Hatimaye nimekuwa baba. Ni raha iliyoje na mimi kuwa baba wa mtu

Hatimaye nimekuwa baba. Ni raha iliyoje na mimi kuwa baba wa mtu

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Mwezi December 2021 nilileta hii mada hapa kwamba natarajia kua baba, na kweli ndani ya mwezi January 2022 nikapata nafasi ya kua baba Kweli.

Girl friend wangu alijifungua salama Salmin mtoto imara wa kiume na nikajisikia faraja kiasi kikubwa kua baba. Niseme ukweli kuna raha ya kua baba ama kuitwa baba. Natamani sasa nipate mtoto mwingine kwa furaha niliyonayo.

Anyway, mimi nimekua bila baba, nilikulia kwa mjomba wangu ambae alinipigisha kwenye tanuru la moto hadi kufika hapa nilipofika. Mimi as long as niko hai nitahakikisha huyu bwana mdogo anapata mahitaji yake yote ya muhimu.

Kwa vile sipendi huu mfumo wetu wa elimu nitahakikisha anasoma either nje ya nchi ama ndani ya nchi lakini sio kwa mtaala wa NECTA huu unaoua thinking, reasoning na unaojaza watu vitu visivyo na msingi kwenye maisha karne hii ya 21.

Wababa wote hongereni, naomba mnikaribishe kwenye chama lenu kubwa.
 
Sawa karibu mwaka 2017 ulikuwa mwaka wangu .. sasa hivi mi kijana wangu tunapiga tu storz za mambo yanayoendelea huko Ukraine. Hongeraa...
 
Hongera. Utu uzima huo, usifurahie kuitwa baba pekee bali uje "What it takes to be Daddy not a Father"
 
Screenshot_20220303-203355.jpg
 
Na mimi mwezi wa nane nitakuwa baba wa watoto kadhaa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Nimegawa mimba kwa mabinti watatu Mungu akisaidia wakajifungua salama wazo la kuoa ndio bye-bye jumlaa.
 
Mwezi December 2021 nilileta hii
mada hapa kwamba natarajia kua baba, na kweli ndani ya mwezi January 2022 nikapata nafasi ya kua baba Kweli.

Girl friend wangu alijifungua salama Salmin mtoto imara wa kiume na nikajisikia faraja kiasi kikubwa kua baba.

Niseme ukweli kuna raha ya kua baba ama kuitwa baba. Natamani sasa nipate mtoto mwingine kwa furaha niliyonayo.

Anyway, mimi nimekua bila baba, nilikulia kwa mjomba wangu ambae alinipigisha kwenye tanuru la moto hadi kufika hapa nilipofika. Mimi as long as niko hai nitahakikisha huyu bwana mdogo anapata mahitaji yake yote ya muhimu.

Kwa vile sipendi huu mfumo wetu wa elimu nitahakikisha anasoma either nje ya nchi ama ndani ya nchi lakini sio kwa mtaala wa NECTA huu unaoua thinking, reasoning na unaojaza watu vitu visivyo na msingi kwenye maisha karne hii ya 21.

Wababa wote hongereni, naomba mnikaribishe kwenye chama lenu kubwa.
Big up kwa sana Chifu
 
Back
Top Bottom