Hatimaye nimepata kazi kupitia JF

Hatimaye nimepata kazi kupitia JF

Shida umesoma episodes bila kusoma comments
Ukawa unarukia episode mpya,unaskip comments.

Hayo yote uliyouliza,na mengine zaidi tulimuuliza na alishayajibu,tena na zaidi.
Rudi tena kasome ..comments pia ni nzuri sana.
Hujakosea, ni kweli nilisoma episode tu sijasoma comments

Hata hivyo sidhani kama swali la mwisho mlimuuliza[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Wadau

Niliahidi hapa kwenye huu uzi wa Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa kwamba ikitokea nimepata sehemu ya kupiga kazi ningewajuza. nachukiua nafasi hii kuwafahamisha kwamba nimefanikiwa/bahatika/barikiwa kupata kazi kutokana na connection ya mdau mmoja aliyepitia huu uzi.

Kwa namna ya pekee napenda kumshukuru mdau huyo kwa kuonesha initiavies za kuniconnect na shirika husika na hatimaye nikafanikiwa kupata hiyo nafasi.

Jinsi ilivyokuwa.

Mdau (ni mdada) alinifata pm na kuniuliza kama ninayosimulia pamoja na CV ninayoweka mwishoni mwa kila episode kama zina ukweli au zina ukakasi. Nikamuhakikishia kwamba hakuna ukakasi wowotw na sina haja ya kudanganya personal life yangu. Akaniambia sawa anaendelea kufatilia stori yangu.

Wiki moja baada ya kumaliza stori yangu akanicheki tena pm kuniuliza kama nishapata job? Nikamwambia bado sijapafanikiwa na naendelea kupambana. Akaniuliza kama namba niliyoweka ni yangu na pia akaniomba email address yangu. Akaniahidi atawasiliana . Tukakubaliana hivyo.

Tarehe 25 Januari mwaka nikapokea email ikiwa imetumwa kwangu (forwarded) kutoka kwenye Shirika moja la kimataifa (Sio UN) likitangaza nafasi moja ya kazi lakini ilikuwa priority ni kwa internal staff. Wanaofanya kwenye haya mashirika yenye program zaidi ya moja wanaweza kunielewa hapa kwamba sometimes zikitokea nafasi za kazi zinatangazwa kwa staff waliopo na mara nyingi ni ngumu sana kwa mtu wa nje kujua kama kuna mchongo upo wazi.

Baada ya muda kidogo nikapokea simu (landline) ya lile shirika. Nikasikia sauti tamu sana ya kike ikiuliza kama mimi ndie Taidume? Kwa kihoro nikajibu ndio mimi. Basi akaniuliza kama nimeiona email. Nikamwambia nimeiona na ndio nilikuwa naendelea kuisoma. Basi akaniambia mimi ni yule mdau wa JF niliyekwambia tutawasiliana.

Kiufupi aliniuliza kama nina interest ya kuapply ile kazi na kama najiona nina uwezo wa kuifanya ile kazi. Nikamwambia ile nina interest nayo na ikitokea nimepata nina uwezo wa kuimudu bila shida. Akaniambia hata yeye anaimani ninaweza kuifanya based on CV, na kama nina interest ni apply haraka japo mimi sikuwa internal staff wa lile shirika lakini haitazuia mimi kuwa shortlisted endapo nitameet the job requirements.

Then akaniambia kwamba ile nafasi is similar na uzoefu niliokuwa nao na yeye ndiye aliyekuwa anaishikilia hiyo position ila alikuwa anaodoka kwenda sehemu nyingine by 1st March hatokuwepo. Hivyo walikuwa kwenye recruitment process yakupata mtu atayeendeleza pale yeye alipoishia. So akaniambia huo ndio msaada anaoweza kunipa mengine ni juu yangu mwenyewe.

