GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Baada ya kufariki kwa kushtukiza kwa rapa namba mbili wa Wenge BCBG yake JB Mpiana aitwae Faustine Nzinga Yankobo (jina la Kimuziki CELLULAIRE) ilichukua muda mrefu kumpata mrithi wa kumsaidia rapa (Atalaku) Kiongozi Pitshou Lisimo ( jina la Kimuziki GENTAMYCINE ) ila kwa sasa ameshapatikana.
Huku ikiamimika kuwa waliokuwa marapa (Atalakus) wa kikosi cha pili cha Wenge BCBG akina Pajo na mwenzake Bin Laden wangeziba pengo ilishindikana mpaka alipopatikana rasmi Atalaku (Rapa) mpya na hatari aitwae Fusse De Guere (kombora la vitani) ambaye kiukweli anafanya vyema na hata kumtishia Mkuu wake wa Kurapu katika Bendi ya Wenge BCBG aitwae GENTAMYCINE.
Na kikubwa kinachomfanya huyu Rapa (Atalaku) mpya Wenge BCBG Fusee De Guere kuwa tishio na kupendwa ni kutokana na kukulia (Kupikwa) na mwanzilishi wa Atalaku (Kurapu) kwa sauti tamu na ya kipekee Yombo Lumbu (jina la kimuziki Tutu Caludji ) ambaye ana chuo maalum cha kutengeneza marapa (Atalakus) huko Congo DR ambapo pia amewatoa Atalakus (Marapa) kama Theo Mbala aliyekuwa kwa marehemu Madilu System, Celeo aliyekuwa kwa Werrason na Kirikiou aliyekuwa kwa Koffi Olomide.
Kwa wale wapenzi wenzangu wa Wenge BCBG yake JB Mpiana mnaotaka kuuona moto wa huyu Atalaku ( Rapa ) mpya wa Wenge BCBG aitwae Fusse De Guere tafuteni sebene (Live) iitwayo JB Mpiana Azo Preparer Generique ya Somo kisha tafuteni na wimbo wa Je ne te Calcule Pas kisha mje mnipe mirejesho yenu hapa.
Long Live Wenge BCBG,
Long Live JB Mpiana,
Long Live Atalaku GENTAMYCINE,
Ukitaka raha tu njoo Wenge BCBG!