Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.
Hivi wewe nani kasema CCM wamemuua?mimi nafikiri Jmushi alileta zile habari za jana kutaka kujua ukweli u wapi kuhusu majina hayo mawili.sasa hapa CCM inaingiaje?wewe mbona una ubaguzi wa kichama?wengine sio wanachama wa chama chochote hapa?kama wewe ni CCM mimi kwa mfano sina chama.
 

Watoe ushirikiano kwa nani? Umejaa vitisho vya bure tu hapa wakati hakuna chochote unachofanya zaidi ya makelele tu. Kwani FBI watachunguza hii case kama nani?

Balali alikuwa mgonjwa na amekufa, wewe umeanza kuja hapa na mambo ya uongo kuwa amebadili majina na kuanza kuharibia watu wengine na chama cha mapinduzi sifa kuwa wanaficha kitu hapa.

kama wewe unajua kilichotokea na una ushahidi kwa nini usiuweke hapa?
 

Kuna kifo chenye utata kisichochunguzwa hapa marekani kama wananchi wakitaka?
Halafu itageuka kuwa vita kati ya wananchi na familia ya Ballali na ndio maana nasema ni heri waweke mambo wazi sasa hivi!
 

Yeye ndiye alileta habari za uongo hapa na kudai kuwa ni za kweli. Kama huu ndio utendaji kazi wake, basi ni uzembe mkubwa kabisa. Amekaa kusema kuwa ccm na serikali inahusika kwenye kifo cha Ballali. Ushahidi uko wapi?

Huu uzushi unaaibisha hii forum. Watu wanakuja tu na mambo ya ajabu ajabu na kujaza pages za JF bila kuwa na ushahidi. kama kuna ushahidi kuwa Ballali hajafa uwekwe hapa. kama kuna ushahidi kuwa serikali na ccm wamehusika kwenye kifo hiki uwekwe hapa.

Haya mengine yote ni kuchafuana tu kisiasa bila mpango wowote.
 
Kuna kifo chenye utata kisichochunguzwa hapa marekani kama wananchi wakitaka?
Halafu itageuka kuwa vita kati ya wananchi na familia ya Ballai na ndio maana nasema ni heri waweke mambo wazi sasa hivi!

Umewauliza FBI na wakasema kuwa wanachunguza? Kuna utata gani kwenye kifo cha Ballali? Ballali aliondoka Tanzania akiwa mzima na akaongoe na watu wa media kuwa yeye si fisadi.

Kama magonjwa yamemkuta akiwa Marekani, basi wewe ni nani kupingana na hali ya maisha. Utata uko wapi hapa?
 
Hata kama alikufa akiwa huru...Halafu tukagundua kuwa hakutakiwa kuwa huru...Then tuna haki ya kuhoji utata wa kifo chake based on mazingira..Mazingira ambayo alikufa ghafla wakati akianza kudhaniwa kuwa hatakuwa mtu huru tena!?
Kwanini afe ghafla wakati alikuwa ameshaanza kuelekea kuupoteza uhuru wake?
Wananchi wa dunia huru wenye kufikiria ki uhuru hawana kesi hapo kweli?
 
Hata kama alikufa akiwa huru...Halafu tukagundua kuwa hakutakiwa kuwa huru...Then tuna haki ya kuhoji utata wa kifo chake based on mazingira..Mazingira ambayo alikufa ghafla wakati akianza kudhaniwa kuwa hatakuwa mtu huru tena!?

Sasa kama unahoji hapa, unategemea nani akupatie majibu hapa?
 

Sidhani kama forum inaaibishwa. Nafikiri ku-quotiwa kwa JF kwenye magazeti ya leo hii kutasaidia zaidi kuitangaza JF. Come back a week from today and uangalie wanachama wangapi wapya watakuwa wamejiunga na JF. Then na wewe anzisha forum yako halafu utu-direct huko, then uone kwa itikadi zako uta-attract watu wangapi. No offense intended!!!!!
 

nimeshindwa maneno ya kuandika kuhusiana na hili ! ulichosema ni SIMPLY IMPOSSIBLE ! kazi za ugavana hapewi mtu yoyote tu yule bila ya uchunguzi ! either serikali ilijua au you made a mistake in your info ! sio kweli ! serikali has to know wanayempa kazi !
 
Nawauliza nyie kina Masaka...Kwanini afe wakati anaanza kutafutwa?
Alitaka kufa huru ili ushahidi wake usitumike?
Ama aliuwawa kwa sababu hiyo hiyo?
Utata hakuna hapo wana jf?
 

Sio kwamba nataka watu wawe na ufuasi wa ccm peke yake, kuihusisha ccm na serikali kwenye huu msiba bila kuwa na uthibitisho ni makosa makubwa sana na sidhani kama inabidi yavumiliwe.