Nilimshuru sana na tukaagana kwa makubaliano kwamba kilichobaki ni upande wangu kukamilisha, yaani niaandae documents zangu vizuri na nisubmitt application kwa wakati. Kweli siku hiyo hiyo nilifanikiwa kuapply kupitia job application link ambayo iliwekwa pale. (Ni zile kazi unazoapply online kupitia system za shirika husika).

Baada ya siku kama tisa nikapokea email kwamba nimekuwa shortilisted for online written interview that it was supposed to be conducted on the following day. Nikacomfirm kufanya ile interviewna nikaifanya siku inayofata. Huwa wanatuma kwenye email lakini wanamechanism zao za kumonitor kama unacheat (plagiarism software) na pia mda wote unatakiwa camera iwe on - kaazi kweli kweli.

Basi nikapiga ile written na baada ya siku kama tatu hivi nipokea email pamoja na simu ya landline za ofisi ile ile (mara hii ikitoka kwa admn)kwamba nimequalify for the second stage, an oral interview. Nilitakiwa ku opt the interview modality kama iwe online through zoom, TEAMS or what ever au kwenda ofisini kwao. Nikaona hawa wastake kunizungua, maswala ya online interview yana changamoto zake mara bando likate au usikivu ukawa duni, nikaamua kuopt kwenda ofisini kwao. Basi nikapangiwa tarehe ya kwenda kwenye oral interview ilikuwa siku tatu mbele.

Sasa nikawa nasubiri simu ya yule dada mwenye sauti tamu kwa hamu anipigie pengine hata nimshukuru kwa hatua ile lakini hakunipigia. Na nisingeweza kumpigia mimi kwa ile landline maana its not professional, japo kumpata ningeweza maana title ya kazi yake nilikuwa naijua maana ndio hio niliyoapply mimi.

Basi siku ya interview ikafika na I was there in time. Procedure zote zikafuatwa hatimaye nikaingia kwenye chumba cha hukumu na kujitetea au wengine wanasema kwenye chumba cha kujiuza ili ununuliwe. Kama mnavyojua kwenye interview kuna ile panelists kujitambulisha basi nikawa makini sana kumjua yule dada wa JF maana walikuwa madada watatu na wanaume wawili. Nikajua akijitambulisha kwa ile position niliyoomba ndio angekuwa yeye. Mpaka wote wanamaliza kujitambulisha sikusikia mwenye ile position, I was a little bit unhappy baada ya kujua connector wangu hayupo pale. Basi nikapiga interview nikasepa zangu.

Huwezi amini on the same day kabla hata sijafika home nikapokea simu kutoka kwenye lile shirika wakiniuliza kama ninaweza kurudi tena pale kesho yake ili tunegotiate baadhi mambo na kuona kama tutaweza kukubaliana for the next employment procedure. Nikasema why not, hata mngesema sasahivi ningegegeuza. Basi tukakubalina kesho yake saa nne asubuhi niende.

Kweli kesho yake nilifika mapema tuu mpaka yule admn akanishangaa nimewahi sana. baada ya muda nikapelekwa kwa HR manager tukaongea ya kukubalina na nikapewa offer letter ambapo nilitakiwa niisaini ndani ya siku mbili kama I accept the offer or otherwise. Mimi sikusubiri nilisaini pale pale na kupata copy yangu. Baadae wakaniuliza kama ninaweza kunza kazi immediately na wakaniomba kama sitojali nikaripoti ndani ya wiki. Basi tukakubaliana pale kureport mapema iwezekanavyo kwa ajili ya orientation na handover from the leaving staff.

Kweli Jumatatu ya tar 19 Feb nikaripoti, nikapokelewa na nikakabidhiwa kwa staff ambaye ndie alikuwa anaondoka kwa orientation na makabidhiano. So I met connector wangu na sitosahau the greeting from from her was "Hello Taidume, congratulation and welcome" kwa sauti ile ile tamu. (TAFADHALI SITAKI MASWALI YENU HAPA KUHUSU NA HUYU DADA NAJUA MNACHOTAKA KUULIZIA - SITOWAJIBU)

Basi nikakabidhiwa rasmi kwake na akaniorient vizuri sana kwa muda wa wiki nzima na akahandiover kazi kwangu smoothly. So rasmi nimeanza majukumu ya kazi mpya tangu tar 1 March this year,

Hakika nimeiona nguvu ya JF kwenye hili, naomba MUNGU awakirimu mara dufu zaidi wale wote wanaotumia muda, nguvu, rasilimali, akili na nafasi zao katika kuwasapoti wengine wenye uhitaji.

Nawashukuru pia wale wote walionishauri au kutoa michango yao kwenye huu uzi hapa jukwaani na pm pia. Wengi nimefahamiana nao kupitia uzi huu and I appreciate your valuable time for connecting with me. Bila kusahau wale wazee wakejeli hahaha I appreciate guuys.

BLESSED
Hongera kwa kufaulu Mkuu, japo mwenzetu ulikuwa na connection. Ile mitihani huwa ni kama wanatunga ya kukomoa!
 
Yote tulimuuliza[emoji23]
Nimemaliza kupitia comments zote ili nione hayo majibu. Ni kweli baadhi ya maswali mliuliza na amaeyajibu.

Lakini nimekuta maswali yangu mawili niliyouliza hamjayauliza.

Nilitaka kufahamu Dada B alipo kwa sasa, ninyi mumeishia kujadili msala alioupata, umahiri wa wale wazee wa Kibondo, Nguvu ya Kiroho ya kukemea ule mtego.

Pia nilitaka kufahamu alipotembelea Wilaya ya Singida Vijijini(maana kasema kila wilaya nchini kaikanyaga), alifika kijiji gani.
 
Ukiwa vizuri kupata koneksheni ni rahisi sana. Wanangu wote watafutaji mwiko kukata tamaa.

Hongera mkuu TAI DUME.
 
Hongera mkuu, laiti duniani ingekuwa hivi kwa wote basi dunia ingekuwa ni sehemu salama zaidi.

Nawe sambaza upendo huo uliopewa, saidia kadri ya uwezo wako unavyoruhusu, pesa ya ziada jitahidi sana kusaidia watu wenye mahitaji. Una mkuta mtu na jua kaliii hili anatembeza bidhaa, hali yake ukiiona unaona kabisa ni tete, huwezi nunua bidhaa mpe hata 200 ambayo kwako si kitu, kwake ina thamani kubwa. Buku kwako si kitu kuna mtu ni muhimu saana, unamuona mtoto nguo zake za shule hazitamaniki una elfu 20 saidia familia yake, dua zake ni faida hapa duniani na kesho ahera.
 
Wakuu samahani.kuna MTU anafanya kazi bandarini au anamfaham MTU yuko pale bandari ya DSM?
 
Wadau

Niliahidi hapa kwenye huu uzi wa Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa kwamba ikitokea nimepata sehemu ya kupiga kazi ningewajuza. nachukiua nafasi hii kuwafahamisha kwamba nimefanikiwa/bahatika/barikiwa kupata kazi kutokana na connection ya mdau mmoja aliyepitia huu uzi.

Kwa namna ya pekee napenda kumshukuru mdau huyo kwa kuonesha initiavies za kuniconnect na shirika husika na hatimaye nikafanikiwa kupata hiyo nafasi.

Jinsi ilivyokuwa.

Mdau (ni mdada) alinifata pm na kuniuliza kama ninayosimulia pamoja na CV ninayoweka mwishoni mwa kila episode kama zina ukweli au zina ukakasi. Nikamuhakikishia kwamba hakuna ukakasi wowotw na sina haja ya kudanganya personal life yangu. Akaniambia sawa anaendelea kufatilia stori yangu.

Wiki moja baada ya kumaliza stori yangu akanicheki tena pm kuniuliza kama nishapata job? Nikamwambia bado sijapafanikiwa na naendelea kupambana. Akaniuliza kama namba niliyoweka ni yangu na pia akaniomba email address yangu. Akaniahidi atawasiliana . Tukakubaliana hivyo.

Tarehe 25 Januari mwaka nikapokea email ikiwa imetumwa kwangu (forwarded) kutoka kwenye Shirika moja la kimataifa (Sio UN) likitangaza nafasi moja ya kazi lakini ilikuwa priority ni kwa internal staff. Wanaofanya kwenye haya mashirika yenye program zaidi ya moja wanaweza kunielewa hapa kwamba sometimes zikitokea nafasi za kazi zinatangazwa kwa staff waliopo na mara nyingi ni ngumu sana kwa mtu wa nje kujua kama kuna mchongo upo wazi.

Baada ya muda kidogo nikapokea simu (landline) ya lile shirika. Nikasikia sauti tamu sana ya kike ikiuliza kama mimi ndie Taidume? Kwa kihoro nikajibu ndio mimi. Basi akaniuliza kama nimeiona email. Nikamwambia nimeiona na ndio nilikuwa naendelea kuisoma. Basi akaniambia mimi ni yule mdau wa JF niliyekwambia tutawasiliana.

Kiufupi aliniuliza kama nina interest ya kuapply ile kazi na kama najiona nina uwezo wa kuifanya ile kazi. Nikamwambia ile nina interest nayo na ikitokea nimepata nina uwezo wa kuimudu bila shida. Akaniambia hata yeye anaimani ninaweza kuifanya based on CV, na kama nina interest ni apply haraka japo mimi sikuwa internal staff wa lile shirika lakini haitazuia mimi kuwa shortlisted endapo nitameet the job requirements.

Then akaniambia kwamba ile nafasi is similar na uzoefu niliokuwa nao na yeye ndiye aliyekuwa anaishikilia hiyo position ila alikuwa anaodoka kwenda sehemu nyingine by 1st March hatokuwepo. Hivyo walikuwa kwenye recruitment process yakupata mtu atayeendeleza pale yeye alipoishia. So akaniambia huo ndio msaada anaoweza kunipa mengine ni juu yangu mwenyewe.

Nilimshuru sana na tukaagana kwa makubaliano kwamba kilichobaki ni upande wangu kukamilisha, yaani niaandae documents zangu vizuri na nisubmitt application kwa wakati. Kweli siku hiyo hiyo nilifanikiwa kuapply kupitia job application link ambayo iliwekwa pale. (Ni zile kazi unazoapply online kupitia system za shirika husika).

Baada ya siku kama tisa nikapokea email kwamba nimekuwa shortilisted for online written interview that it was supposed to be conducted on the following day. Nikacomfirm kufanya ile interviewna nikaifanya siku inayofata. Huwa wanatuma kwenye email lakini wanamechanism zao za kumonitor kama unacheat (plagiarism software) na pia mda wote unatakiwa camera iwe on - kaazi kweli kweli.

Basi nikapiga ile written na baada ya siku kama tatu hivi nipokea email pamoja na simu ya landline za ofisi ile ile (mara hii ikitoka kwa admn)kwamba nimequalify for the second stage, an oral interview. Nilitakiwa ku opt the interview modality kama iwe online through zoom, TEAMS or what ever au kwenda ofisini kwao. Nikaona hawa wastake kunizungua, maswala ya online interview yana changamoto zake mara bando likate au usikivu ukawa duni, nikaamua kuopt kwenda ofisini kwao. Basi nikapangiwa tarehe ya kwenda kwenye oral interview ilikuwa siku tatu mbele.

Sasa nikawa nasubiri simu ya yule dada mwenye sauti tamu kwa hamu anipigie pengine hata nimshukuru kwa hatua ile lakini hakunipigia. Na nisingeweza kumpigia mimi kwa ile landline maana its not professional, japo kumpata ningeweza maana title ya kazi yake nilikuwa naijua maana ndio hio niliyoapply mimi.

