HATIMAYE: Mazda CX-5 imeingia Top 5 ya gari zinazoingizwa Tanzania kutoka Japan

HATIMAYE: Mazda CX-5 imeingia Top 5 ya gari zinazoingizwa Tanzania kutoka Japan

Mazda za SA hazina huo mfumo wa DPF na sio sumbufu na sio mazda tu gari zao nyingi hata Subaru ya SA ipo tofauti na Japan kwa usumbufu ingawaje parts zinaweza kuingiliana...
Pia hizo Mazda CX -5 hata SA zilikua kwenye demand kubwa sana miaka miwili iliyopita na CX -3 na kabla ya hiyo ilikuwepo Hyundai Tucsson...
Mimi SA naangalia mwaka tu na mileage ili nipate gari ambayo haijatumika sana na niweze kulipa kodi Tanzania kama haina uchakavu wa muda mrefu wao gari za 2004,2005,2006 na miaka ya nyuma zaidi nyingi zikipata ajali hata kama sio mbaya sana wanaziweka kwenye code 3 kwa maana ukiinunua ukairekebisha hutakiwi kuuza ila code 2 ndio unaweza kununua na kuuza wakati Tanzania mtu anaagiza gari imempita Umri au yupo nayo sawa hiyo lazima isumbue sasa gari ya mwaka 2000 labda uagize tractor ndio itakua sawa sio SUV...
Asante sana kwa feedback nzuri, ngoja tusubiri hio Mazda CX-5 ulioagiza toka SA ili utupe breakdown ya cost zote including kodi ya TRA. Maana kwa vyovyote Mazda za kutoka huko zitakuwa poa sana and reliable
 
Asante sana kwa feedback nzuri, ngoja tusubiri hio Mazda CX-5 ulioagiza toka SA ili utupe breakdown ya cost zote including kodi ya TRA. Maana kwa vyovyote Mazda za kutoka huko zitakuwa poa sana and reliable
Mazda za SA kodi yake ni Tsh 10m mpaka 17m kwa matoleo ya 2020 nadhani na pia madza ipo kwenye kundi la Nissan na Ford kodi zake ni rafiki kama utapata gari ambayo haina uchakavu ni tofauti na Toyota upate ya mwaka huo huo kodi naona zimetofautiana karibu mara mbili au tatu zaidi ukiweza nunua gari bei kubwa harafu liwe na uchakavu kidogo au lisiwe na uchakavu kabisa la kuanzia 2017 kuendelea ili upate punguzo la kodi kwenye haya magari niliyoyataja mfano Ford ranger DC ya 2013 kodi ya ni kubwa kuliko Ford Ranger DC ya 2917 kila kitu kiwe sawa...
 
𝙻𝚘𝚘𝚔𝚒𝚗𝚐 𝚝𝚘 𝚐𝚎𝚝 2018 𝚂𝚄𝙱𝙰𝚁𝚄 𝙵𝙾𝚁𝙴𝚂𝚃𝙴𝚁 𝚇𝚃
That's 5th gen.
1280px-2019_Subaru_Forester_2.5i_Premium,_front_10.6.19.jpg
1280px-2019_Subaru_Forester_2.5i_Premium,_rear_10.6.19.jpg
1280px-Subaru_FORESTER_Premium_(5BA-SK9)_interior.jpg
 
Kuna kipindi JF ukisema nataka kununua gari kila mtu anakuambia Carina Ti
Hiyo ilikuwa kipindi kile namba za usajili zinakaa miaka 6 hazijabdalika, hiki kipindi cha kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake kila kukicha namba Mpya, za Serikali zenyewe zimefika STN na bado uchaguzi huu hapa jirani, maokoto yatakuwa nje nje!
 
Karibuni telegram group la Mazda CX-5 ili upate maarifa na uelewa juu kutoka Kwa wamiliki wa hapa bongo
 
Hizi gari zina shida gsni?

Mengi ya haya magari yakiingizwa nchini wamiliki wanayapeleka gereji na ukipata kwenye highway unaweza kukutana nazo baadhi wamepaki pembeni wamefungua boneti.
 
Hizi gari zina shida gsni?

Mengi ya haya magari yakiingizwa nchini wamiliki wanayapeleka gereji na ukipata kwenye highway unaweza kukutana nazo baadhi wamepaki pembeni wamefungua boneti.
Nadhani, kwa kusikia na kusoma, Shida ya hizi gari ni cooling system (coolant bypass na mara nyingine, radiator cap). Sambamba na hilo issue ya DPF ambayo nayo hufikia hadi kuharibu cylinder head na turbo. Inataka service kwa wakati na mafuta masafi kama ilivyo modern diesels nyingi. Vingine kabda itakuwa ni matatizo ya kawaida.
Kwa engine, ya Prtrol ni reliable zaidi ila ziko chache na perfomance (power/fuel consumption ratio) si nzuri sana kama ya diesel.
 
Back
Top Bottom