Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.
Sasa haya maswali mnapoyauliza hapa kwenye mtandao mnategemea nani awajibu. Kama kweli kuna maswali kwa nini wasiulizwe hao mnaofikiri kuwa wamehusika.

Mimi siamini kuwa CCM wamemuua Balali, yeye amekufa kama vile binadamu wote hapa tutakavyokua siku moja. Kuanza kuleta habari za uongo kama Mushi alizoleta hapa jana kuwa Balali amebadilisha majina na kuanza kuwasiliana na watu wengine ni uzushi usioweza kuvumiliwa.
Hivi wewe nani kasema CCM wamemuua?mimi nafikiri Jmushi alileta zile habari za jana kutaka kujua ukweli u wapi kuhusu majina hayo mawili.sasa hapa CCM inaingiaje?wewe mbona una ubaguzi wa kichama?wengine sio wanachama wa chama chochote hapa?kama wewe ni CCM mimi kwa mfano sina chama.
 
Na kwa wale wanaojidanganya kuwa FBI hawatakuja kutoa taarifa za ukweli siku moja..Then waendelee na ndoto zao!
Unless ni kweli amekufa!Na ukweli wa mazingira ya kifo kuwekwa bayana!
Narudia...Ni bora watoe ushirikiano ili tumwache Ballali alale pema peponi kama wanavyotaka!

Watoe ushirikiano kwa nani? Umejaa vitisho vya bure tu hapa wakati hakuna chochote unachofanya zaidi ya makelele tu. Kwani FBI watachunguza hii case kama nani?

Balali alikuwa mgonjwa na amekufa, wewe umeanza kuja hapa na mambo ya uongo kuwa amebadili majina na kuanza kuharibia watu wengine na chama cha mapinduzi sifa kuwa wanaficha kitu hapa.

kama wewe unajua kilichotokea na una ushahidi kwa nini usiuweke hapa?
 
Kuna kifo chenye utata kisichochunguzwa hapa marekani kama wananchi wakitaka?
Halafu itageuka kuwa vita kati ya wananchi na familia ya Ballali na ndio maana nasema ni heri waweke mambo wazi sasa hivi!
 
Hivi wewe nani kasema CCM wamemuua?mimi nafikiri Jmushi alileta zile habari za jana kutaka kujua ukweli u wapi kuhusu majina hayo mawili.sasa hapa CCM inaingiaje?wewe mbona una ubaguzi wa kichama?wengine sio wanachama wa chama chochote hapa?kama wewe ni CCM mimi kwa mfano sina chama.

Yeye ndiye alileta habari za uongo hapa na kudai kuwa ni za kweli. Kama huu ndio utendaji kazi wake, basi ni uzembe mkubwa kabisa. Amekaa kusema kuwa ccm na serikali inahusika kwenye kifo cha Ballali. Ushahidi uko wapi?

Huu uzushi unaaibisha hii forum. Watu wanakuja tu na mambo ya ajabu ajabu na kujaza pages za JF bila kuwa na ushahidi. kama kuna ushahidi kuwa Ballali hajafa uwekwe hapa. kama kuna ushahidi kuwa serikali na ccm wamehusika kwenye kifo hiki uwekwe hapa.

Haya mengine yote ni kuchafuana tu kisiasa bila mpango wowote.
 
Kuna kifo chenye utata kisichochunguzwa hapa marekani kama wananchi wakitaka?
Halafu itageuka kuwa vita kati ya wananchi na familia ya Ballai na ndio maana nasema ni heri waweke mambo wazi sasa hivi!

Umewauliza FBI na wakasema kuwa wanachunguza? Kuna utata gani kwenye kifo cha Ballali? Ballali aliondoka Tanzania akiwa mzima na akaongoe na watu wa media kuwa yeye si fisadi.

Kama magonjwa yamemkuta akiwa Marekani, basi wewe ni nani kupingana na hali ya maisha. Utata uko wapi hapa?
 
