Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
Wakuu Amani iwe kwenu!!
Nimebahatika kusafiri Tena kusafiri kutoka kahama kwenda mpanda -katavi Kwa lengo la kuendelea kuangalia fursa za kilimo na ufugaji nk.
Na hapa nitakupisha maeneo yote tangu safari nilipoianza.
Safari niliianzia kahama katika stend ya Cdt kahama to mpanda nauli 30k
nilipanda gari ya Ally's mnano majira ya saa3:00 asbh safari ilianza rasmi.
Nikiwa nimebahatika kukaa na mkaka mtu mzima mwenyeji wa Tabora na hapo ndipo aliposhukia.
Basi safari ilianza saa3 asbh kutoka stend ya Cdt njia yote hiyo kutoka kahama Hadi Tinde ardhi isiyo na rutuba Huwa inashuhudiwa Kila na anayepita maeneo hayo.
Maeneo hayo yote Hadi nzega hakuna mvua ya maana iliyo nyesha japo watu wanalazimika kulima lakini kiukweli ukiona unaona kabisa ardhi inahitaji mvua hii.
Tumesafiri Hadi nakaribia Tabora mjini hapo ndo nikaanza kuona matumaini ya mvua na haliya hewa walau kuwa nzuri mazingira pia kuonyesha angalau ukijani .
Naam Tabora tulifika saa7 mchana. gari haikukaa sana tukaamsha.
Baada ya kutoka Tabora mji nadhani Hadi sehemu Moja panaitwa IPOLE (Wenyeji mtanikosoa maana sikupata kusoma vizuri vibao gari ilikuwa fire sana) hizi sehemu hapa kuwa pazuri pia.
Punde tuliingia porini kama kawaida hapa nitanena machache.
FURSA NILIYOIONA ( KWA SERIKALI) KWENYE PORI HILI.
Kwanza nikili wazi tunaongozwa na viongozi wasiokuwa na upeo (akili/maarifa) wa kutatua changamoto za wananchi hasa wasomi wetu hapa.
Kwa Elimu yangu ndogo nilipofika kwenye pori lile takribani tulitumia masaa2:40 gari ikiwa speed ukiunganisha na pori la Katavi basi weka masaa3 na ushehe maana niliona Kuna daraja ndo mpakani nikaona ubao umeandikwa karibu Katavi mji mkubwa uliofuata ni INYONGA.
Hilo pori niliona halina kitu zaidi ya mizinga ya nyuki michache sana Tena mingi imeanguka na zaidi ni ya kienyeji yaani ya magome ya miti.
Iwapo kama tungelikuwa na viongozi wenye maono na wenye huruma Kwa wadogo zetu hasa waliosoma ufugaji nyuki( BEE KEEPING)
Pale kama serikali ikiweza au kuweka mizinga milioni mbili tu Nina uhakika itatengeneza ajira zaidi ya vijana wenzetu zaidi ya 50,000/=
japo lile pori likiwekewa miundo mbinu hata mizinga zaidi ya m2 unaweza weka pale na Bado enelo likabaki
miundombinu ya kuweka mle ni maji na kupanda miti yenye maua mengi nadhani wataalamu wa hili manaijua.
ni ajabu sana hii Nchi hata kwenye Nchi kumi inayozalisha asali Kwa wingi Duniani haimo kitu ambacho ni maajabu sana.
imagine kama wenyeji Kwa Sasa wanaweka tu mizinga kienyeji bila kuweka miundombinu muhimu Kwa nyuki na Bado Tabora ni wazalishaji wakubwa wa asali vipi pakiboreshwa?
na tukumbuke mizinga mingi ni ya kienyeji na mara nyingi wanavuna mara1 tu Kwa mwaka.
Serikali inatumia Hela nyingi sana kununua ma V8 lakini vijana wenzetu hawana ajira V8 Moja inauwezo wa kutengeneza mizinga ya kisasa zaidi ya 2500!
Hii nimepigia Kwa Kila mzinga mmoja ugharimu Tsh 200,000/= V8 Moja nimeipa m500.
Hapo Bado serkali inaweza kupunguza gharama Kwa kuingia porini Kisha kuchana mbao mle mle na hizo hizo ndo zikatumika kutengeneza mizinga hiyo.
hapo Nina uhakika haitazidi gharama ya 70k Kwa Kila mzinga. Hao mafundi wapo wengi hata ukichukua wanafunzi wa veta wakawa wanafanya kazi ya kutengeneza hiyo mizinga unapunguza zaidi gharama.
Kumbuka Lita Moja ya asali mbichi tunauziwa 13000-15000 huku kahama.
Serikali unashindwa vipi basi kufanya haya? Nini faida ya kuwa na mahifadhi ya mistu yasikuwa na tija kubwa zaidi?
Kwani ufugaji nyuki utaharibu vipi hifadhi? kwani serkali haiwezi kutenga eneo sahihi Kwa ufugaji wa nyuki?
Nchi hii si Ina mapori mengi tu makubwa hasa? Cha ajabu asali ni anasa kwenye Nchi hii wapo watu kula asali Hadi aandikiwe au aambiwe dawa uliyooewa kachanganye na asali mbichi licha ya kuwa tunajua wazi asali inafaida kedekede.Naishia hapa unaweza kukosoa wazi hili au kuongezea nyama zaidi.
