tofauti na ilivyotarajiwa. Jina la Nyerere linanajisiwa kwa vitendo na biashara haramu vinavyofanyika pale ili hali mtoto wa mama Maria Makongoro ni kiongozi wa serikali anaetakiwa kuwa mfano wa kulinda sheria za nchi.
 
kwa hio wanahamishwa kwa sababu ya biashara haramu au kwa sababu ni eneo la hifadhi ya barabara ?

Mkunduguyangu wa Wilaya unanichanganya ujue ?
 
Yule mganga wao hajafua dafu......... Maana waliita mtaalam afanye mambo ili wasitolewe
Nawasikitikia sana watu. Kuna mahali Kibaha wanaenda kuloga usiku wa manane Tena watu wa maana eti mwenye Ardhi Asahau, serikali isahau na wananuiza eti Kwa nguvu za kafara Sheria isichukue mkondo wake.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ukisimuliwa na ukawaona hao watu utasema wanasingiziwa. Ila ndio ukweli tulionao.. mtu anauziwa Miguu ishiri kwa ishirini laki Tano halafu anailogea mwa Milioni mbili kwa miaka miwili.. ukistaajabu ya Musa utayaona ya watanzania, waganga na wenyeviti wa mitaa..

Ujinga ni glaukoma kwa Tanzania yetu bado unatutafuna taratibu ila kwa hakika.
 
Back
Top Bottom