Hata kama alikufa akiwa huru...Halafu tukagundua kuwa hakutakiwa kuwa huru...Then tuna haki ya kuhoji utata wa kifo chake based on mazingira..Mazingira ambayo alikufa ghafla wakati akianza kudhaniwa kuwa hatakuwa mtu huru tena!?
Kwanini afe ghafla wakati alikuwa ameshaanza kuelekea kuupoteza uhuru wake?
Wananchi wa dunia huru wenye kufikiria ki uhuru hawana kesi hapo kweli?
 
Hata kama alikufa akiwa huru...Halafu tukagundua kuwa hakutakiwa kuwa huru...Then tuna haki ya kuhoji utata wa kifo chake based on mazingira..Mazingira ambayo alikufa ghafla wakati akianza kudhaniwa kuwa hatakuwa mtu huru tena!?

Sasa kama unahoji hapa, unategemea nani akupatie majibu hapa?
 
Yeye ndiye alileta habari za uongo hapa na kudai kuwa ni za kweli. Kama huu ndio utendaji kazi wake, basi ni uzembe mkubwa kabisa. Amekaa kusema kuwa ccm na serikali inahusika kwenye kifo cha Ballali. Ushahidi uko wapi?

Huu uzushi unaaibisha hii forum. Watu wanakuja tu na mambo ya ajabu ajabu na kujaza pages za JF bila kuwa na ushahidi. kama kuna ushahidi kuwa Ballali hajafa uwekwe hapa. kama kuna ushahidi kuwa serikali na ccm wamehusika kwenye kifo hiki uwekwe hapa.

Haya mengine yote ni kuchafuana tu kisiasa bila mpango wowote.

Sidhani kama forum inaaibishwa. Nafikiri ku-quotiwa kwa JF kwenye magazeti ya leo hii kutasaidia zaidi kuitangaza JF. Come back a week from today and uangalie wanachama wangapi wapya watakuwa wamejiunga na JF. Then na wewe anzisha forum yako halafu utu-direct huko, then uone kwa itikadi zako uta-attract watu wangapi. No offense intended!!!!!
 
Marehemu alikuwa na Green Card, serikali ya US ilimnyanga'anya viza ya u-Governor aliyokuwa amepewa kama ofisa wa serikali yetu kuweza kuingia na kutoka US, lakini otherwise hata serikali yetu haikujua kuwa marehemu alikuwa na green card, ndio kikawa chanzo cha kujichanganya kwa serikali yetu na exactly what serikali ya US ilikifanya,

Serikali ya US isingeweza kumrudisha marehemu bongo, unless kama tunayo mahusiano ya namna hiyo kisheria, halafu pia serikali yetu haikuwahi kutamka wazi kuwa marehemu alikuwa mtuhumiwa anayetafutwa kisheria,

according to the dataz ni kwamba mjane yuko na hasira sana na serikali yetu ambayo anaijua vizuri sana kuhusu ukweli wa ishu nzima, sasa tusubiri mazishi yaishe, ninajua kuna mengi yanakuja, ambayo ni mazuri kwa taifa letu!

nimeshindwa maneno ya kuandika kuhusiana na hili ! ulichosema ni SIMPLY IMPOSSIBLE ! kazi za ugavana hapewi mtu yoyote tu yule bila ya uchunguzi ! either serikali ilijua au you made a mistake in your info ! sio kweli ! serikali has to know wanayempa kazi !
 
Nawauliza nyie kina Masaka...Kwanini afe wakati anaanza kutafutwa?
Alitaka kufa huru ili ushahidi wake usitumike?
Ama aliuwawa kwa sababu hiyo hiyo?
Utata hakuna hapo wana jf?
 
Sidhani kama forum inaaibishwa. Nafikiri ku-quotiwa kwa JF kwenye magazeti ya leo hii kutasaidia zaidi kuitangaza JF. Come back a week from today and uangalie wanachama wangapi wapya watakuwa wamejiunga na JF. Then na wewe anzisha forum yako halafu utu-direct huko, then uone kwa itikadi zako uta-attract watu wangapi. No offense intended!!!!!

Sio kwamba nataka watu wawe na ufuasi wa ccm peke yake, kuihusisha ccm na serikali kwenye huu msiba bila kuwa na uthibitisho ni makosa makubwa sana na sidhani kama inabidi yavumiliwe.

CCM haihusiki na kifo cha Ballali kwa hiyo watu waache kuhiusisha na kifo hiki. Ballali aliugua na sasa amekufa na kuzikwa. Wale wanaopinga waseme tu ni kwa nini wanapinga na walete uthibitisho wa maneno yao.
 
Nawauliza nyie kina Masaka...Kwanini afe wakati anaanza kutafutwa?Alitaka kufa huru ili ushahidi wake usitumike?
Ama aliuwawa kwa sababu hiyo hiyo?
Utata hakuna hapo wana jf?

Kwani kuna mtu anajua siku yake ya kufa? Wewe unajua utakufa lini? Hakuna mtu mwenye uamuzi wa lini afe. Katika hili bado hakuna logic kwenye swali lako.
 
Either Aliuwawa Ili Ushahidi Usitumike
Ama Ni Mpango Wa Zamani Kuanzia Serikali Ya Mkapa kwa makubaliano yao na Ballali.. Wakamleta Kufanya Uharamia Wakijua Atakufa Kwa Kansa Na Hivyo Familia Yake Itapata Manufaa.Hii posibility ipo kwasababu jama labda alikuwa keshaambiwa kuwa ngoma ntolee baada ya mika 7 na akala dili na mfisadi wa nchi yetu walipomtoa huko IMF na kumweka BOT ambapo waliiuza nchi huku wakijua kuwa ushahidi utakufa baada ya miaka hiyo 7!
Ama Ni Kweli Ame Fake Kifo Chake Na Serikali Haijui
Ama Amafake Kifo Chake Na Serikali Imeshiriki
Ama Ni Kweli Aliwekewa Sumu Wakati Akiwa Wamesha Mset Up Na Mapesa Kutoka!
Tatizo Hapo Ni Kwanini Familia Haijasema Ukweli Wa Kila Kitu!
Sasa Hayo Hapo Juu Hakuna Kesi Hapa Ya Kupelekeshana?
 
Either Aliuwawa Ili Ushahidi Usitumike
Ama Ni Mpango Wa Zamani Kuanzia Serikali Ya Mkapa Wakamleta Kufanya Uharamia Wakijua Atakufa Kwa Kansa Na Hivyo Familia Yake Itapata Manufaa
Ama Ni Kweli Ame Fake Kifo Chake Na Serikali Haijui
Ama Amafake Kifo Chake Na Serikali Imeshiriki
Ama Ni Kweli Aliwekewa Sumu Wakati Akiwa Wamesha Mset Up Na Mapesa Kutoka!
Tatizo Hapo Ni Kwanini Familia Haijasema Ukweli Wa Kila Kitu!
Sasa Hayo Hapo Juu Hakuna Kesi Hapa Ya Kupelekeshana?

hata kama hayo uliyosema ni ya kweli (mimi sioni kama kuna ukweli wowote), je hapa JF kupiga makelele usiku na mchana na kuleta habari za uongo kama zile ulizoleta jana ndio njia sahihi. Kwa nini unataka kuchafua watu na serikali yako bila sababu?
 
Sio kwamba nataka watu wawe na ufuasi wa ccm peke yake, kuihusisha ccm na serikali kwenye huu msiba bila kuwa na uthibitisho ni makosa makubwa sana na sidhani kama inabidi yavumiliwe.

CCM haihusiki na kifo cha Ballali kwa hiyo watu waache kuhiusisha na kifo hiki. Ballali aliugua na sasa amekufa na kuzikwa. Wale wanaopinga waseme tu ni kwa nini wanapinga na walete uthibitisho wa maneno yao
.

babu tushawazoea hao ! lets take it as they go !
 