Tulivuka pori hili kubwa na hatimae tukaingia INYONGA Hali si nzuri kivile japo huwezi linganisha na kahama,nzega nk.
Tulipita stend hiyo si kubwa sana Wala haijachangamka kivile.
hapo niliona mafuta ya mawese na asali kidogo wanauza sikuuliza bei maana sikushuka.
Vilevile Kuna pori jingine hapa kati kubwa tu!!
kama nilivyosema haikuwa rahisi kusoma vibao Kwa sababu ya speed ya gari.
Hatimae tuliingia mpanda mji Kwa hakika kabla hujaufikia mji huo Hali inabadilika ghafla hii mito na mabonde unaanza kuona.
kilimo Cha mahindi kinaanza kuonekana haliyahewa nzuri nk
mnamo saa1:20 Tukaingia stend. Nilipokelewa na konda (msukuma) tukawa kama tumewahi fahamiana kabla Moja Kwa Moja alinipeleka sehemu ya kulala(lodge)
Tulipiga story kidogo na badae tukaenda kukata ticket Tena ya kwenda mwese na niliambiwa nitashukia KASILIPU.
Baada ya kukata ticket nilienda kula mgahawani Nje tu na geti la kuingilia abiria nilikula hapo Kwa mara ya kwanza samaki aina ya migebuka.
Kesho yake kama ilivyoada niliamka nikajiweka sawa kwanza nikamch
eki yule konda kumuaga akaniambia yeye Bado amelala ....hivyo nikaenda stend ya zamani.
Kwa vile gari ilikuwa inaondoka saa3 asubuhi Mimi nilifika saa1 tu nikiwa na maana nipate muda walau wa kuzunguka mjini na kusoma mazingira zaidi!
Nilimuita boda mmoja nikamkaribisha supu na chapati huku akinipa ABC Kisha nikamuomba anipeleke maeneo maarufu ya hapo mjini
Moja ya eneo maarufu tulienda Mpanda Hotel na kwingineko na hata Kilima hewa.
Pia nilifika sokoni kufanya research ya mazao japo ilikuwa asubhi Bado sikupata kile nilichokuwa nakihitaji zaidi hasa Kwa upande wa nafaka.
Baada ya kutembea hapa na pale na humo hatimae nilienda kupanda gari na safari ilianza saa3:7
ukweli ni kwamba Mpanda Ina milima kama morogoro tu utofauti wake ni wingi wa hiyo milima.
Hatimae nilifika pale nilipoambiwa nishukie na nikamkuta mwenyeji wangu.
Changamoto kubwa ni mtandao wa Voda haushiki kabisa hata kidogo hivyo ukiamua kujitungua sajiri halotel na Yas ndo zinafanya vizuri kule.
Safari ilianza kuingia porini ni chaka to Chaka milima na mabonde.
Kuna sehemu unafika mnashuka kwenye pikipiki mnatembea kwanza.
tulienda Kwa mwendo wa lisaa1 ndo tukafika Kwa mwenyeji wangu
Aisee huku Kuna mabonde Bado Yako bikira kabisa Yana rutuba ya kutosha.
Mfano Angalia udongo huu ulivyo
changamoto kubwa hasa ni milima Kuna milima hatari
kitu kingine usafirishaji ni Kwa bodaboda tu japo hakuna mzigo ambao hautasombwa.
Maeneo hayo ni mzuri sana Kwa kilimo na kama ukihitaji kilimo Cha umwagiliaji hakuna kumwagilia.
Wenyeji wake hulima maharage kiangazi lakini kamwe hawamwagilii zao lolote humwagilii Kwa sababu ardhi inasapot unyevu muda wote!
Kwa upande wa ufugaji ni wewe na mtaji wako tu maeneo ni makubwa ajabu nyasi za kutosha na maji ya kutosha.
Unaweza Fuga ng'ombe, mbuzi,kondoo kuku na Bata Kwa uhuru wote bila kero yoyote kule hata kama wakiwa huria au nusu huria!
Kuna mbuzi mbegu kubwa mfano wa Boer goat!hii unaweza kataa.
Huyu mbuzi Hana mwaka
Kule mashamba hawauzi Kwa heka nikukatiana eneo mnaelewana basi.
Kumbuka nilifikia Kwa wasukuma wale wa kizamani kabisa kulala ni changamoto nyingine hapo walinirudisha nyuma miaka 27 iliyopita ndo nakumbuka ilikuwa mara yangu ya mwisho kulalia ngozi ya ng'ombe.
Huyu mwenyeji wangu wanang'ombe zaidi ya 170 kondoo na mbuzi zaidi ya 300 lakini Bado wanalala namna
hiyo
japo hii sio shida zangu tulikula vizuri na kulala na mapema tukaanza kutembea kuelekea barabarani palikuwa panaitwa mwese no2 tulitumia masaa2 na ushee hapo ni Kwa mguu ni milima Kwa milim
a hatimae tulifika na bahati nzuri nikapata gari.
Hayo ni Kwa uchache kati ya niliyoyaona na kujifunza.
PIA SOMA Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji