Mourinho akakiri kabisa hajawah kutana na mchezaji anayempa wakat mgumu ktk mbinu kumkaba km Lionel Messi.
Anasema Messi ni mashine ile sio mtu wa kawaida.
Baada ya kuitoa Barca UEFA, Mourinho alisifika saana kwa kusuka timu, akawekewa dau zito na Perez wa Madrid ili kuja kuukomesha utawala wa Barca ya Messi.
Mourinho akachukua timu, timu ikiwa na Ramos, Pepe, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso, Ozil, Di Maria, Benzema, Ronaldo na golini akiwa kipa namba moja wa Spain, Iker Casillas.
Derby ya kwanza kabisa pale Spain kwa msimu huo ilipigwa pale Camp Nou. Barca wakiwa na Iniesta, Xavi, Messi, Villa na Pedro. Wala Barca hawakuwa na washambuliaji wakali sana pale mbele zaidi ya Villa na Messi, hata benchi hawakuwa na watu wa kazi.
Mourinho na Madrid yake walijipanga saan kumzuia Messi, mwisho wa siku Madrid anakufa 5 bila, hata kona hakupata. Goli zote hizo zimesababishwa na Messi. Messi alikuwa anamchukua Pepe, Khedira na takataka zingine anaziburuza kisha anamtafuta Pedro au Villa, watu wanaweka mpira wavuni.
Nenda Youtube katafute hii game. Andika Barca 5 madrid 0.