Hatimaye Mods nao kuanza kutekeleza kauli ya Pinda

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,357
Pamoja na FaizaFoxy kusamehewa kutoka kwenye kifungo kinachosemekana kuwa kilikuwa cha maisha, taarifa zilizoko juu ya meza yangu ni kwamba Mods nao wataanza kutekeleza kauli ya Pinda.

Jana nilimtumia Mkuu wa Mamods PM kutaka kujua kama JF ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani ya members, nijue chanzo halisi cha vurugu zinazozoendelea kule Jukwaa la Siasa na matatizo haya na jinsi gani Mods wanavyoyashughulikia kwa sababu yapo malalamiko kutoka kwa baadhi ya Members kuwa wanapigwa ban na Mods.

Mod Mkuu amenijibu na naomba kumnukuu: "Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona members fulani anasema eti Mods wanawapa ban members wa JF. Ukitumia lugha chafu, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa ban tuu...hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba JF tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.

"Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi Mods watakupiga ban tuu.... Mimi nasema Mods wawapige ban tuu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka."

Aidha Mod Mkuu amesema JF imedhamiria kurejesha matumizi ya lugha safi likiwamo Jukwaa la ChiChat na kuwataka WanaJF wawachie Mods wafanye kazi hiyo. Amesema JF ina orodha ya Members wanaosemekana kuwa ni vyanzo vya lugha chafu na matatizo yanayotokea Jukwaa la Siasa na kushangaa wale wanaopinga kupewa ban kwao.

"Lazima tuwapige ban na kama katika kuwapiga ban watafanya jeuri, jeuri, watapigwa ban tuu kabla ya kupelekwa kunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda. Nami nasema Mods wajipange imara wahakikishe wanadhibiti hali hii," alimalizia PM yake Mod Mkuu.

WanaChitchat waja juu

Akizungumzia PM hiyo, Arushaone alisema: "Kauli ya Mod Mkuu inakiuka sheria za JF na imethibitisha kwamba matumizi mabaya ya Mods na kusababisha bans kwa Members yana baraka za JF."

Alisema kauli ya Mod Mkuu kama ilivyokuwa ya Paw hapo awali zinatoa mwelekeo kwamba bans zonazotembea Jukwaa la ChiChat zina baraka za JF.

Vibabu na Vibibi vya Chitchat vyakerwa

Babu Asprin aka ODM alisema Mod Mkuu hakustahili kabisa kutoa kauli kama hiyo. Alisema Mod Mkuu hapaswi kuwa na jazba, bali anatakiwa kuwa na busara na kuzungumza kwa kuzingatia sheria za JF badala ya kutoa matamshi ambayo siyo mwafaka kwa JF inayoongozwa kwa kufuata sheria na taratibu.

Nae Fixed Point amesema kauli hiyo ya Mod Mkuu, mbali ya kwenda kinyume cha sheria za JF, inaweza kuhatarisha amani. Amesema matumizi ya ban kupita kiasi kudhibiti hali yoyote korofi hayaruhusiwi.

Baada ya kutoka jela ambako alikuwa anatumikia kifungo chake FaizaFoxy aliulizwa na nngu007 mbona yuko kimya akamjibu:
Low profile!

Hata hivyo, nilipomwuliza anajisikiaje kutoka kifungoni na kama ni kifungo hicho au ni kauli ya Mod Mkuu imemfanya kuwa na "low profile" alichefuka na kunijibu:

Hawa mods wabaya sana wakanipachika jina "JF Ban 1", sijui walilitolea wapi, badala ya kumpa hilo jina @Malaria Sugu wakanipachika mimi. Wananshangaza!
 
EMT najuwa ulinitetea sana nilipokuwa banned. Ahsante kwa hilo, napenda kuwaombea wafungwa wenzangu wote waachiwe huru kama nilivyoachiwa mimi. Ikiwa hata wahaini wa kweli wanaachiwa magerezani na Serikali kwa misaha mbali mbali nadhani itakuwa ni busara kubwa Rais wa JF akisita kundelea kuwanyanyasa wale wanaoifanya JF iwe JF na kuwapa msamaha na kuwawachia huru kama nilivyoachiwa mimi. Nawatakia wote Ramadhan njema.
 
Last edited by a moderator:

Uanzishe thread kutueleza jinsi kulivyo huko jela na pia maoni ya wafungwa wengine.
 
FaizaFoxy ulipotea shosti...... Karibu tena....ramadhani njema
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy back in action waaaaaaaaoooo!!!!!! huwa siachi kukunukuu "unanchekesha"....sasa je moto ni ule ule ? ( source: jide aka anaconda aka binti machozi).
 
Last edited by a moderator:
Welcome back FaizaFoxy...this time uwe mpole ili tusikukose tena bhana! Afu jamaa yangu Crashwise yuko single kama wewe, tafadhali wasilianeni kwani you'll make a great couple.
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…