Hatimaye Rapa (Atalaku), (Pitshou Lisimo) wa Wenge BCBG ampata Msaidizi wake Tishio Fusee De Guere

Hatimaye Rapa (Atalaku), (Pitshou Lisimo) wa Wenge BCBG ampata Msaidizi wake Tishio Fusee De Guere

Kuna changamoto ya afya ya akili hapa bila shaka
 
Hivi Werrason na JB Ni kweli waliungana kurudisha kundi upya na vp Kuna album iliyotoka ua pamoja?
Umeenda Google au Umeingia katika Kurasa zao za Kimitandao za Bendi zao Wenge BCBG yake JB Mpiana na Wenge Maison Mere yake Werrason na ukakosa Jibu la Swali lako hili?
 
Sema coco lisimo saivi vocal inakwangua sana mshauri apige mayai mabichi na asali kwa wingi
 
Baada ya kufariki kwa kushtukiza kwa rapa namba mbili wa Wenge BCBG yake JB Mpiana aitwae Faustine Nzinga Yankobo (jina la Kimuziki CELLULAIRE) ilichukua muda mrefu kumpata mrithi wa kumsaidia rapa (Atalaku) Kiongozi Pitshou Lisimo ( jina la Kimuziki GENTAMYCINE ) ila kwa sasa ameshapatikana.

Huku ikiamimika kuwa waliokuwa marapa (Atalakus) wa kikosi cha pili cha Wenge BCBG akina Pajo na mwenzake Bin Laden wangeziba pengo ilishindikana mpaka alipopatikana rasmi Atalaku (Rapa) mpya na hatari aitwae Fusse De Guere (kombora la vitani) ambaye kiukweli anafanya vyema na hata kumtishia Mkuu wake wa Kurapu katika Bendi ya Wenge BCBG aitwae GENTAMYCINE.

Na kikubwa kinachomfanya huyu Rapa (Atalaku) mpya Wenge BCBG Fusee De Guere kuwa tishio na kupendwa ni kutokana na kukulia (Kupikwa) na mwanzilishi wa Atalaku (Kurapu) kwa sauti tamu na ya kipekee Yombo Lumbu (jina la kimuziki Tutu Caludji ) ambaye ana chuo maalum cha kutengeneza marapa (Atalakus) huko Congo DR ambapo pia amewatoa Atalakus (Marapa) kama Theo Mbala aliyekuwa kwa marehemu Madilu System, Celeo aliyekuwa kwa Werrason na Kirikiou aliyekuwa kwa Koffi Olomide.

Kwa wale wapenzi wenzangu wa Wenge BCBG yake JB Mpiana mnaotaka kuuona moto wa huyu Atalaku ( Rapa ) mpya wa Wenge BCBG aitwae Fusse De Guere tafuteni sebene (Live) iitwayo JB Mpiana Azo Preparer Generique ya Somo kisha tafuteni na wimbo wa Je ne te Calcule Pas kisha mje mnipe mirejesho yenu hapa.

Long Live Wenge BCBG,

Long Live JB Mpiana,

Long Live Atalaku GENTAMYCINE,
Nilimkubali sana coco lisimo kwenye wimbo LE BARON utunzi wake JD LOKO kauwa sana mule
Ukitaka raha tu njoo Wenge BCBG
 
Sema coco lisimo saivi vocal inakwangua sana mshauri apige mayai mabichi na asali kwa wingi
Haitwi Coco Lisimo bali anaitwa Pitshou Lisimo ( jina la Kimuziki au Kazi ni GENTAMYCINE ) na huyo Coco Lisimo ambaye karibu katika Rapu zake humuimba ni Kaka yake mkubwa na ndiyo aliyemlea ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Congo DR.
 
Nilimkubali sana coco lisimo kwenye wimbo LE BARON utunzi wake JD LOKO kauwa sana mule
Haitwi Coco Lisimo bali anaitwa Pitshou Lisimo ( jina la Kimuziki au Kazi ni GENTAMYCINE ) na huyo Coco Lisimo ambaye karibu katika Rapu zake humuimba ni Kaka yake mkubwa na ndiyo aliyemlea ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Congo DR.
 
Haitwi Coco Lisimo bali anaitwa Pitshou Lisimo ( jina la Kimuziki au Kazi ni GENTAMYCINE ) na huyo Coco Lisimo ambaye karibu katika Rapu zake humuimba ni Kaka yake mkubwa na ndiyo aliyemlea ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Congo DR.
Hivi mkuu kuna ukweli wowote kwamba mwimbajia wa wenge bcbg JULES KIBENS ni professor na nje ya muziki ni mwalimu wa chuo kikuu huko drc?
 
Hivi mkuu kuna ukweli wowote kwamba mwimbajia wa wenge bcbg JULES KIBENS ni professor na nje ya muziki ni mwalimu wa chuo kikuu huko drc?
Absolutely Big Yes Mkuu kuwa Jules Kibens ( a.k.a Molongeshi ) ni Mwalimu ( Le Professeur ) Kitaaluma na kabla ya kutua Wenge BCBG alikuwa akifundisha Chuo Kikuu Congo DR Somo la Lugha ya Kifaransa aliyoibobea mno.

Kwa sasa Jules Kibens ndiyo Kiongozi wa Wanamuziki ( Artiste Director ) wa Bendi ya Wenge BCBG huku Mkurugenzi wa Bendi akiwa ni Mpiga Drums ( Mkaanga Chips ) Hatari Seguen Mignon Maniata huku Rais na Mmiliki wa Bendi akiwa ni Mwenyewe Jean Bedele Tshituka Mpiana.

Kwa sasa 99% ya Nyimbo zote za Bendi ya Wenge BCBG zikitungwa ni lazima zipitie kwa Fundi wa Lugha Jules Kibens ili aziweke sawa na ashauri maneno ya Kutumia na ndiyo maana ukitaka kukisikia Kifaransa cha ndani kabisa Sikiliza Nyimbo za Wenge BCBG.

Kila la Kheri.
 
Back
Top Bottom