CCM haihusiki na kifo cha Ballali kwa hiyo watu waache kuhiusisha na kifo hiki. Ballali aliugua na sasa amekufa na kuzikwa. Wale wanaopinga waseme tu ni kwa nini wanapinga na walete uthibitisho wa maneno yao.
 
Nawauliza nyie kina Masaka...Kwanini afe wakati anaanza kutafutwa?Alitaka kufa huru ili ushahidi wake usitumike?
Ama aliuwawa kwa sababu hiyo hiyo?
Utata hakuna hapo wana jf?

Kwani kuna mtu anajua siku yake ya kufa? Wewe unajua utakufa lini? Hakuna mtu mwenye uamuzi wa lini afe. Katika hili bado hakuna logic kwenye swali lako.
 
Either Aliuwawa Ili Ushahidi Usitumike
Ama Ni Mpango Wa Zamani Kuanzia Serikali Ya Mkapa kwa makubaliano yao na Ballali.. Wakamleta Kufanya Uharamia Wakijua Atakufa Kwa Kansa Na Hivyo Familia Yake Itapata Manufaa.Hii posibility ipo kwasababu jama labda alikuwa keshaambiwa kuwa ngoma ntolee baada ya mika 7 na akala dili na mfisadi wa nchi yetu walipomtoa huko IMF na kumweka BOT ambapo waliiuza nchi huku wakijua kuwa ushahidi utakufa baada ya miaka hiyo 7!
Ama Ni Kweli Ame Fake Kifo Chake Na Serikali Haijui
Ama Amafake Kifo Chake Na Serikali Imeshiriki
Ama Ni Kweli Aliwekewa Sumu Wakati Akiwa Wamesha Mset Up Na Mapesa Kutoka!
Tatizo Hapo Ni Kwanini Familia Haijasema Ukweli Wa Kila Kitu!
Sasa Hayo Hapo Juu Hakuna Kesi Hapa Ya Kupelekeshana?
 

hata kama hayo uliyosema ni ya kweli (mimi sioni kama kuna ukweli wowote), je hapa JF kupiga makelele usiku na mchana na kuleta habari za uongo kama zile ulizoleta jana ndio njia sahihi. Kwa nini unataka kuchafua watu na serikali yako bila sababu?
 

babu tushawazoea hao ! lets take it as they go !
 

mkuu unakuwa willy gamba wa JF

kunywa maji kwanza halafu vuta subira maandishi yako ni kumbu kumbu sasa kuwa mvumilivu.

wakati ndio wenye maamuzi si kila kitu kinakuja kwa dakika moja

nasaha zangu kwako maana umekuwa na pupa ya kutupa
 
Kuna mtu anayejua kama habari za kansa ni za kweli?
 

siku zote kuna watu hupenda udaku na kupenda mambo yaende au watu waamini wanavyotaka wao


hawana nafasi ya kujiuliza au kufanya tathmini ni watu wa ovyo sana

hata rafiki yangu mkjj amewan'gamua maana wao wanataka kila mtu awe na mawazo yao kwa sasa mkjj anaonekana msaliti
 
Hizi ni assumptions ambazo niko entittled to provided mtuhumiwa aliekufa akiwa huru ndiye aliyekuwa mtuhumiwa namba moja kwenye sakata lote la EPA!
We kwanini unafikiri wamarekani wamekomalia kwenye utolewaji wa ripoti badala ya wapi alipo Ballali?
Wanataka kuuona ukweli ambao haukuhusisha kumuhoji suspect number one!
Na sisi tunataka tuione hiyo ripoti ya uchunguzi ambayo haikumuhoji mtuhumiwa namba moja na wala haikumtafuta mtuhumiwa namba moja!Bali walisubiri mpaka afe akiwa huru ndio watangaze kuwa anahitajika!
Na kama kwenye ripoti watadai kumuhoji..Then tunataka tuelewe ni lini na wapi!
 
mkuu unakuwa willy gamba wa JF

kunywa maji kwanza halafu vuta subira maandishi yako ni kumbu kumbu sasa kuwa mvumilivu.

wakati ndio wenye maamuzi si kila kitu kinakuja kwa dakika moja

nasaha zangu kwako maana umekuwa na pupa ya kutupa

Tatizo lake analazimisha mambo hadi anajikuta akileta habari za uongo mtupu hapa JF. Kuna watu wanalaumu wana ccm kuwa wanaharibu JF lakini naona kuwa wapinzani ndio wanataka kuharibu huu mtandao.

Yaani habari za uzushi na uongo mkubwa ili kuipaka serikali na ccm matope bila kuwa na uthibitisho wowote ule. Yeye atulie kidogo na afanye uchunguzi na akishapata ushahidi aje hapa kuutoa kama vile wengine wengi wanafanya hapa.

Si vibaya kutokuamini kuwa Ballali amekufa, lakini kutaka kuhusisha kifo cha Ballali na ccm au serikali bila ushahidi ni makosa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…