Basi siku ya interview ikafika na I was there in time. Procedure zote zikafuatwa hatimaye nikaingia kwenye chumba cha hukumu na kujitetea au wengine wanasema kwenye chumba cha kujiuza ili ununuliwe. Kama mnavyojua kwenye interview kuna ile panelists kujitambulisha basi nikawa makini sana kumjua yule dada wa JF maana walikuwa madada watatu na wanaume wawili. Nikajua akijitambulisha kwa ile position niliyoomba ndio angekuwa yeye. Mpaka wote wanamaliza kujitambulisha sikusikia mwenye ile position, I was a little bit unhappy baada ya kujua connector wangu hayupo pale. Basi nikapiga interview nikasepa zangu.

Huwezi amini on the same day kabla hata sijafika home nikapokea simu kutoka kwenye lile shirika wakiniuliza kama ninaweza kurudi tena pale kesho yake ili tunegotiate baadhi mambo na kuona kama tutaweza kukubaliana for the next employment procedure. Nikasema why not, hata mngesema sasahivi ningegegeuza. Basi tukakubalina kesho yake saa nne asubuhi niende.

Kweli kesho yake nilifika mapema tuu mpaka yule admn akanishangaa nimewahi sana. baada ya muda nikapelekwa kwa HR manager tukaongea ya kukubalina na nikapewa offer letter ambapo nilitakiwa niisaini ndani ya siku mbili kama I accept the offer or otherwise. Mimi sikusubiri nilisaini pale pale na kupata copy yangu. Baadae wakaniuliza kama ninaweza kunza kazi immediately na wakaniomba kama sitojali nikaripoti ndani ya wiki. Basi tukakubaliana pale kureport mapema iwezekanavyo kwa ajili ya orientation na handover from the leaving staff.

Kweli Jumatatu ya tar 19 Feb nikaripoti, nikapokelewa na nikakabidhiwa kwa staff ambaye ndie alikuwa anaondoka kwa orientation na makabidhiano. So I met connector wangu na sitosahau the greeting from from her was "Hello Taidume, congratulation and welcome" kwa sauti ile ile tamu. (TAFADHALI SITAKI MASWALI YENU HAPA KUHUSU NA HUYU DADA NAJUA MNACHOTAKA KUULIZIA - SITOWAJIBU)

Basi nikakabidhiwa rasmi kwake na akaniorient vizuri sana kwa muda wa wiki nzima na akahandiover kazi kwangu smoothly. So rasmi nimeanza majukumu ya kazi mpya tangu tar 1 March this year,

Hakika nimeiona nguvu ya JF kwenye hili, naomba MUNGU awakirimu mara dufu zaidi wale wote wanaotumia muda, nguvu, rasilimali, akili na nafasi zao katika kuwasapoti wengine wenye uhitaji.

Nawashukuru pia wale wote walionishauri au kutoa michango yao kwenye huu uzi hapa jukwaani na pm pia. Wengi nimefahamiana nao kupitia uzi huu and I appreciate your valuable time for connecting with me. Bila kusahau wale wazee wakejeli hahaha I appreciate guuys.

BLESSED
Na wewe ujitahidi kuwa binadamu sasa maana mavi-jana ya siku hizi hamchelewi kupandisha mabega! Kuwasaidia na wengine wanaohitaji kusaidiwa! Kumbuka ulikotoka!
 
Ama kweli utapata ulichokiijia JF, hongera sana.

All the best mkuu
 
Majukumu yallikuwa mengi hadi nimechelewa kuona huu uzi, hata nikipitia ule wa mwanzo nikawa sijaona mrejesho.

Hongera sana mkuu, kila la kheri kwenye majukumu yako mapya.
 
hongera mkuu, hakika hardwork pays, sasa tunakuomba na wewe uwe daraja kwa wengine mungu atakubariki sana akina sisi wa sosholoji na wengine
 
Back
Top Bottom