Hatimaye nimepata kazi kupitia JF

Shida umesoma episodes bila kusoma comments
Ukawa unarukia episode mpya,unaskip comments.

Hayo yote uliyouliza,na mengine zaidi tulimuuliza na alishayajibu,tena na zaidi.
Rudi tena kasome ..comments pia ni nzuri sana.
Hujakosea, ni kweli nilisoma episode tu sijasoma comments

Hata hivyo sidhani kama swali la mwisho mlimuuliza[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Hongera kwa kufaulu Mkuu, japo mwenzetu ulikuwa na connection. Ile mitihani huwa ni kama wanatunga ya kukomoa!
 
Yote tulimuuliza[emoji23]
Nimemaliza kupitia comments zote ili nione hayo majibu. Ni kweli baadhi ya maswali mliuliza na amaeyajibu.

Lakini nimekuta maswali yangu mawili niliyouliza hamjayauliza.

Nilitaka kufahamu Dada B alipo kwa sasa, ninyi mumeishia kujadili msala alioupata, umahiri wa wale wazee wa Kibondo, Nguvu ya Kiroho ya kukemea ule mtego.

Pia nilitaka kufahamu alipotembelea Wilaya ya Singida Vijijini(maana kasema kila wilaya nchini kaikanyaga), alifika kijiji gani.
 
Ukiwa vizuri kupata koneksheni ni rahisi sana. Wanangu wote watafutaji mwiko kukata tamaa.

Hongera mkuu TAI DUME.
 
Hongera mkuu, laiti duniani ingekuwa hivi kwa wote basi dunia ingekuwa ni sehemu salama zaidi.

Nawe sambaza upendo huo uliopewa, saidia kadri ya uwezo wako unavyoruhusu, pesa ya ziada jitahidi sana kusaidia watu wenye mahitaji. Una mkuta mtu na jua kaliii hili anatembeza bidhaa, hali yake ukiiona unaona kabisa ni tete, huwezi nunua bidhaa mpe hata 200 ambayo kwako si kitu, kwake ina thamani kubwa. Buku kwako si kitu kuna mtu ni muhimu saana, unamuona mtoto nguo zake za shule hazitamaniki una elfu 20 saidia familia yake, dua zake ni faida hapa duniani na kesho ahera.
 
Wakuu samahani.kuna MTU anafanya kazi bandarini au anamfaham MTU yuko pale bandari ya DSM?
 
Na wewe ujitahidi kuwa binadamu sasa maana mavi-jana ya siku hizi hamchelewi kupandisha mabega! Kuwasaidia na wengine wanaohitaji kusaidiwa! Kumbuka ulikotoka!
 
Ama kweli utapata ulichokiijia JF, hongera sana.

All the best mkuu
 
Majukumu yallikuwa mengi hadi nimechelewa kuona huu uzi, hata nikipitia ule wa mwanzo nikawa sijaona mrejesho.

Hongera sana mkuu, kila la kheri kwenye majukumu yako mapya.
 
hongera mkuu, hakika hardwork pays, sasa tunakuomba na wewe uwe daraja kwa wengine mungu atakubariki sana akina sisi wa sosholoji na wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…