Either Aliuwawa Ili Ushahidi Usitumike
Ama Ni Mpango Wa Zamani Kuanzia Serikali Ya Mkapa Wakamleta Kufanya Uharamia Wakijua Atakufa Kwa Kansa Na Hivyo Familia Yake Itapata Manufaa.Hii posibility ipo kwasababu jama labda alikuwa keshaambiwa kuwa ngoma ntolee baada ya mika 7 na akala dili na mfisadi wa nchi yetu walipomtoa huko IMF na kumweka BOT ambapo waliiuza nchi huku wakijua kuwa ushahidi utakufa baada ya miaka hiyo 7!
Ama Ni Kweli Ame Fake Kifo Chake Na Serikali Haijui
Ama Amafake Kifo Chake Na Serikali Imeshiriki
Ama Ni Kweli Aliwekewa Sumu Wakati Akiwa Wamesha Mset Up Na Mapesa Kutoka!
Tatizo Hapo Ni Kwanini Familia Haijasema Ukweli Wa Kila Kitu!
Sasa Hayo Hapo Juu Hakuna Kesi Hapa Ya Kupelekeshana?

mkuu unakuwa willy gamba wa JF

kunywa maji kwanza halafu vuta subira maandishi yako ni kumbu kumbu sasa kuwa mvumilivu.

wakati ndio wenye maamuzi si kila kitu kinakuja kwa dakika moja

nasaha zangu kwako maana umekuwa na pupa ya kutupa
 
Kuna mtu anayejua kama habari za kansa ni za kweli?
 
Sio kwamba nataka watu wawe na ufuasi wa ccm peke yake, kuihusisha ccm na serikali kwenye huu msiba bila kuwa na uthibitisho ni makosa makubwa sana na sidhani kama inabidi yavumiliwe.

CCM haihusiki na kifo cha Ballali kwa hiyo watu waache kuhiusisha na kifo hiki. Ballali aliugua na sasa amekufa na kuzikwa. Wale wanaopinga waseme tu ni kwa nini wanapinga na walete uthibitisho wa maneno yao.

siku zote kuna watu hupenda udaku na kupenda mambo yaende au watu waamini wanavyotaka wao

hawana nafasi ya kujiuliza au kufanya tathmini ni watu wa ovyo sana

hata rafiki yangu mkjj amewan'gamua maana wao wanataka kila mtu awe na mawazo yao kwa sasa mkjj anaonekana msaliti
 
Hizi ni assumptions ambazo niko entittled to provided mtuhumiwa aliekufa akiwa huru ndiye aliyekuwa mtuhumiwa namba moja kwenye sakata lote la EPA!
We kwanini unafikiri wamarekani wamekomalia kwenye utolewaji wa ripoti badala ya wapi alipo Ballali?
Wanataka kuuona ukweli ambao haukuhusisha kumuhoji suspect number one!
Na sisi tunataka tuione hiyo ripoti ya uchunguzi ambayo haikumuhoji mtuhumiwa namba moja na wala haikumtafuta mtuhumiwa namba moja!Bali walisubiri mpaka afe akiwa huru ndio watangaze kuwa anahitajika!
Na kama kwenye ripoti watadai kumuhoji..Then tunataka tuelewe ni lini na wapi!
 
mkuu unakuwa willy gamba wa JF

kunywa maji kwanza halafu vuta subira maandishi yako ni kumbu kumbu sasa kuwa mvumilivu.

wakati ndio wenye maamuzi si kila kitu kinakuja kwa dakika moja

nasaha zangu kwako maana umekuwa na pupa ya kutupa

Tatizo lake analazimisha mambo hadi anajikuta akileta habari za uongo mtupu hapa JF. Kuna watu wanalaumu wana ccm kuwa wanaharibu JF lakini naona kuwa wapinzani ndio wanataka kuharibu huu mtandao.

Yaani habari za uzushi na uongo mkubwa ili kuipaka serikali na ccm matope bila kuwa na uthibitisho wowote ule. Yeye atulie kidogo na afanye uchunguzi na akishapata ushahidi aje hapa kuutoa kama vile wengine wengi wanafanya hapa.

Si vibaya kutokuamini kuwa Ballali amekufa, lakini kutaka kuhusisha kifo cha Ballali na ccm au serikali bila ushahidi ni makosa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom